Haya magroup ya shule mmlishamaliza shule miaka yapata 12. mnachangishana Hivi mimi ndiye nawaza negative?

Annie X6

JF-Expert Member
Mar 16, 2023
405
750
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
 
ONgeza nyama kidogo
 
Hata kama si fraud.

Mimi labda naamini sana watu kwenye misiba, sasa fraud inakujaje?.

Mtu anamuua mzazi ili mumchangie? Watu wanaenda kumkabidhi mfiwa rambirambi kwenye msiba, ina maana mfiwa ana fake msiba ili apewe rambirambi au fraud inakuwaje hapo?

Kwangu suala la fraud silioni sana.

Ila, hata kama si fraud, tujitengenezee utamaduni mwingine wa kujiwekea akiba na kujitosheleza wenyewe bila kuchangishanachangishana kila inapotokea msiba.

Kuna watu wengine sio big deal, kuna watu wengine mnawaumiza kwa michango ya kila mara. Hata ikiwa michango ni ya hiyari, kwenye macho ya wengi watu wanaona haya.

Pia, mimi nina allergy na vimichangomichango ya kila mara, inabidi watu wawe na fund ya kutoa pesa haraka hata kama inahitajika kwa dharula. Sasa hivi vimichango mpaka watu watafutane, wafukuzane, wahimizane, tarehe zikiwa mbaya mpaka wasubiri mwisho wa mwezi, karaha tupu.

Afadhali hata kuchanga kwenye mfuko kwa mwaka mzima. Halafu misiba ikitokea mna fixed amount mnaweza kutoa kwa kila member.

Mfuko kama huu utaondoa matatizo kama ya mtu kuchangia wengine na kutochangia wengine, jambo ambalo mara nyingine linaleta mgawanyiko.

Hivi kwa nini watu kama wa bima wasichangamkie watu kukata bima ya maisha? Kuna bima mpaka za vikundi, hivi vikundi vya shule havijui hii bima? Au hizi bima zina matatizo ambayo mimi ndiye siyajui?

Au ndiyo utamaduni wetu kuchangishana watu wajione wako pamoja? Maana kuna jamaa yangu mmoja alikataa kuchangiwa harusi, akasema kama kuna mtu anataka kuchangia harusi yake achangie kijiji cha Wamasai wapate maji, kwa ni nzuri tu asiwape watu mzigo wa kuchanga.

Lakini, kikichotokea ni kwamba, kuna watu walimsema kuwa anaringa na anajiona anaweza kumaliza gharama za harusi yake peke yake bila ya kuwapa watu nafasi ya kuchangia.

Wamakonde walisema "Ukichimama.nchale, ukikimbia nchale".

Ukichangisha lawama. Usipochangisha lawama.
 
Mambo mengine ni ya hiyari chukua hatua usilalamike
Mkuu,

Hakuna hiyari ikiwa kuna kiranja ana ki Excel spreadsheet anahesabu nani kachangia mara ngapi. Huo ni mfumo wa nipe nikupe tu.

Yani hata ukisema mimi sichangi, we have to do better, unakuwa unahesabiwa mchawi hutaki kuchangia watu. You become a social outcast.

Sasa hapo hiyari iko wapi?

Hiyari yenye social cost si hiyari hiyo.

Mimi bora hata uniambie kuna mfuko wa kuchangia kwa mwaka naweza kuwa mwepesi kuliko hivi vimichango vya ad hoc naviona viko kushoto kweli. Ingawa nachangia kwa kiasi changu bado.

Yani naona ni kama alama ya umasikini najiingiza humo.
 
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
Kwani huwa unashurtishwa kuchanga??

Nimejiwekea desturi moja sitaki group la chochote kwenye simu yangu ambalo halina maslahi ya moja kwa moja kwangu.

Nikimuhitaji school mate nitamtafuta individually, sio matangazo ya kwenye group.

Athari kubwa ya haya magroup ni kujipa unnecessary pressure ya maisha in the sense kwamba watu wamefanikiwa kwa tofauti kimaisha.

Unaweza aidha ukajikuta unahoji uwepo wako duniani kwa kuona wenzio wa rika sawa wamepiga hatua kubwa kuliko wewe ama ku attract attention/vizinga na vijicho kutoka kwa wale watakaohisi umewazidi kimaisha.
 
