Hawa ndio vibaraka wa Edward Lowasa miongoni mwa waliochukua fomu kuomba ridhaa ya CCM urais 2015

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau amani iwe kwenu.

Mchakamchaka wa makada wa CCM waliochukua fomu kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang'anyiro cha Urais kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2015 unaendelea. Kwa sasa Makada hao wapo mikoani kusaka wadhamini huku wengine wakitulia tulii baada ya kuchukua fomu hizo kwa kukosa fedha za kusaka wadhamini. Hakika ni jambo la faraja kuona kuwa chama changu kimetoa fursa ya kutosha kwa kila anayeona kuwa anafaa kuwa Rais wa nchi hii bila kujali hali ya mtu. Miongoni mwa waliochukua fomu wapo wakulima, wafanyakazi, mawaziri, viongozi wenye hadhi kimataifa, vijana, wazee na wagonjwa. Hii ni fursa pekee na huwezi kuona ndani ya chama chochote isipokuwa ndani ya CCM pekee. Kule Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad pekee ndiye aliyejitokeza kuwania nafasi ya urais na yeyote aliyejaribu kujitokeza kupitia chama cha CUF alinyamazishwa kimya kimya. Kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano, ni Ibrahim Lipumba pekee ndiye aliyeruhusiwa na chama kuwania nafasi ya Urais huku vyama vingine kama CHADEMA vikishikwa na kwikwi kwa vile mtu waliyemtegemea, Dr Slaa hadhi yake imeendelea kuporomoka hasa baada ya kupora mke wa mtu. Kwa sasa CHADEMA hawana mbadala wa Dr Slaa na wanaumiza kichwa jinsi ya kupambana na Prof Lipumba ndani ya UKAWA.

Tukiacha hayo, je unafahamu kuwa miongoni mwa waliochukua fomu ni makuwadi wa Edward Lowasa? Tulia nikujuze.

MATHIAS MENRAD CHIKAWE
Huyu ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea kwa tiketi ya CCM. CHIKAWE pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Chikawe hakuwa na mpango wa kugombea nafasi ya Urais kwa sababu hana uwezo huo. Hata hivyo, ni ushawishi na uwezeshaji wa Edward Lowasa ndio uliomsukuma Chikawe kujitokeza kugombea nafasi hiyo. Lowasa amegharamia fomu ya Chikawe, kulipa usafiri, posho, chakula na malazi kwa wapambe wa Chikawe waliosafiri toka mikoa ya kusini hadi Dodoma pamoja na gharama zote zinazohusiana na zoezi la kusaka wadhamini.

Lengo la Lowasa kufanya hivyo ni kuwagawa na kuwachanganya watu wa mikoa ya kusini ambao wengi waliweka tumaini lao kwa mwana wa kwao, Benard Kamilius Membe. Mpango uliopo ni kwamba ikiwa Lowasa atapenya kwenye tundu la sindano na kuingia kwenye Tano Bora, sambamba na Benard Membe, basi Chikawe atatangaza rasmi kumuunga mkono Lowasa. Aidha, ikiwa Chikawe atafanikiwa kuingia tano bora na Lowasa akatupwa nje, basi Lowasa atatangaza kumuunga mkono Chikawe. Haya ndiyo makubaliano yao.

HARRISON MWAKYEMBE
Huyu kaingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais hatua ya mwisho tena kimya kimya mithili ya mtoto wa Mkulima. Kachukua fomu kwa shinikizo na kagharamiwa kila kitu na Edward Lowasa. Ndio. Unabisha? Ukweli ndo huo. Ukweli ni kwamba, Sakata la Richmond limemuumiza sana Lowasa. Hakika limemtia doa kubwa ambalo ni aghalabu kufutika. Ni sakata hilo la Richmond ndilo lililomfanya Lowasa kwa kumtumia shushushu wake Apson Mwang'onda kuagiza sumu Israel kwa lengo la kumthulubu Mwakyembe na kutaka kumuua huku akijiona. Ndio na ndio uhalisia. Mwakyembe akanyonyoka nywele mithili ya mtoto mwenye kwashakoo huku ngozi yake ikitoka pumba mithili ya mahindi yaliyokobolewa. Hizi ni taarifa nyeti sana na wachache wanajua. Mwakyembe alinasa wakati alipoenda mkoa fulani ambapo mhudumu wa ofisi moja ya serikali aliyepewa maelekezo rasmi baada ya kupata mpunga wa maana aliweka sumu hiyo kwenye taulo inayotumika baada ya kunawa mikono. Mbaya zaidi, mhudumu huyo naye ametangulia mbele ya haki baada ya watu hao ambao ni katili kupindukia kukatisha uhai wake baada ya kuona anaweweseka kutokana na mateso aliyokuwa anayapata Mwakyembe. Heko imwendee Rais Kikwete ambaye amenusuru maisha ya Mwakyembe baada ya kugharamia matibabu ya hali ya juu huko India na sasa Mwakyembe amerejea katika hali yake ya zamani.

