Hatua zinaendelea kuchukuliwa kuhusu tuhuma na shutuma zilizotolewa

Mnyika asante kwa update. Ni kweli kabisa, suala hili lifanyiwe kazi, na sisi tunawaombea Mungu wale wanaolifanyia kazi, tufike mahala tupate suluhisho. Kuhusu Kadi, ufafanuzi umetolewa sana, ila OLE WAO, wao wanaowapotezea muda wa-TANZANIA kwa ujadili suala la kadi. Hata bila kuangalia kanuni,ukweli ni kuwa mtu akihama chama si lazima arudishe kadi, maana kadi inakuwa tayari imekuwa 'INVALID'. Ila kwa kuwa wa-Tanzania wengi ni wepesi wa kupokea mambo bila kutafakari ndio maana hoja kama hizi zinaibuliwa.
 
Naona we bado hjaelewa kwani umeambiwa usubr but we umeanza kutoa maamuz,au we gamba?

Ndugu huyo mtu Gaijin achana naye maana naona tatizo lake ni kubwa kuliko tunavyofikiri. Ameoneysha dhahili hana literature kwenye semantics na stylistics na ndio maana uchangiaji wake uko to biased and prejudiced. Ameshindwa kuficha mapenzi yake kwa Shonza. Anataka kulazimisha kosa lisilo kosa kwa Dr. Slaa na tuhuma ambazo hazijachunguzwa.
 
Avanti, asante kwa maoni yako hata hivyo zingatia kuwa 'press' yangu ipi? Ikiwa wewe kweli ni mwanachama wa CHADEMA na una malalamiko dhidi ya kadi ya Dr Slaa andika rasmi kwa chama. Kabla ya kuandika malalamiko hayo usome kwanza katiba ya CHADEMA, katiba ya CCM na sheria ya vyama vya siasa. Dr Slaa ameshasema wazi kwamba yeye si mwanachama wa CCM, ni mwanachama wa CHADEMA toka alipohama CCM. Mwanachama akihama chama kimoja tayari anapoteza uanachama wake wa chama cha awali, hii ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, katiba za vyama vya siasa na pia hukumu ya mahakama ambayo imewahi kutolewa kuhusu suala la kadi. Ukishazingatia hayo na bado ukaendeleza suala hilo na ikiwa kwenye ni mwanachama utakuwa umeingia kwenye mtego wa kipuuzi wa CCM.

JJ

Ili CCM wasiweze kuendelea na hii propaganda ya kumchafua Dr, kwa nini asiite press conference akaichoma moto hiyo kadi ya CCM? Kwani inamgharimu nini
 
Me nimekatishwa sana tamaa na baadhi ya viongozi wa Chadema(Vilaza) tume jaribu kufight sana wana Chadema na kukisimamia chama ila wengine kumbe walikuwa wana pasua chama sisi tukiwa hatujui,me nadhani Chama sasa hivi kitoe uwamuzi mzito sana la sivyo kitapoteza wanachama wengi sana fanyeni uwamuzi mzito sana,nilikuwa number moja kumtetea Zitto humu ndani kwa kuwa nilimuona ni kiongozi bora kumbe alikuwa ana mambo yake mwenyewe,so nitaanza tena ramsi after kuona maandiko ya chama na uwamuzi mliochukua zidi ya hawa masalia, na hatuwezi kukata tamaa mpaka kieleweke chadema sio ya kina Zitto so lazima uwamuzi mgumu ufanyie na tupate maamuzi kamili as soon as possible....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ndugu huyo mtu Gaijin achana naye maana naona tatizo lake ni kubwa kuliko tunavyofikiri. Ameoneysha dhahili hana literature kwenye semantics na stylistics na ndio maana uchangiaji wake uko to biased and prejudiced. Ameshindwa kuficha mapenzi yake kwa Shonza. Anataka kulazimisha kosa lisilo kosa kwa Dr. Slaa na tuhuma ambazo hazijachunguzwa.

Nimegundua michango yake since second thread nikaona na yeye ni wale wale wapo after something ana force vitu ambavyo anaona havipo na anataka viwepo

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kwa wengi tusio na ushabiki wa vyama lakini tunapenda mabadiliko ya kimfumo na kiuchumi,kinachoendelea ni kitu cha kusikitisha.