Hata kama si fraud (mimi labda naamini sana watu kwenye misiba, sasa fraud inakujaje, mtu anamuua mzazi ili mumchangie?) hata kama si fraud, tujitengenezee utamaduni mwingine wa kujiwekea akiba na kujitosheleza wenyewe bila kuchangishanachangishana kila inapotokea msina.

Kuna watu wengine sio big deal, kuna watu wengine mnawaumiza kwa michango ya kila mara. Hata ikiwa michango ni ya hiyari, kwenye macho ya wengi watu wanaona haya.

Pia, mimi nina allergy na vimichangomichango ya kila mara, inabidi watu wawe na fund ya kutoa pesa haraka hata kama inahitajika kwa dharula. Sasa hivi vimichango mpaka watu watafutane, wafukuzane, wahimizane, tarehe zikiwa mbaya mpaka wasubiri mwisho wa mwezi, karaha tupu.

Afadhali hata kuchanga kwenye mfuko kwa mwaka mzima. Halafu misiba ikitokea mna fixed amount mnaweza kutoa kwa kila member.

Hivi kwa nini watu kama wa bima wasichangamkie watu kukata bima ya maisha? Kuna bima mpaka za vikundi, hivi vikundi vya shule havijui hii bima?

Au ndiyo utamaduni wetu kuchangishana watu wajione wako pamoja? Maana kuna jamaa yangu mmoja alikataa kuchangiwa harusi, akasema kama kuna mtu anataka kuchangia harusi yake achangie kijiji cha Wamasai wapate maji, kwa ni nzuri tu asiwape watu mzigo wa kuchanga.

Lakini, kikichotokea ni kwamba, kuna watu walimsema kuwa anaringa na anajiona anaweza kumaliza gharama za harusi yake peke yake bila ya kuwapa watu nafasi ya kuchangia.

Wamakonde walisema "Ukichimama.nchale, ukikimbia nchale".

Ukichangisha lawama. Usipochangisha lawama.
Kuna aliekushurtisha kuwepo kwenye hayo magroup?? Unajua kuwa whatsapp ina option ya kuzuia kuweza kuingizwa kwenye magroup kiholela.

Mengi ya haya magroup ya shule/familia huwa ni scheme ya kuvuna ya ma admin.
Sio necessarily pesa, hata ile social validation in the sense kuwa kuna watu wanataka kufidia mapungufu ya maisha yao kwa kutaka kufuatilia maisha ya wengine na saa nyingine kuyatia dosari maisha ya wenzao kama hivyo kwa kufuatilia mara ngapi umechangia na kukuweka doa utu wako pale usipochanga.

Technology imekuwa sana kiasi cha kutohitaji ma group kuweza kuwa in touch na wengine. As it is huko shule sio kwamba nilikuwa rafiki na wote niliosoma nao. So why should that change after 20 years?
 
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
u-ndugu kufaana na sio kufanana 🐒
 
Kule kuna teams. Sasa mimi huwa naondoka kabisa. Halafu zamani nilikiwa naondoka wananirudisha ghafla bin vuu. Halafu nikawa naondoka naacha maagizo wasinirudishe, basi anakuja mwanangu mmoja inbox anaanza kunipiga sound ananiambia baba wanao tumepooza sana njoo uje utupe vitu vyako adimu vile unavyotoaga tumekumiss sana.

Wale sio watu niliokutana nao barabarani wala JF. Wengine wanangu wa kweli kabisa nawaelewa tumekua pamoja kuna stories fulani naweza kupiga nao wao tu dunia nzima hakuna atakayezielewa.

Sasa kuna wanangu fulani hao siwezi kuwakatalia narudi kwa heshima yao, na ukisharudi ndiyo unakuwa umerudi kundini sanasana unaweza kusema hapa nitapunguza interactions tu.

Ila Whatsapp ingekuwa na ignore list kama JF ingekuwa poa sana. Kuna watu wana uchawa plus plus halafu mimi sikopeshi nikianza kutupiana nao maneno inakuwa kama a 2Pac diss record, I don't do it, I overdo it..

