Hatua muhimu za kuchukua ili kujilinda na athari mbalimbali za El Nino.

carnage21

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
521
1,258
Mamlaka zote za hali ya hewa duniani hujaribu kutahadharisha kuhusu athari za El Nino na kutoa wito wa wananchi kuchukua tahadhari.
Kwa kifupi mbali na hatua zinazofanywa na nchi kupitia Mamlaka zake kwenye kufuatilia tukio hili na kulitolea taarifa mara kwa mara na hatua za kuchukua, mwananchi wa kawaida na yeye ana jukumu la kufanya, ili kujiandaa na kuchukua tahadhari asiathirike na athari zinazoletwa na El Nino.
Baadhi ya hatua za kuchukua, zinazopendekezwa na wataalamu ni;
  • Kuzingatia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini kwako.
  • Kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa watalaamu katika sekta husika ili kupunguza athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa.
  • Epuka kukaa, kutembea sehemu hatarishi kama kwenye mikondo ya maji na umeme hasa kipindi cha mvua na upepo mkali.
  • Kuhama kwenye maeneo ya mabonde hasa nyakati za mvua zinapoanza
  • Wakati wote kuwa na akiba ya chakula, fedha, maji, dawa (kwa maelekezo) na vifaa vya huduma ya kwanza (First Aid Kit).
  • Msaidie jirani yako kwenye dharura.
  • Kuwa na mawasiliano ya watoa huduma za dharura, ya majirani zako na ya kiongozi wako wa eneo unaloishi.
  • Shirikisha majirani, ndugu na jamaa taarifa muhimu kuhusu El Nino.
  • Toa taarifa kwa Mamlaka inapotokea dharura yoyote katika eneo lako unaloishi.
Lets stay put and God bless us.
 
Back
Top Bottom