Gaijin namuona kama independent thinker anayesimamia usawa,haki na principles.kama slaa hana kosa hakuna haja ya yeye kukataa uchunguzi huru.slaa must know better kuhusu situation ya kesi ya nyani kwenda kwa ngedere.alilalamika tume ya uchaguzi kutokuwa huru kwa kuwa iliteuliwa na raisi/kikwete. Ategemee wapinzani wake ndani ya chadema kufeel the same.hawawezi kupeleka kesi inayonhusu kwake.

Kwangu mimi hii ni challenge kwa chadema kurekebisha katiba yake,ili kuondoa madaraka makubwa kwa individuals,na yahamishiwe katika mfumo. Hamna haja ya kupigania chadema iende ikulu 2015,kama haiko tayari kupigania mfumo imara ndani ya chadema,kama haiko tayari kupigania haki na usawa,kama haiko tayari kuonesha watanzania kuwa status quo will not be tolerated.

Putting slaa and zitto as bigger than life figures is disheartening for some of us who saw glimpse of hope in chadema.

Muda si mrefu tutarudi kwenye kukubali fikra za katibu na mwenyekiti.

Walichokifanya kina Ben na wenzake ni upuuzi wa hali ya juu.

Naamini Chadema waanze kufanya aptitude tests za makada wake,maana so far wamereveal ni jinsi gani hawastahili vyeo,dhamana na majukumu waliyopewa.
 
Kwa wake pro chadema wengi humu,wameacha kutazama vitu kwa uhalisia wake.

As long as I support slaa initiatives and fight for a better TZ in the future,I don't support his blind idolising as an individual to be of any good.remmber kikwete circa 2005?

One thing is clear,no one man in history has managed to remain the same figure once unlimited power is bestowed upon him.

Its time Chadema puts clear limits and counter balances power it has afforded ita leaders.

Once this is done,hizi biashara za masalia wa zitto kabwe,kina Ben,kina Juliana etc,hazitakuwepo,kwani they will not be workig for the benefit of a single person but the position bestowed upon that person,which can be taken away instantly should there be clear abuse.

