Hatutaki viwanda vinavyotugeuza watumwa na mateka wa nchi yetu wenyewe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,408
52,059
Na, Robert Heriel

Je, sisi ni watumwa?
Je, sisi ni Mateka? Nauliza sisi ni misukule?
Ukiambiwa viwanda vimejengwa, uliza swali hili je kimeajiri wafanyakazi au watumwa?

Mada hii ni chungu, kama huna uvumilivu naomba uishie hapa. Lugha itakayotumika ni lugha ngumu, lugha isiyopendeza, kwani kukemea jambo lisilopendeza inahitaji lugha isiyopendeza.

Niite Taikon wa Fasihi, Rafiki wa Siriel, Kutoka nyota ya Tibeli, Yenye mbawa Mbili, ipaayo katika ulimwengu mmoja hata mwingine.

Mara kwa mara nimekuwa nikisikisia serikali ikijivunia kujenga viwanda maelfu elfu na kuajiri watu. Basi Taikon nikisikia hivyo roho yangu kwatu inachekelea, inafurahi, inacheza Amaboko! Kwa sababu najua Watanzania wenzangu wanaenda kufanyakazi na kujipatia kipato kupitia viwanda hivyo.

Sasa Juzi nikiwa Morogoro kwenye kijiwe fulani, niliket, vijana wengi walikuwa wakibalidilishana mawazo, mimi nilikuwa kimya. Punde mada ya siasa zikatia timu, na hapo ndipo nikataka kujua uelewa wa vijana hao kwenye ishu za kisiasa.

Kundi moja lilikuwa likiisifu serikali kwa mazuri wakati jingine likiiponda. Ni sawa kwa vijana. Moja ya hoja zilizonivutia kwa watetezi wa Serikali ni kuhusu Viwanda. Vijana wale watetezi wa serikali wanasema; Serikali ya awamu hii imejenga viwanda vingi sana. Serikali ya viwanda hii. Hakika CCM ndio chama Dola.

Mimi nilifurahi kuona vijana wakitambua jitihada za serikali na kuipongeza. Sasa nami kwa mara ya kwanza nikafungua mdomo wangu.Nikauliza; Wewe unafanya kazi wapi? Akanijibu; Kiwandani kwenye kiwanda cha ...." Nikasema moyoni ndio maana, Mungu ikabiriki serikali. Sasa swali la pili nililomuuliza ndio lilibadilisha muelekeo wa baraka zangu na shukurani zangu.

Nilimuuliza; Unalipwa shilingi ngapi? na unafanya kazi masaa mangapi?
Hapo hapo ndipo kizaa zaa kilipoanza, alipata kigugumizi cha ghafla ambacho kiliniogopesha, pengine nilifikiri atakufa kwa namna alivyokuwa anatetemeka. Bahati wengi wa vijana pale wameajiriwa naye kiwandani. Wakajibu; Tunalipwa 125,000/= na tunfanya kazi masaa 12 kwa siku, kwa wiki tunafanya kazi siku sita.

Machozi yalinitoka, nilijikuta siwezi kuongea kitu. Watu wakanishangaa. Nikazuga kuna kitu kimeniingia machoni ili wasielewe kinachonitoa machozi.

Umri wao ni kati ya 35 - 45, hakuna mwenye kiwanja, hakuna mwenye nyumba, kijana wa umri huo anawaza kununua kitanda na godoro, kijana wa umri huo hawezi kulipa kodi ya 25,000/= Wengi wao wanaishi nyumbani licha ya umri kuwatupa mkono. Si kwamba hawafanyi kazi, si walishanambia wanafanya kazi viwandani, mshahara wao ni 125,000 kwa mwezi, na kwa siku wanafanya kazi masaa 12, shift ya usiku na mchana. Looh!

Sasa turejee hapa kwenye mada.

Hivi tunajenga viwanda ili tuwageuze vijana wetu mateka?
Hivi tunajenga viwanda ili tuwafanye vijana wetu watumwa?
Hivi tunajenga viwanda ili tuwafanye vijana wetu misukule?

Jamani, unajua masaa kumi na mbili sio mchezo hata kama kazi unalipwa hela nyingi, kufanya kazi masaa kumi na mbili kila siku kwa siku sita si mchezo. Sasa vijana wengi waliopo viwandani wanalipwa mishahara ya hovyo, naweza kusema wamegeuzwa watumwa, wamegeuzwa misukule na mateka ndani ya nchi yao.

Serikali lazima iangalie jambo hili, huwezi jisifu unajenga viwanda vinavyogeuza wananchi wako watumwa, huwezisifu hata kidogo.

Unajua zamani watu walichukuliwa utumwani kwenda kutumikishwa kwenye maviwanda na mashamba, na migodi huko ughaibuni. Utumwa ukakemewa, sisemi uliisha, bali ulihamishwa kutoka ughaibuni na kurejeshwa kwenye nchi hizo hizo zilizokuwa zinalalamika kuchukuliwa utumwani. Sasa yale maviwanda na mashamba yamehamishiwa huku huku kwenye nchi zetu. Je watakaotumikia mashamba hayo ni kina nani?

Ni bora tusiwe na viwanda kama hali yenyewe ndio hiyo. Hatuwezi kuwa na viwanda vinavyogeuza vijana na wanawake zetu watumwa, mateka, na kuishi maisha ya hovyo.

