Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Aisee kwa watengeneza filamu, hii inaweza kuwa bonge la picha kama muswada wako utakamilika una stori za maisha ya kawaida, mapenzi, urongo kidogo yaani imekamilika halafu inaleta hamu ya nini kifuatacho kuanzia kwenye mapenzi, kwenye biashara na maisha mengine ya mtaani!!! Ila Unaweza msaliti kwakuwa wewe hujawa mwenyezi mungu bado upo mawindoni fanya kinachoweza kukuweka sasa!!!
 
Kwa kweli ni more than slow,hii inampunguzia wafuatiliaji wa Uzi wake pendwa,...jitahidi bw BM X6
Mbona ameshatoa ufafanuzi.....Alisema aliandika booonge la gazeti lakini kwa bahati mbaya kwenye notepad aliposave ikajifuta

Kwahyo inampa uvivu,na ameamua kuandika vipande vichache na kuvipost kila anapopata muda
 
Na isipofanya kazi hii mbinu, huoni italeta majanga zaidi? Though lengo langu kuu sio kupita nae
Hapo utakuwa umemshusha confidence na hutamtongoza real kwahiyo hata kusumbua tena , atakuwa mpole kwako,
 
mmash umekuja peke yako huku hatujashtuana ndugu?! Niliiacha kwanza episodes ziwe nyingi ndio nijinafasi, nimeambulia mbili tu haha. Sio mbaya kama ilijifuta kwenye notepad yake.
Vipi lakini kwema?
 
Ilipoishia

Annie: "Sikujua kama unaletaga Wanawake zako humu ndani nikiwa sipo, mwenyewe unajikuta mjanja kuwahi kuwatoa Asubuhi Asubuhi"

BM: "Unajua sikuelewi!"

Annie: "Hunielewi kitu gani Wakati humu Leo umelala na Mwanamke, Jana usiku nimepiga simu yako akapokea huyo mwanamke"

Duh! huyo atakuwa ni Caryn, si nilisahau simu yangu Jana kwenye Gari yao asee, sasa nikawa nawaza jibu la kumpa Annie huku nikiwaza kwann Caryn amepokea simu yangu na atakuwa amemjibu nini Annie hadi amepanic hivi

Muendelezo

SEASON 2 Episode 3

Nikawa nawaza kitu Cha kumuambia Annie, sitaki kumdanganya kwasababu anachofikiria sijakifanya na pia sitaki kumuambia ukweli kwasababu nikifanya hivyo nitasababisha Hawa watu wawili kujuana (Caryn & Annie) kitu ambacho sitaki kitokee

Nikamuuliza Annie "kwani huyo Mwanamke aaliyepokea simu yangu amekujibu nini"

Annie: "Wewe usitake kujua alichonijibu ila Jua tu ni Mwanamke ndio aliyepokea simu, iko wapi kwanza simu yako?"

BM: "Unajua simu yangu jana niliisahau kwa sister, nimefika nyumbani Jana usiku ndio nikajua kwamba simu sina, so huenda labda alipokea sister alijua ni Mimi nampigia"

Annie: "Dada yako yupi unamuongelea hapa?"

BM: "Kwani wewe unamjua yupi? si wa Yombo

Annie: "You're lying BM, Dada yako sauti yake naijua, yule niliyemsikia mimi sio Dada yako kabisa, Kwanza Dada yako tangu lini akaongea Kizungu"

BM: "Ooh, kwahiyo wewe ndio binadamu pekee unaejua kuongea Kingereza sio?"

Annie: "Usi skip the main topic, Ukweli unaujua kwamba Dada yako hajui na wala hawajai kuongea hata sentensi moja ya Kingereza, Sasa yule niliyemsikia kwenye simu ni nani?"

BM: "Sasa mimi nitajuaje wakati simu kama unavyoniona hapa sipo nayo"

Nikaamka nikaingia bafuni kujimwagia Maji faster ili nifanye Mpango wa kuipata simu, nilivyotoka Bafuni nikamuomba Annie simu yake ili nipige namba yangu

Annie: "Tusisumbuane saa hizi, kwanza simu yako haipatikani tangu sijatoka nyumbani nilikuwa naipiga"

Nikajiandaa kwaajili ya kutoka kwenda kwa kina Caryn lakini bado sijapata jibu kwamba kwann Caryn aliamua kupokea simu yangu, kwasababu hatujafika kwenye level ya kuzoeana kiasi hicho, sasa wakati namuaga Annie si akalianzisha tena

Annie: "Unaenda wapi?"