Otherwise
 
Tangu wanachama wachache wa CHADEMA walipoanza kutuhumiana na kushutumiana kupitia JF watoa maoni mbalimbali mmetoa mwito kwa chama kuchukua hatua na wengine mmehitaji majibu kutoka viongozi wengine na kwangu kuhusu hali hiyo iliyojitokeza. Ifahamike tu kuwa mara baada ya tuhuma na shutuma hizo kuandikwa nimewasiliana na baadhi ya wahusika waliotumia majina yaliyothibitishwa (verified users) ili wawasilishe maelezo navielelezo vyao kwa chama ili hatua ziweze kuchukuliwa. Nimechukua hatua hiyo kwa kuzingatia katiba ya chama ibara ya 5.3 na Kanuni za chama 7.7.5, Maadili yachama 10.0 Itifaki ya chama 12.0. Aidha, nimewasiliana pia na uongozi wa BAVICHA ili waweze kuagiza viongozi na wanachama wake waliohusika watimize wajibu huo kwa mujibu wa kanuni za kuongoza Baraza la Vijana wa CHADEMA kwa kuzingatia pia katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama. Pamoja na kusubiri maelezo na vielelezo toka kwa waliotakiwa kuwasilisha, ifahamike kuwa hata kabla ya kuandikwa kwa tuhuma na shutuma za hivi karibuni zilizotolewa na wanachama wenye majina yaliyothibitishwa, chama (kupitia Kurugenzi ya Ulinzi naUsalama) kilishaanza uchunguzi kuhusu madai ya kuwepo kwa baadhi ya wanachama wenye kukichafua chama na viongozi wake katika mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano. Aidha, ushushushu umekuwa ukiendelea kufuatilia nyendo za wapinzani wa nje ya chama zenye mwelekeo wa kuhujumu kwa kutumia mbinu haramu vuguvugu la mabadiliko nchini linalohamasishwa na CHADEMA. Hivyo, maelezo na vielelezo vitavyowasilishwa vitashughulikiwa pia kwa kuzingatia ripoti za uchunguzi huo na hatua stahiki kuchukuliwa kwa watakaothibitika kukiuka katiba,kanuni, maadili na itifaki ya chama na pia maamuzi ya ziada yatafanyika juu ya wahujumu wa mabadiliko nchini watakaobainishwa. Kwa mliohoji kuhusu matakwa ya kanuni za CHADEMA kuhusiana na tuhuma na shutuma zilizojitokeza nawashauri mrejee sura ya kumi ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama hususan kifungu cha 10.0 kinachohusu Maadili ya Viongozi, Sifa mahususi za Viongozi na Maadili ya wanachama. Maadili ya CHADEMA yanakataza kiongozi kutoa tuhuma zozote dhidi ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelekezwa kwenye kanuni za chama. Ni marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu chama, kiongozi na mwanachama yoyote na viongozi wanapaswa kutofautisha kati ya kashfa na ukosoaji wa kisiasa. Ni kinyume pia na maadili ya CHADEMA kwa mwanachama kufanya upinzani dhidi ya chama na kujihusisha na makundi ya majungu ya kuchonganisha viongozi na wanachama. Badala yake mwanachama anapaswa kuwa mwanaharakati wa kweli katika kutetea maslahi ya chama na jamii kwa ujumla kwa kuzingatia madhumuni, itikadi na falsafa ya CHADEMA. CHADEMA imekuwa na kawaida ya kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu kupitia vikao vyake na vyombo vyake vya kikatiba hivyo natoa rai kwa wanachama na watanzania wote wanaounga mkono mabadiliko kuwa wavumilivu na wastahimilivu ili hatua hizo zichukuliwe misingi ya haki na ukweli. CHADEMA inaendelea na dhima yake kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu; masuala na matukio yanayojitokeza dhidi ya dhamira hiyo yachukuliwe kama changamoto katika kazi ya kuwezesha vuguvugu la mabadiliko. Kwa sasa kipaumbele ni kusimamia maamuzi ya kamati kuu iliyomalizika karibuni kwa kurejea pia mikakati na mipango ambayo chama kinaendelea kuitekeleza ya kuwaunganisha watanzania kwa falsafa yake ya “Nguvu ya Umma” mpaka kieleweke. JJ
Mheshimiwa JJ nashukuru kwa maelezo mazuri sana.Kinachonifurahisha ni kwmaba pamoja na hizo vurugu zao na na contsnt bombardment of postings bado crucial figure za masalia hazitochomoka kanuni ulizodokeza hapoa juu.Ndhani biashara itakuw aimekwisha. Waache wakualike ktk mawazo yao mafupi for sometimes kabla hawajaanza kuwa fructrated tena na kuanza kutukana.
 
Kwa wake pro chadema wengi humu,wameacha kutazama vitu kwa uhalisia wake. As long as I support slaa initiatives and fight for a better TZ in the future,I don't support his blind idolising as an individual to be of any good.remmber kikwete circa 2005? One thing is clear,no one man in history has managed to remain the same figure once unlimited power is bestowed upon him. Its time Chadema puts clear limits and counter balances power it has afforded ita leaders. Once this is done,hizi biashara za masalia wa zitto kabwe,kina Ben,kina Juliana etc,hazitakuwepo,kwani they will not be workig for the benefit of a single person but the position bestowed upon that person,which can be taken away instantly should there be clear abuse. Otherwise
ila si masalia wala ZZK.The spoiled kid, kadekezwa sana kwa kupewa ushauri wa bure na kil akiukataa bado alibebwa.
 
Tangu wanachama wachache wa CHADEMA walipoanza kutuhumiana na kushutumiana kupitia JF watoa maoni mbalimbali mmetoa mwito kwa chama kuchukua hatua na wengine mmehitaji majibu kutoka viongozi wengine na kwangu kuhusu hali hiyo iliyojitokeza.

Ifahamike tu kuwa mara baada ya tuhuma na shutuma hizo kuandikwa nimewasiliana na baadhi ya wahusika waliotumia majina yaliyothibitishwa (verified users) ili wawasilishe maelezo navielelezo vyao kwa chama ili hatua ziweze kuchukuliwa. Nimechukua hatua hiyo kwa kuzingatia katiba ya chama ibara ya 5.3 na Kanuni za chama 7.7.5, Maadili yachama 10.0 Itifaki ya chama 12.0.