Mtu unakuwa tajiri kwa kutumikisha ndugu zetu, mtu unakuwa tajiri kwa kuwalipa mishahara ya kitumwa vijana wetu. Usishangae tajiri namba moja mpaka kumi nao wanahusika na kuwageuza vijana wetu watumwa kwa kuwafanyisha makazi masaa mengi huku ujira ukiwa haufiki 200,000/=

Serikali nayo inayaona mambo haya inachekelea, ati kisa inachukua kodi. Kodi ndio igeuze vijana, na wanawake wetu kuwa watumwa. Kodi! Kodi!
Serikali badala ihangaike kutunga sheria zitakazowapa maslahi wananchi wake, hasa wafanyakazi wa sekta binafsi kwa maana nafahamu wafanyakazi wa serikalini kima cha chini ni 375,000/=. Sasa mbona sheria za kima cha chini cha wafanyakazi wa viwandani ni 100,000/=

Serikali kama kuna sheria ambazo ilipaswa ibadilishe na kuisimamia mapema basi ni sheria hizo za mishahara ya wafanyakazi hasa wa sekta binafsi lakini serikali kimya.

Je Serikali imekubaliana na vijana kufanya utumwa?
Je serikali yetu imekubaliana na wanawake wetu kugeuzwa mateka na wamiliki wa maviwanda?

Ni bora tusiwe na viwanda, kuliko viwepo alafu vigeuze vijana na wanawake wetu mateka.

Alafu kuna watu watasema, kama hutaki kazi acha. Pumbavu! Yaani ujenge kiwanda kwenye nchi yetu, kwenye mkoa wetu, wilaya yetu, kata yetu, alafu uchume utajiri kupitia nchi yetu, mali zetu, watu wetu, alafu unasema kama hatutaki kazi kisa mishahara midogo tuache. Kwenye Ardhi yetu, Looh! Wewe ndio kama huwezi kutulipa mishahara rafiki, inayokidhi mahitaji yetu, ndio uondoke, tafuta nchi ywa watumwa, tafuta wilaya za watumwa, tafuta mikoa ya watumwa ndio ukajenge kiwanda chako huko, watakapopenda ufanye na utambe katika ardhi yao. Lakini sio kwetu.

Ni bora tubaki tunachunga mbuzi na kondoo tukiwa huru kuliko kuajiriwa na kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
Ni bora tubaki tunalima nyanya, na mahindi hata kama hayatakuwa na soko lakini tupo huru kuliko kuwa misukule.

Serikali inawaambia vijana wachape kazi, tena Mhe. Rais anakuambia Hapa kazi tuu, lakini kazi za kitumwa hatutaki, kazi za kisukule hatutaki.

Serikali kama ilikuwa na nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania hasa vijana na wanawake wa taifa hili ingehakikisha kima cha chini walau kiwe 500,000/= kiwandani na serikalini. Mtu kama hawezi atafute nchi zingine za kitumwa akaanzishe viwanda vyake huko vya kipuuzi.

Hatuwezi kuwa na utitiri wa viwanda vinavyozalisha watumwa na misukule. Ni bora tuwe na kiwanda kimoja au kisiwepo kabisa. Kuliko kuwa na viwanda vya watumwa.

Najua kuna watu watadhani sijui mchango wa viwanda kwenye kodi. Naufahamu. Lakini ni bora serikali ikose kodi za viwanda vinavyozalisha watumwa na mateka kuliko iwe navyo alafu watu wazidi kuteseka.

Narudia tena; Serikali ingepaswa aingalie zaidi maslahi ya watu wake kabla ya kitu chochote kile. Kisha zifuate hizo sheria zingine sijui sheria za mitandao ya kijamii, sijuyi sheria za vyombo vya habari.

Hivi 200,000/= kwa mwezi inampeleka wapi kijana. Piga hesabu anafanya masaa kumi na mbili, akitoka amechoka.

Alafu vijana haohao wakitetewa na watu hawajielewi, yaani wapo wapo hivi. Mtu unamiaka 30 bado unawaza habari ya kitanda na godoro, unawaza hela ya kula, unalipwa sijui 180,000/= bado unasifu ujinga.

Ndio maana nilimwambia Tundu Lisu, asipoteze Muda wake kutetea wapumbavu na masikini, Kwa maana hao hao ndio walimuua Yesu, walitaka Kumuua Musa(Hawa utasema huwajui. Walimuua Muammar Ghadafi wa Libya, Patric Lumumba wa Congo(Hawa pengine ukawajua)

Taikon nimemaliza, leo sitaki maswali, kama hujaelewa basi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Ukiacha suala la mishahara midogo, hivi hivyo viwanda tunavyoaminishwa vimejengwa na hii serikali viko wapi?

Hapa nilipo naona viwanda vilevile vilivyokuwepo toka awamu iliyopita, na kabla ya awamu iliyopita, sijui nyie wenzangu huko mlipo kuna viwanda vipya?
 
Viwanda hewa huvioni??
 
Yes, Yes, Yes!
 
nakukubali umeongea point ndugu yangu,wasio kukubali ni wale mazuzu na misukule ya mainzi ya kijani mtani wangu
 
Kama hakuna viwanda vingi watu watalipwa hata ugali maharage tu kama ujira kufanya kazi viwandani
 
Back
Top Bottom