Kifupi ukiona group lina uduanzi ukajikata ni vigumu sana kuwakatalia wana fulani fulani wakikuzukia mara kadhaa wakikuomba urudi kundini.

Halafu kwa sisi tulio mbali na Bongo kunaweza kutokea habari muhimu za kitaa ukazikosa so mara nyingine kukaa kundini hata kwa kuperuzi mara chache chache inasaidia.

Pia, genuinely kabisa, huwezi kujua unaweza kumsaidia vipi mtu akiwa katika hali gani, kuna kitu nilifanya nikaona so simple lakini kilisaidia maisha ya mtu kwa njia ambayo nilivyoambiwa na madaktari sijaamini.
 
Mkuu,

Hakuna hiyari ikiwa kuna kiranja ana ki Excel spreadsheet anahesabu nani kachangia mara ngapi. Huo ni mfumo wa nipe nikupe tu.

Yani hata ukisema mimi sichangi, we have to do better, unakuwa unahesabiwa mchawi hutaki kuchangia watu. You become a social outcast.

Sasa hapo hiyari iko wapi?

Hiyari yenye social cost si hiyari hiyo.

Mimi bora hata uniambie kuna mfuko wa kuchangia kwa mwaka naweza kuwa mwepesi kuliko hivi vimichango vya ad hoc naviona viko kushoto kweli. Ingawa nachangia kwa kiasi changu bado.

Yani naona ni kama alama ya umasikini najiingiza humo.
Bora kutumia crowdfunding platforms kama GoFundMe ambapo watu wataweza kuchangia kwa kuweka majina yao wazi au yabaki kutokujulikana [anonymous].
 
Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....

Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k

Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
😄Dont play selfish.. dwag
 
Bora kutumia crowdfunding platforms kama GoFundMe ambapo watu wataweza kuchangia kwa kuweka majina yao wazi au yabaki kutokujulikana [anonymous].
Kibongobongo anonymous unahesabika hujachanga na pesa yako inaweza kuliwa.

Famasiala na wabongo?

Kwenye kuandika majina tu unaona watu wanaogopa fraud, itakuwa huko kwenye anonymous?

Kuna siku nilitaka kuchangia anonymous, the sum was embarassing by Bongo standards, jamaa akanikatalia, akasema inabidi watu waone jina niwape motisha.

Yani ikiwa anonymous hainogi kama ukiona jina la mtu 🤣🤣🤣
 
Kwani huwa unashurtishwa kuchanga??

Nimejiwekea desturi moja sitaki group la chochote kwenye simu yangu ambalo halina maslahi ya moja kwa moja kwangu.

Nikimuhitaji school mate nitamtafuta individually, sio matangazo ya kwenye group.

Athari kubwa ya haya magroup ni kujipa unnecessary pressure ya maisha in the sense kwamba watu wamefanikiwa kwa tofauti kimaisha.

Unaweza aidha ukajikuta unahoji uwepo wako duniani kwa kuona wenzio wa rika sawa wamepiga hatua kubwa kuliko wewe ama ku attract attention/vizinga na vijicho kutoka kwa wale watakaohisi umewazidi kimaisha.
🤣.

I’m not sure if I’m weird, selfish, different, or a little bit of everything, ila mimi sipo kwenye group hata moja!
 
Kibongobongo anonymous unahesabika hujachanga na pesa yako inaweza kuliwa.

Famasiala na wabongo?

Kwenye kuandika majina tu unaona watu wanaogopa fraud, itakuwa huko kwenye anonymous?

Kuna siku nilitaka kuchangia anonymous, the sum was embarassing by Bongo standards, jamaa akanikatalia, akasema inabidi watu waone jina niwape motisha.

Yani ikiwa anonymous hainogi kama ukiona jina la mtu 🤣🤣🤣
Jamii yetu iko judgemental sana hususan kwenye baadhi ya mambo kama haya ya michango.

Mtu kama mimi napenda kusaidia watu wanapohitaji msaada lakini napenda kufanya hivyo kimya kimya bila kujulikana.

Ukilazimisha niweke jina, nasepa.

Si ajabu wapo watu wengine kama mimi ambao labda wangependa kuwa wachangiaji lakini hawachangii kutokana na kutokuweza kubakia anonymous.
 
Back
Top Bottom