Aidha, nimewasiliana pia na uongozi wa BAVICHA ili waweze kuagiza viongozi na wanachama wake waliohusika watimize wajibu huo kwa mujibu wa kanuni za kuongoza Baraza la Vijana wa CHADEMA kwa kuzingatia pia katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.

Pamoja na kusubiri maelezo na vielelezo toka kwa waliotakiwa kuwasilisha, ifahamike kuwa hata kabla ya kuandikwa kwa tuhuma na shutuma za hivi karibuni zilizotolewa na wanachama wenye majina yaliyothibitishwa, chama (kupitia Kurugenzi ya Ulinzi naUsalama) kilishaanza uchunguzi kuhusu madai ya kuwepo kwa baadhi ya wanachama wenye kukichafua chama na viongozi wake katika mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano.

Aidha, ushushushu umekuwa ukiendelea kufuatilia nyendo za wapinzani wa nje ya chama zenye mwelekeo wa kuhujumu kwa kutumia mbinu haramu vuguvugu la mabadiliko nchini linalohamasishwa na CHADEMA.

Hivyo, maelezo na vielelezo vitavyowasilishwa vitashughulikiwa pia kwa kuzingatia ripoti za uchunguzi huo na hatua stahiki kuchukuliwa kwa watakaothibitika kukiuka katiba,kanuni, maadili na itifaki ya chama na pia maamuzi ya ziada yatafanyika juu ya wahujumu wa mabadiliko nchini watakaobainishwa.

Kwa mliohoji kuhusu matakwa ya kanuni za CHADEMA kuhusiana na tuhuma na shutuma zilizojitokeza nawashauri mrejee sura ya kumi ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama hususan kifungu cha 10.0 kinachohusu Maadili ya Viongozi, Sifa mahususi za Viongozi na Maadili ya wanachama.

Maadili ya CHADEMA yanakataza kiongozi kutoa tuhuma zozote dhidi ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelekezwa kwenye kanuni za chama. Ni marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu chama, kiongozi na mwanachama yoyote na viongozi wanapaswa kutofautisha kati ya kashfa na ukosoaji wa kisiasa.

Ni kinyume pia na maadili ya CHADEMA kwa mwanachama kufanya upinzani dhidi ya chama na kujihusisha na makundi ya majungu ya kuchonganisha viongozi na wanachama. Badala yake mwanachama anapaswa kuwa mwanaharakati wa kweli katika kutetea maslahi ya chama na jamii kwa ujumla kwa kuzingatia madhumuni, itikadi na falsafa ya CHADEMA.

CHADEMA imekuwa na kawaida ya kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu kupitia vikao vyake na vyombo vyake vya kikatiba hivyo natoa rai kwa wanachama na watanzania wote wanaounga mkono mabadiliko kuwa wavumilivu na wastahimilivu ili hatua hizo zichukuliwe misingi ya haki na ukweli.

CHADEMA inaendelea na dhima yake kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu; masuala na matukio yanayojitokeza dhidi ya dhamira hiyo yachukuliwe kama changamoto katika kazi ya kuwezesha vuguvugu la mabadiliko.

Kwa sasa kipaumbele ni kusimamia maamuzi ya kamati kuu iliyomalizika karibuni kwa kurejea pia mikakati na mipango ambayo chama kinaendelea kuitekeleza ya kuwaunganisha watanzania kwa falsafa yake ya “Nguvu ya Umma” mpaka kieleweke.

JJ
Thanks for info, tutasubiri hayo maamuzi kwa uhai wa chama.
 
Ukiwa kama msemaji mkuu wa chama tutalajie lini kusikia kuwa mnawachukulia hatua vibaraka wote ndani ya chama juu ya tuhuma zinazo endelea kukichafua chama kwa ajiri ya maslai yao binafsi
 
Mbona wafanyakazi wengi wa serikali wana kadi mbilimbili moja ya kumlizisha mwajili +Pili ya Mapenzi yake kwa Cdm.....sioni issue kwa. Slaa kumilili Kadi mbili..
 
