Haya maneno bado yapo vyuoni? Wazee wa Madesa, Simbi, Vizenga, Missile, Bombshell. Simulizi waliokamatwa au kushuhudia matukio wakati wa UE

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,417
11,071
Hello lads and ladies.

Legends!

Tupitie flashbacks zetu tukiwa campus notes zina majina yake, vikaratasi vya kuibia majibu kwenye Tests na UE na majina yake.

Wakali wa vizenga, dessa, simbi kwenye soksi , chooni, network collabo za chooni, signal kama zote. Wale ambao hawakuwahi kutumia desa au kuomba majibu Kwa majirani wote. Wasomea kijiji na makanisa karibuni.

Mimi kazi yangu ilikuwa kuwasumbua wasimamizi ili washikaji wapate muda wa kuibiana.

Flow your flashbacks here.

Kuna wenye umaarufu wao. Mkali wa coursework, Mkali wa UE, Mzee wa kubalance, mfuasi wa sup, bila sup anaumwa.

Wadiz
 
Ahahahahaaa umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa FoE (siku hizi COeT) tunafanya UE pale A4 kama sijakosea. Dr. Mvungi wakati huo ndo anatusimamia. Kuna mwamba alikuwa anaitwa Stephano, alikuwa na desa lake analitumia. Wakati huo Mvungi yupo kwenye ngazi za kuelekea juu kwenye ofisi za mkuu wa idara ya umeme.

Si akamwona mwamba anadesa. Akashuka fasta. Jamaa akachukua karatasi tupu akaifinyanga na kuitupa dirishani kwa nje. Mvungi akaiwahi I karatasi, kumbe tupu. Jamaa akalimeza desa lake. Ushahidi ukapotea.
 
Kuna kitu nilishindwa kabisa kwenye chumba cha mtihani. CHEATING ya aina yeyote ile nilikua siwezi, nakumbuka kuna pepa nikaingilia kijiji cha watu nikapewa sharti la kutoa majibu mbele kupeleka nyuma, nilishindwa wale wa nyuma yangu wote walipata sup 😁. Kuanzia hapo nikawa nakimbiwa
 
Ahahahahaaa umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa FoE (siku hizi COeT) tunafanya UE pale A4 kama sijakosea. Dr. Mvungi wakati huo ndo anatusimamia. Kuna mwamba alikuwa anaitwa Stephano, alikuwa na desa lake analitumia. Wakati huo Mvungi yupo kwenye ngazi za kuelekea juu kwenye ofisi za mkuu wa idara ya umeme.

Si akamwona mwamba anadesa. Akashuka fasta. Jamaa akachukua karatasi tupu akaifinyanga na kuitupa dirishani kwa nje. Mvungi akaiwahi I karatasi, kumbe tupu. Jamaa akalimeza desa lake. Ushahidi ukapotea.
 
Ahahahahaaa umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa FoE (siku hizi COeT) tunafanya UE pale A4 kama sijakosea. Dr. Mvungi wakati huo ndo anatusimamia. Kuna mwamba alikuwa anaitwa Stephano, alikuwa na desa lake analitumia. Wakati huo Mvungi yupo kwenye ngazi za kuelekea juu kwenye ofisi za mkuu wa idara ya umeme.

Si akamwona mwamba anadesa. Akashuka fasta. Jamaa akachukua karatasi tupu akaifinyanga na kuitupa dirishani kwa nje. Mvungi akaiwahi I karatasi, kumbe tupu. Jamaa akalimeza desa lake. Ushahidi ukapotea.
Huyo engineer wa UE🤣🤣🤣
 
kuna mwana UE anaingia na simu anaweka laini ambayo hakuna mtu yoyote anaijua ikiwa na bundle la maana. hapo ni ku Google tu.
 
Kuna mwamba mmoja aliandika majibu kwenye feni (panga boy) juu ya ceiling. Akawa ana desa fresh sangapi joto likawa kali ikawashwa feni mwana akaanza kuzungusha kichwa kama feni inavyozunguka mpaka msimamizi akaomba msaada kuwa kuna mtahiniwa kapandwa na majini.
 
Hello lads and ladies.

Legends!!

Tupitie flashbacks zetu tukiwa campus notes zina majina yake, vikaratasi vya kuibia majibu kwenye Tests na UE na majina yake.

Wakali wa vizenga, dessa, simbi kwenye soksi , chooni, network collabo za chooni, signal kama zote. Wale ambao hawakuwahi kutumia desa au kuomba majibu Kwa majirani wote. Wasomea kijiji na makanisa karibuni.

Mimi kazi yangu ilikuwa kuwasumbua wasimamizi ili washikaji wapate muda wa kuibiana.

Flow your flashbacks here.

Kuna wenye umaarufu wao
Mkali wa coursework, Mkali wa UE, Mzee wa kubalance, mfuasi wa sup, bila sup anaumwa.

Wadiz
Simbi ilikuwa commona sana SUA sijui siku hizi!!!!
Neno simbi ni kutoka neno Symbiosis.

Maana yake

Symbiosis, any of several living arrangements between members of two different species, including mutualism, commensalism, and parasitism. Both positive (beneficial) and negative (unfavourable to harmful) associations are therefore included, and the members are called symbionts.
 
Umetisha Mzee wa Dark city na kididimo, Vipi kwa Sisco
 
Ahahahahaaa umenikumbusha mbali sana.

Tulikuwa FoE (siku hizi COeT) tunafanya UE pale A4 kama sijakosea. Dr. Mvungi wakati huo ndo anatusimamia. Kuna mwamba alikuwa anaitwa Stephano, alikuwa na desa lake analitumia. Wakati huo Mvungi yupo kwenye ngazi za kuelekea juu kwenye ofisi za mkuu wa idara ya umeme.

Si akamwona mwamba anadesa. Akashuka fasta. Jamaa akachukua karatasi tupu akaifinyanga na kuitupa dirishani kwa nje. Mvungi akaiwahi I karatasi, kumbe tupu. Jamaa akalimeza desa lake. Ushahidi ukapotea.
Mwamba huyo huyo alikuwa na kipaji cha kuandika fasta sana. Tukiingia naye kwenye test, yeye anagawa tu maswali. Utamsikia Bantu Lady nisaidie swali la kwanza, Evelyn Salt nisaidie swali la pili, Mshana Jr nisaidie swali la tatu, mpaka yote yaishe. Sasa akiarudishiwa majibu anaandika fasta kama mashine. Sasa ile mara ya kwanza si akawa wa kwanza..!!! Akaanza kutamba kwamba darasa lina vilaza hadi yeye anakuwa wa kwanza..!!! KWANI ALISAIDWA TENA.!!
 
Kuna mwamba aliona ya kazi gani akaingia na simu ni mwendo kutype maswali tu message za majibu zinarudi upendo unasambazwa.Mpumbavu yule akakosea step simu ikatoa mlio.Ulipigwa msako kwenye ile zone ,hakuna simu ilipatikana.Yule mpiga msako kosa alilofanya alianzia juu akaacha soksi,kumbe lijamaa limeisunda kwenye soksi anarudi kukagua soksi kumbe jamaa kaibana kwenye kiuno na mkanda.Lilisevu ila lilikoma kabisa kuingia na vibomu.
 
Back
Top Bottom