Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Hotuba yake kwa Wabunge wale wale ambao miaka sita baadaye wameamua kumgeukia Ngeleja; Wabunge wanaosahau kuwa Kikwete huyo huyo ndiye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini na hawakumkoromea hivi.. well.. kama kweli watu wamekasirishwa na tatizo la umeme mtu sahihi siyo Waziri Mkuu wala Waziri wa Nishati ni Rais.. na chama chake...
Nishati
Mheshimiwa Spika:
Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani.
Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini.
Mheshimiwa Spika:
Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma.
Na hivyo ndivyo tutakavyofanya. Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua mipango ya umeme wa Mto Rusumo na Stigler's Gorge.
Vile vile tutaharakisha upatikanaji wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.
Mheshimiwa Spika:
Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa, kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma katika gridi ya Taifa.