Avanti, asante kwa maoni yako hata hivyo zingatia kuwa 'press' yangu ipi? Ikiwa wewe kweli ni mwanachama wa CHADEMA na una malalamiko dhidi ya kadi ya Dr Slaa andika rasmi kwa chama. Kabla ya kuandika malalamiko hayo usome kwanza katiba ya CHADEMA, katiba ya CCM na sheria ya vyama vya siasa. Dr Slaa ameshasema wazi kwamba yeye si mwanachama wa CCM, ni mwanachama wa CHADEMA toka alipohama CCM. Mwanachama akihama chama kimoja tayari anapoteza uanachama wake wa chama cha awali, hii ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, katiba za vyama vya siasa na pia hukumu ya mahakama ambayo imewahi kutolewa kuhusu suala la kadi. Ukishazingatia hayo na bado ukaendeleza suala hilo na ikiwa kwenye ni mwanachama utakuwa umeingia kwenye mtego wa kipuuzi wa CCM.

JJ
Kijana wewe unatoa majibu yanayoonyesha una weledi wa hali ya juu na unastahili kuwa mwenezi wa chama kikubwa kama Chadema. Nimejaribu kujiuliza kama swali la Avanti angekuwa amepewa Nape nini angejibu? ni ukweli ulio wazi kuwa Nape angeporomosha matusi na kejeli nyingi sana na hata hilo jibu lake lingekosa mpangilio wa kisomi. Hongera Mnyika.
SOMO KWA NAPE;
Please Nape,nafasi yako ni kubwa sana kwa chama kikubwa kama CCM hivyo nawe jaribu kujifunza kutoka kwa Kijana mwenzio Mnyika jinsi anavyojieleza kwa heshima hata pale anapokuwa analengwa kudhalilishwa. Majibu yako ya kimipasho yanakuvunjia heshima ndio maana hauishi kushambuliwa kwa hoja zako.
Natumaini 2013 utabadilika ili tuonje raha ya mijadala mizuri huku ukijibu hoja mbalimbali bila kebehi na matusi. Hayo ya matusi mwachie Lusinde na watu wake wa Mtera wewe simamia Chama ambacho kimekuamini kwamba unaweza kukieneza.
 
Asante Mnyika,angalizo tu hatutegemei haya mambo yachukue muda mrefu na blah blah nyingi.Watuhumiwa wote wamesema wanaushahidi hivyo hilo si suala la kusubiri mwezi ni within 48hrs enough!

Kuhusu hatua hatutegemei ichukue muda mrefu watu kuwajibishwa maana pia umekiri hata Chama kilishafanya uchunguzi hivyo hizi ni nyama tu za kuongeza.Hatutaki tuambiwe hadithi zaidi ya wahusika kuchukuliwa hatua.

Tunataka 2013 mwanzoni tujue muelekeo wa Chama,kama tunaenda na makundi kama haya tena wengine tutanyanyua mikono kutetea vyama tusubiri harakati mitaani pengine zitasaidia.

Mwisho tuache tabia za CCM,tukiri kuna mgawanyiko ndani ya Chama hivyo kauli za Mh Mbowe eti hakuna mgawanyiko zinasikitisha.Kuna mgawanyiko usio wakupuuzia,tunataka tuone uharaka na umakini ktk kuamua mambo yenu wenyewe ili tuwaamini.

Mr. Mtazamo, nafikiri hapa Duniani hakuna chama ambacho kipo in Heaven, yaani there's no different idealogical mind sets, sifikiri hivo hata kidogo. Na ndo maana kinaitwa Chama ambacho hujengwa na MISINGI ya itikadi,maono na accountability. Miki nafikiri hawa vijana wa BAVICHA walikuwa off track katika ujumla wake, make CHAMA kama CHAMA kinaendeshwa na kanuni na misingi yake, mnaweza kuwa different ideas au maono lakini kanuni za uendashaji zipo pale na kama kuna mwanachama mwenye shida na kitu fulani nafikiri kanuni za chama zinaelekeza jinsi ya kuwasilisha dukuduku zako bila kuathiri credentials za chama na mwanachama mwingine.
So the path they chose wa wrong, wangeweza kusikilizwa vizuri, lakini njia waliyotumia ya kutuhumu wasn't an appropriate one.

Mnyika hongera sana brother kwa maelezo yako, bado tupo kwenye mapigano ya mabadiliko and God be with us all mpaka kieleweke.
 
