Hatupaswi kuwalaumu Marehemu?

leroy

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,590
2,141
Hoja iko Mezani wana jamvi,
Nimekuwa nikiwasikia baadhi ya watu wakisema hakuna haja ya kuwalaumu na kuwashutumu watu waliokufa mathalan hata kwa mambo yanayoathiri wale walio hai walioachwa.
Nataka kujua kimantiki, hoja hii ina ukweli wowote?

Vietnam3_13_RoadFromDalat_ChristianGraveyard.JPG
 
Hoja iko Mezani wana jamvi,
Nimekuwa nikiwasikia baadhi ya watu wakisema hakuna haja ya kuwalaumu na
kuwashutumu watu waliokufa mathalan hata kwa mambo yanayoathiri wale
walio hai walioachwa.
Nataka kujua kimantiki, hoja hii ina ukweli wowote?

CONFIG]55173[/ATTACH]
Hoja hiyo ina mantiki na ukweli kwa vile hata ukimlaumu marehemu haisaidii kwa vile amekufa na hazisikii lawama hizo.Lawama ziende kwa aliye hai ili aweze kujirekebisha.
NB:Watu wanaweza kujifunza kupitia makosa ya marehemu ili yasijirudie na kuleta athari kwa jamii.
 
Marehemu hawezi kujitetea, ukimlaumu, unamuonea, angekuwa hai angeweza kujibu shutuma, akiwa mfu, unakuwa unajipendelea, maana utabwabwaja peke yako, halafu hatutausikia upande wa pili.
Ndo maana hata wakati wa msiba, sifa nzuri za marehem ndizo hutamkwa.
Mkisema mabaya yake, mnamuonea kwa vile hana nafasi ya kujitetea, maana huenda anasingiziwa.
Mabaya na lawama kwa marehemu humuachia yeye na Mungu wake wamalizane huko!
 
kwanza kwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kumlaumu marehemu hata kidogo........kwanza utaonekana huna akili kwa kweli coz hackii wala hawezi kujibu,so haina haja ya kumlaumu marehem
 
Marehemu hata kama ukimlaumu ataamuka ili ajirekebishe?.
THE UNSEEN IS ILLUSTRATED BY THE SEEN.
 
Back
Top Bottom