Mwakyembe aliumia sana baada ya kujua siri hiyo na hakika alikuwa tayari kuwataja wahusika. Hata hivyo busara ilitumika. Lowasa alimtuma Apson aongee na Mwakyembe na amweleze mkasa mzima. Lowasa alitoa maelekezo kuwa yupo tayari kutoa kiasi chochote cha fedha atakachohitaji Mwakyembe na kuanzia hapo watakuwa marafiki. Ilikuwa vigumu sana kwa Mwakyembe kukubali hilo. Hata hivyo baada ya kutafakari sana na kuingiwa na hofu ya kudhuliwa tena, Mwakyembe alikubali na tangu wakati huo mahusiano yao ni mazuri. Hivi juzi kuna watu waliandika waraka unaohusu sakata la Richmond na kudai kuwa ulitoka kwa Mwakyembe. Mwakyembe aliukana waraka huo na alisema kuwa kwa sasa wana mahusiano mazuri na Lowasa na kwamba ugomvi wao uliishia pale Dodoma na kwamba kilichotokea ni ajali ya kazi.

Inadaiwa kuwa Mwakyembe ameshawishiwa na swahiba wake Lowasa ili kupunguza nguvu za Prof Mwandosya ambaye ameingia makubaliano na Membe ya kushirikiana kwenye kinyang'anyiro hicho. Kwamba, ni dhahiri kuwa Mwakyembe hatafika hata tano bora. Hata hivyo, Mwakyembe atatumika na Lowasa kwa jambo moja tu la kumsafisha na kashfa ya Richmond ambayo inaendelea kumtesa kila kukicha. Mwakyembe amekubali kazi hiyo na kwa sasa anafanya kazi kubwa ya kuandaa maelezo ya kupingana na ripoti ya Richmond. Ndio. Huu ni ukweli ambao ni aghalabu kuusikia ukisemwa.

LAZARO NYALANDU
Huyu, ni Waziri wa Maliasili na Utalii. Ni muda mrefu alitangaza kuwania nafasi ya Urais. Mkakati wake ulikuwa ni wa wazi. Hata hivyo, Lowasa ameingia makubaliano naye ili Lazaro amuunge mkono pindi akifanikiwa kupenya kwenye tano bora. Lowasa anamhofia sana Mwigulu Nchemba kwa upande wa kanda ya kati. Hivyo makubaliano yake na Nyalandu yanalenga kuweka mtego ambao utawagawa watu wa kanda ya kati ikiwa wote Lowasa na Mwigulu au Nyalandu na Mwigulu watafanikiwa kuingia kwenye tano bora. Haijapata kutokea Nyalandu akiweka msimamo wake juu ya rushwa na ufisadi.

WILLIAM NGELEJA
Ujio wake kwenye kinyang'anyiro hiki ni wa kimkakati zaidi. Kwanza, Ngeleja anaona kuwa aliondolewa kwenye Wizara ya Nishati na Madini kwa mizengwe na kwamba anaona kuwa anao uwezo wa kuendelea kuongoza nafasi hiyo. Makubaliano yaliyopo na Lowasa ni kwamba ikiwa Lowasa atafanikiwa kuingia tano bora sambamba na kada yeyote wa kanda ya ziwa, iwe Magufuli, Wassira, Muhongo ama Mpina, Ngeleja aelekeze nguvu zake kwa Lowasa na hivyo kuwagawa watu wa kanda ya ziwa. Hapa ni divide and win. Matarajio ya Ngeleja ni kwamba ikiwa Lowasa atashinda Urais, ateuliwe kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hawa ni baadhi ya makada wa CCM ambao kwa utashi wao na kwa kushawishiwa au kulazimishwa wameamua kusimama ili wahesabiwe kwenye safari ya matumaini. Nitaendelea kuwajuza zaidi kwa kadri nitakavyopata taarifa za maana na za hakika juu ya Team Lowasa. Mpaka kieleweke. Ni rahisi sana kupata taarifa kutoka kwa fisadi Lowasa kwa vile tumo ndani yake.
 