Mimi kama mtanzania mzalendo na mwenye mapenzi mema na nchi yangu, ninapendwa kujitokeza mbele ya wana JF na watanzania kwa ujumla kuliombe taifa langu na wale wote wanaopigania haki za wanyonge kama CDM inavyofanya. Siku za hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya vujana wa chadema wanaotumiwa na CCM ili kuivuruga chadema kwa madai kwamba Kabwe Zuberi Zitto na Dr W Peter Slaa sio wanacha waaminifu ndani ya chama.

Napenda kusema kwamba watu hao wanaowazalilisha viongozi wetu hawa ni wasaliti kwa chama na taifa kwa ujumla na bado hawajakomaa kisiasa. Wanaodai Dr Slaa na Zitto ni wana CCM wanapaswa kujua kwanza sifa za mtu kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na sio kupewa vijisent na CCm uku wakiwataka wakaeneze propaganda. Wanaojua historia ya CDM na mafanikio iliyo nayo hawataacha kuwataja Dr Slaa na ndg Zitto kama miongoni mwa viongozi wailikijenga chama kwa nguvu zao zote na kwa moyo wa dhati hadi kufikia hapa kilipo.

Ni wazi kuwa kuimarika kwa chama na kupata umaarufu tunao ushuhudia sasa nguvu na jasho la viongozi wetu hawa wawili na wengine hengi zinapaswa huheshimiwa na huenziwa. Namalizia kwa kusema kwamba vijana hawa wawaache viongozi wetu hawa na fedha wanazopewa na CCM nguvu wanazotumia kufavunjia heshima basi wazitumie kuimarisha chama.
 
Vumbi tu! Mlikuwa wapi muda wote? Matatizo lukuki, nazidi kusisitiza uongozi ni tatizo, kaka angalia nawe usije ukawa mojawapo ya tatizo kwa sababu tayari press yako iko biased kwamba "viongozi wamekashifiwa". Hao wanatakiwa kujibu tuhuma na kila mmoja ana haki kidemokrasia kutaja maonevu, mfano Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM ambako mimi siafiki ni kashfa?

Sana sana, kama hamna kitachotamkwa kuhusu kadi mi najitoa CDM na wewe mwenyewe utakosa kura yangu.

Jitoe mapema kama unadhani hoja ya kadi ya magamba ni big deal. Umetumwa na Nepi.
 
Mimi kama mtanzania mzalendo na mwenye mapenzi mema na nchi yangu, ninapendwa kujitokeza mbele ya wana JF na watanzania kwa ujumla kuliombe taifa langu na wale wote wanaopigania haki za wanyonge kama CDM inavyofanya. Siku za hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya vujana wa chadema wanaotumiwa na CCM ili kuivuruga chadema kwa madai kwamba Kabwe Zuberi Zitto na Dr W Peter Slaa sio wanacha waaminifu ndani ya chama.

Napenda kusema kwamba watu hao wanaowazalilisha viongozi wetu hawa ni wasaliti kwa chama na taifa kwa ujumla na bado hawajakomaa kisiasa. Wanaodai Dr Slaa na Zitto ni wana CCM wanapaswa kujua kwanza sifa za mtu kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na sio kupewa vijisent na CCm uku wakiwataka wakaeneze propaganda. Wanaojua historia ya CDM na mafanikio iliyo nayo hawataacha kuwataja Dr Slaa na ndg Zitto kama miongoni mwa viongozi wailikijenga chama kwa nguvu zao zote na kwa moyo wa dhati hadi kufikia hapa kilipo.

Ni wazi kuwa kuimarika kwa chama na kupata umaarufu tunao ushuhudia sasa nguvu na jasho la viongozi wetu hawa wawili na wengine hengi zinapaswa huheshimiwa na huenziwa. Namalizia kwa kusema kwamba vijana hawa wawaache viongozi wetu hawa na fedha wanazopewa na CCM nguvu wanazotumia kufavunjia heshima basi wazitumie kuimarisha chama.
Spining at work you cant compare Zitto the snake and Dr Slaa
 