BM: "Si kwa Sister kuchukua simu"

Annie: "Tunaenda wote na mimi nikamsalimie sister, sijaonana nae siku nyingi"

Nikaona huyu ananipima tu kujidai kutaka kwenda kumsalimia sister

BM: "Siendi kwa sister direct kuna mahali naenda kwanza, badae ndio nitapitia kwenda kuchukua simu"

Annie: "huna haja ya kujieleza sana nilijua huwezi kubali kuongozana na mimi kwasababu simu haiko huko unakoniambia"

Nikamuacha japo kibabe nikasepa, nikadaka ndinga hadi kwa Mzee, nilivyoingia tu getini nilivyoona Jeep haipo nikajua moja kwa moja kwamba Caryn nae hayupo, nilifika kwa Mzee mida ya saa 11 am halafu ilikuwa Monday

Nilimkuta Michelle ila Caryn na Mama yake hawakuwepo, japo tangu natoka Tabata nilijua sitamkuta Caryn ila ilinibidi nije ili kuweza kupata namba yake, nikamuomba sister Michelle ampigie kwanza akaguna halafu akanambia

Michelle: "Sasa hivi Caryn yupo Ofisini kwa ninavyomjua yule hawezi kupokea simu especially yangu"

BM: "Kwanini sasa, je kama Kuna Emergency?"

Michelle: "We shika simu jaribu bahati yako"

Kweli nilichukua simu nakumpigia iliita hadi ikakata, nikatakakupiga tena Michelle akanikataza, nikahisi Michelle kidizaini flani kama anamuogopa Caryn, nikapiga tena mara text ikaingia kwenye simu ya Michelle nikampatia simu

Kumbe aliyetuma text ni Caryn, Michelle ananipa simu namuuliza vipi? ananiambia we soma mwenyewe

Baada ya kumpigia simu na kutokupokea akaamua kutuma text "You know I do not appreciate calls like that while I'm working"

Ila Caryn bhana sometimes huwa sijui anajikuta nani?

BM: "Kwahiyo sister Michelle unataka kuniambia huyu mtu akiwa Ofisini huwa hapokei simu yeyote kabisa au ni simu zako tu"

Michelle: "Kuna baadhi ya simu anazipokea kama simu ya Mzee"

BM: "Sasa mm nitapataje simu yangu"

Michelle: "Mtumie msg maana hapo hajui kama ni wewe ndio unamtafuta"

Nikamtumia Caryn ujumbe, kwani ulijibiwa sasa, hadi nikasahau kilichonipeleka kwa Mzee tukapiga sana story na Michelle, nikaanza kumchimba kwann yeye na Caryn haziivi? akanifungukia

Kumbe mchongo ulikuwa hivi, Michelle aliomba pesa kwa Caryn ili afanye Biashara, Caryn akakubali akampa sister wake milioni 11 cash tena akamuambia hakuna ulazima wa kunirudishia hii pesa.

Basi Michelle akachukua kibunda, wiki ya kwanza, ya pili, ya 3 hadi imefika mwezi Caryn akaona hapati feedback yeyote akaanza kumbana sister ake ni Biashara gani hiyo anafanya ambayo yeye hajaiona,

Kila akimbana anaingilia kushoto anatokea kulia, siku moja Caryn akakaza hadi Michelle akafunguka, kumbe Michelle alivyochukua kile kibunda kutoka kwa Caryn moja kwa moja akampelekea bwana ake ndio afanye Biashara

Caryn akasema sio kesi, akataka kuonana na huyo Shemeji yake ili ajue ni Biashara gani hiyo anafanya na maendeleo yake yapoje, mtiti ndio ukaanzia hapa, Michelle ikabidi aongee na bwana ake lakini naye akawa anapigwa chenga, saundi nyingi huku Caryn anataka kujua milioni 11 zimefanya Nini

Kwa mujibu wa Michelle amedai hizi 11 Millions alizotoa Caryn zimetoka kwenye mfuko wa Caryn kabisa binafsi, sio Pesa za Mzee wala sio za Mama, na pia hii issue hadi Sasa hivi wanaijua wao wawili tu wa 3 nikiwa mimi, Caryn hakumuambia Mzee wala Mama yake kwamba kuna pesa kampa Michelle

Sasa Caryn alivyozidi kumbana Dada yake ikabidi Michelle awakutanishe Caryn pamoja na bwana ake, hii yote ni kutaka kujisafisha lakini Michelle hakujua kwamba ndio anamuharibia bwana ake hivyo

Mwisho wa siku Caryn akakutana na Shemeji yake, Sasa bhana kumbe mchizi Pesa kweli alipewa lakini alichokifanya sasa ni kwamba alianzisha mradi wa kufuga kuku, Uzuri anapozifugia hizo Kuna Kuna eneo kubwa tu unaweza kufuga hadi kuku 1,000 lakini kwa mujibu wa Michelle kuku aliokuwa anafuga jamaa hawazidi kuku 200.