Hivi CCM imeanza lini kuwa na mafisadi.?? Maana nakumbuka wewe ni mmojawapo wa walikuwa wanapinga sana kwamba CCM ina mafisadi.... Au uraisi ndo umeleta mafisadi..??
Mkuu, sijawahi kupinga uwepo wa mafisadi ndani ya CCM. Wapo sana na bahati nzuri wanafahamika. Katibu Mkuu wetu ametuasa kuwa uchaguzi wa 2015 utumike kuwaflush out hawa mafisadi wote na mazalia yao
 
hapo kwa mwakyembe umekosea.
Mkuu, nilijua hili wengi watakanusha. Ila ndo uhalisia. Binafsi niliposikia habari hii kwa mara ya kwanza sikuamini mpaka nilipofanya utafiti mdogo na kupewa vielelzo kadhaa. Hakika nilishikwa na butwaa kweli. Sikuamini. Ila ukweli ndo huo
 
Miongoni mwa waliochukua fomu wapo wakulima, wafanyakazi, mawaziri, viongozi wenye hadhi kimataifa, vijana, wazee na wagonjwa.
Ondoa hii mitu mapema, Ikulu siyo wodi ya wagonjwa..(by Lusinde)
 
Mtoa mada, UNAHARIBU CCM.....!!!!


UNAUA CCM yetu.... acha kukichafua chama...!!! 🐭🐭🐭🐶
 
Lizaboni , nakushauri tu, Huwezi kuzuia mafuriko kwa kiganja cha mkono. Hakuna namna tena, watanzania wameshaaamua kuwa baada ya KIKWETE ni LOWASSA. By hook or crook!
Mkuu MUSSA ALLAN, mimi pia ni Mtanzania na naamini kuna Watanzania wengi ambao hawampendi Lowasa si kwa vile tu anatoka Kaskazini ambako ni nyumbani kwako bali ni kwa matendo yake ya ufisadi na afya yake kuwa mgogoro. Hili lipo wazi na nitaendelea kulisemea mpaka kieleweke
 
Mkuu, nilijua hili wengi watakanusha. Ila ndo uhalisia. Binafsi niliposikia habari hii kwa mara ya kwanza sikuamini mpaka nilipofanya utafiti mdogo na kupewa vielelzo kadhaa. Hakika nilishikwa na butwaa kweli. Sikuamini. Ila ukweli ndo huo

mkuu hakuna mwanaccm mnafiki kama mwakyembe nq sitta.
 
kwa kiasi fulani ukosahihi. wagombea wengine wanaomuunga mkono lohaasa ni mohamedi gharibu bilali na hata january makamba..
Ahsante Mkuu hapa pa Ghalib. Pa Makamba sina hakika. Kuhusu Mohamed Ghalib Bilal ni kwamba wamewekeana makubaliano kuwa ikiwa Lowasa atafanikiwa kuteuliwa na chama kuwania Urais, Mgombea Mwenza wake atakuwa Mohamed Ghalib Bilal. Nilipitiwa tu mkuu ila hii niliinyaka mapema kabisa
 
Mkuu MUSSA ALLAN, mimi pia ni Mtanzania na naamini kuna Watanzania wengi ambao hawampendi Lowasa si kwa vile tu anatoka Kaskazini ambako ni nyumbani kwako bali ni kwa matendo yake ya ufisadi na afya yake kuwa mgogoro. Hili lipo wazi na nitaendelea kulisemea mpaka kieleweke

Komredi, sikatai wako ambao hawamkubali LOWASSA, Lakini Watanzania walio wengi wanaamini LOWASSA ndio kimbilio lao, kwenye ngazi ya urais, hilo halina mjadala.
 
Back
Top Bottom