Avanti, asante kwa maoni yako hata hivyo zingatia kuwa 'press' yangu ipi? Ikiwa wewe kweli ni mwanachama wa CHADEMA na una malalamiko dhidi ya kadi ya Dr Slaa andika rasmi kwa chama. Kabla ya kuandika malalamiko hayo usome kwanza katiba ya CHADEMA, katiba ya CCM na sheria ya vyama vya siasa. Dr Slaa ameshasema wazi kwamba yeye si mwanachama wa CCM, ni mwanachama wa CHADEMA toka alipohama CCM. Mwanachama akihama chama kimoja tayari anapoteza uanachama wake wa chama cha awali, hii ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, katiba za vyama vya siasa na pia hukumu ya mahakama ambayo imewahi kutolewa kuhusu suala la kadi. Ukishazingatia hayo na bado ukaendeleza suala hilo na ikiwa kwenye ni mwanachama utakuwa umeingia kwenye mtego wa kipuuzi wa CCM.

JJ

Asante sana mkuu nilipatwa na hasira sana na huyu jamaa nikaanza kuandika kumjibu kama haya ya kwako na maneno makali juu yake ila nilipoona umemjibu kisheria nikamua kuacha! Huyu siyo chadema na kweli ni chadema ni bora ajitoe tu sasa hivi maana njaa yake ikokaribu sana hawezi kuvumilia mpaka mwisho!
 
Nimeona leo kwenye gazeti la Mtanzania(27/12/2012) kwamba kuna virusi ndani ya CHADEMA na watapita kushughulikiwa na kudai hakuna mgogoro ndani ya chama. Kwa kauli hizi za katibu mkuu wa baraza la vijana wa chadema Taifa Bw.Deo Munishi zipo kipropaganda zaidi na zinadhirisha udhaifu wake katika utendaji kazi kwenye Baraza la vijana.

Kwanza kabisa Katibu mkuu wa Bavicha Taifa ameshindwa kuwatetea Makatibu wa Bavicha mikoa ili kushiriki vikao vya Bavicha kwa mujibu wa mwongozo wa mabaraza upande wa BAVICHA ibara ya 6.8.6 wajumbe wa kamati tendaji, ambapo Katibu huyu na safu yake wamekuwa wakikiuka katiba ya chama na kuwaita wenyeviti wa mikoa kwenye vikao vya kamati tendaji kama kilichofanyika Morogoro mwaka huu.

Kikao hicho kilitakiwa kushirikisha Makatibu wa Bavicha mikoa kwa mjibu wa katiba na mwongozo wa mabaraza lakini waliitwa wenyeviti wa mikoa hii ninaweza kuita kama fadhila ya uchaguzi wa Bavicha uliofanyika 2011, ambapo na mimi nilikuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Bavicha.

Namshangaa sana bosi wangu huyu na imenibidi nihoji hata uwezo wake wa
kuliongoza baraza maana anaposema hakuna migogoro wakati kwenye mitandao ya kijamii kama JamiiForum tunasoma kabisa vijana wakilumbana na hata makamu mwenyekiti wa bavicha Taifa Juliana Shoza kuonekana kutofanya kazi na safu yake kisa ikionekana hakuna maelewano baina ya viongozi wa juu wa baraza hilo.

Kwanza katibu huyu hatuoni alichokifanya tangu amekuwa katibu, ametembelea mkoa gani hapa nchini akaomba kukutana na viongozi wote wa bavicha wa majimbo na wilaya na kufanya nao vikao kwa maendeleo ya bavicha? Sioni kama tuna baraza
ila tuna jina la baraza. Kashindwa hata kuwatetea viongozi wa mikoa wa
bavicha kushiriki M4C badala yake kila anayetoka CCM leo anaingia kwenye ziara za M4C na wakongwe kuwekwa pempembeni au kutokufikiriwa na katika Baraza kuna vijana waliogombea ubunge wanauwezo mzuri kabisa wa kuwa kwenye ziara za M4C lakini hawafikiriwi, badala ya kuwatetea leo anasema eti kuna virus.

Sasa makatibu wa Bavicha mikoa wote nchi nzima tunaandaa mkakati wa kuandamana kumtaka atoke kwenye kiti chake cha ukatibu kwani ameshindwa kutetea makatibu wake. Badala yake Makatibu tunafanya kazi kwa kuletewa taarifa na wenyeviti.Tumechoka sasa.

DEOGRATIUS KISANDU

KATIBU WA BARAZA LA VIJANA(BAVICHA) MKOA WA TANGA.
27/12/2012
 
Back
Top Bottom