Hatua za kinidhamu zichukuliwe mara moja

Ladslaus Modest

JF-Expert Member
Jun 27, 2008
635
20
Wapendwa Mods na wana JF, mie ninapendekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Mtu mmoja anayeandika thread za matusi na kuposti hapa JF tangia jana.

Kama inawezekana kuwepo na ombi maalum la mtu kujirejista, maana huu uhuru wa kujirejista ndio unaofanya baadhi ya wenzetu wasio na maadili kuandika matusi hapa.

Nawasilisha

Mchungaji Ladslaus
 
heshima yako mchungaji,
ulichosema ni kweli kabisa,naona JF inavamiwa sasa,huu uhuru naona wengine wanautumia vibaya
ushauri wangu
kama mtu unaona huna cha kupost basi ni vizuri kuwa msomaji tu,kwani hapa hakuna mashindano ya mabandiko wala hatutafuti mshindi wa bingwa wa mabandiko mengi,ustaarabu tuuweke mbele
 
Mtimti,
Unafikiri huyo mtu ana shida na post nyingi? kafungua account mpya kwa ajili ya kutukana tu, ndiokwanza ana post 2. Nafikiri iwepo restriction sasa, ukitakakujiunga basi utume maombi maalumu. Maana tunatumia vibaya uhuru huu.
 
Jana alitumia jina tofauti na sasa, leo asubuhi ametuma posti karibu kila jukwaa. Ninachoshukuru ni kuwa mods wanazifuta mara anapotuma. Ila ni vyema kukawepo na maombi maalum kama yeyote anataka kuwa 'member' wa JF.

Nawasilisha.

Mchungaji Ladslaus
 
kwani mods anashindwa kuifungia IP ya hiyo computer anayoitumia ili asiweze tena kujiunga,maana najua kuwa hatokuwa na uwezo wa kumiliki computer zaid ya moja
 
Huyo ni taahira. Hapa JF watu tunatofautiana kila siku lakini hatutumii maneno machafu au matusi ya nguoni dhidi ya wale tunaotofautiana nao. Huyo taahira hastahili kuwepo hapa ukumbini.
 
Katika mambo ya usalama hakuna anayependa kukurupuka kuanzia kuban au kufungia watu lazima kwanza unapofanya hivyo uhakikishe ni kwelie huyo unayemdhania ndio anayefanya hivyo ? Au ni ni mwingine anatumia nakii za wengine mfano fulani ameenda internet cafe utaban internet cafe ? Au mtu ameenda chuo utaban chuo ? Lazima mambo haya yaangaliwe inawezekana anayetukana ana malengo yake anataka mwingine ndio afungiwe kwa kutumia vifaa vya mwingine ndio maana mnatakiwa muvute subira

nakumbuka miaka hiyo katika chatroom walikuwa wanakurupuka kuban ip kumbe mtu ameenda internet cafe anatukana unaban internet cafe karibu zote jijini
 
heshima yako mchungaji,
ulichosema ni kweli kabisa,naona jf inavamiwa sasa,huu uhuru naona wengine wanautumia vibaya
ushauri wangu
kama mtu unaona huna cha kupost basi ni vizuri kuwa msomaji tu,kwani hapa hakuna mashindano ya mabandiko wala hatutafuti mshindi wa bingwa wa mabandiko mengi,ustaarabu tuuweke mbele

mchungaji unakumbuka tuliambiwa tusamehe mara 70 ?? Ukipigwa shavu la kushoto mpe la kulia ??

Sasa unalalamika nini
 
Wapendwa Mods na wana JF, mie ninapendekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Mtu mmoja anayeandika thread za matusi na kuposti hapa JF tangia jana.

Kama inawezekana kuwepo na ombi maalum la mtu kujirejista, maana huu uhuru wa kujirejista ndio unaofanya baadhi ya wenzetu wasio na maadili kuandika matusi hapa.

Nawasilisha

Mchungaji Ladslaus

Yakhe Muondosheni hatuifai katika jamvi. Hivi lakini, kwanini atukane!, Hana hoja hana sera huyo.
 
mchungaji unakumbuka tuliambiwa tusamehe mara 70 ?? Ukipigwa shavu la kushoto mpe la kulia ??

Sasa unalalamika nini

Eehee, Ndugu yangu Shy;

Imeandikwa kuwa Mpende Mungu kuliko vyote na Mpende Binadam mwenzako kama unavyojipenda mwenyewe.

Pia imeandikwa kuwa: "Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe".

Mtukanaji yeyote ni Shetani hivyo na huyo anayetukana wenzake ni Shetani.
 
Naona wikiendi ilikuwa patashika sana hapa jamaa na matusi yake tena hakomi kabisa forums zote anapachika tu. hata kama ni ugonjwa wa akili sio vile, frustration zingine zinahitaji mtu uchill kidogo au uende mazoezi namna hii. Naunga mkono ila itakuwa ni ngumu kidogo kuwazuia wenye nia mbaya na pia inaweza kuwanyima wenye mawazo mazuri fulsa ya kuyatoa kwa mda huo. Nafikiri moderators wanafanya kazi nzuri kuondoa threads za namna hiyo.
 
Back
Top Bottom