Caryn akasoma mchezo akaona Kuna upigaji unaendelea, Milioni 11 kwa kuku 200 tu, mbaya zaidi kumbe Michelle mwenyewe hakujua kama mchizi wake pesa kaiwekeza kwenye kuku, nae ndio ilikuwa mara ya kwanza kuona huo mradi

Caryn akamlaumu Sasa Dada yake kwa uzembe na hiyo yote ni kwasababu Michelle anampenda sana mchizi so Kuna mambo mengine yeye anaweza kuyaona ni ya kawaida kumbe sio kawaida

Alichokifanya Caryn akamuambia Dada yake amuandikie Kila Senti ilivyotumika kwenye ule mradi, Sasa kwasababu Michelle yeye hakufanya manunuzi yeyote kwenye ule mradi ikabidi amuambie Bwana ake alichoambiwa na Caryn, Wakati Caryn anasubiria mahesabu kumbe na yeye kazama chimbo kufanya research zake ili kupata makadirio ya pesa zilizotumika kwenye kale kamradi

Mwisho wa siku Caryn akapata hesabu zake akabaki kusubiria hesabu za upande wa pili, hesabu ya upande wa pili ilivyokuja mkeka unasoma kwamba mradi umetumia milion 8 na milioni 3 zilizobaki zipo bank kwaajili ya ku backup mradi

Unaambiwa Caryn aliisoma Ile karatasi huku anang'ata meno, Michelle anasema ukiwa unaongea na Caryn akaanza kung'ata meno basi ujue hicho unachomuambia tayari kashaanza kukitiria mashaka

Michelle anakuambia Caryn alivyomaliza kusoma Ile karatasi akatingisha tu kichwa akaondoka zake (hakuongea chochote) na tangu siku hiyo wakawa hawapatani kama mwanzo

Tukaendelea na mastory mengine, nikapiga na lunch kabisa, Michelle akanambia nimcheki Caryn tena mida kama hii ndio anaweza kupokea simu, na kweli nilivyopiga akapokea

BM: "Hello"

Caryn: "Sema"

BM: "BM naongea hapa, Sasa rafiki angu huwezi pokea simu na unajua uko na simu yangu huon...."

Caryn: "Wait...simu ni ya kwangu huwezi kunipangia kupokea au kutokupokea"

BM: "Sawa, simu yangu naipataje"

Caryn: "2 hours from now nitakuwa Sinza Dukani"

BM : "Michelle kwanini mdogo wako anaringa sana?"

Michelle: "Hujamzoea tu, ila Caryn ni mtu poa sana mm namuelewa"

BM: "Chukua simu yako bhana acha mm nianze kwenda mdogo mdogo"

Nikaondoka kwa Mzee nikaelekea sinza, nikaenda hadi Dukani, muda ambao nimefika Dukani Caryn alikuwa Bado hajafika, Mdada wa Dukani alishapewa taarifa kwamba kuna mtu atakuja ambae huyo Mtu ndio mm, so nika chill

Punde si punde (sijui nimepatia kiswahili) Caryn akafika, moja kwa moja kapitiliza kwa mfanyakazi wake, baada ya kumalizana nae akanifanyia ishara ya kuondoka, tukatoka Dukani tukaingia kwenye gari

Caryn: "Simu yako hii hapa, Kuna kingine ulisahau?"

BM: "Hakuna, kuna kitu nataka nikuulize?"

Caryn: "Go ahead"

BM: "Jana kuna simu ilipigwa na ukapokea?"

Caryn: "Haijawahi kutokea nikapokea simu isiyonihusu"

BM: "Sasa mbona kuna mtu anadai alinipigia halafu simu ikapokelewa"

Caryn: "Ooh yeah I forgot, wewe jana uliconnect Bluetooth kwenye gari, na hii gari uliconnect Bluetooth simu huwa inajipokea na by the time simu yako inapigwa Mimi nilikuwa naongea na simu, nilikuja kushtuka simu imeshajipokea nikakata"

Maelezo ya Caryn yalijitosheleza na ni kweli Ile gari uki connect Bluetooth simu ikipigwa ndani ya sekunde kadhaa kama hujapokea simu inajipokea, kazi imebaki kwangu kumuelewesha Annie sasa

Nikaachana na Caryn pale pale sinza nikaibuka zangu nyumbani, Annie sikumkuta nikampigia simu nikaongea nae fresh kama hakijatokea kitu

Ilivyofika saa 11pm usiku Annie akaja home na wakati naongea nae kwenye simu nilimuuliza kama anakuja akasema haji.

BM: "Si ulisema hutakuja wewe"

Annie: "Ndio Nimekuja kuna ubaya?"

BM: "Ubaya ni kwamba ungekuja halafu ukanikosa je?"

Annie: "Uzuri ni kwamba funguo ninazo, so ningeingia ndani na kulala"

Conversation flani hivi ilikuwa dry sana, nikaona hapa ngoja nijilalie yasije yakafukuliwa yaliyofukiwa

Asubuhi na mapema Annie ananiomba Hela ya Saloon, nikampatia, baada ya masaa 3 karudi ananipa na taarifa ambayo sikuielewa

Annie: "Babe nimepata kazi, next week natakiwa nikaripoti"

BM: "Ukaripoti wapi?"

Annie: "Mwanza"

BM: "Mwanza? kwanza sijakuelewa"

Annie: "Hujanielewa Nini Sasa hapo"

BM: "Sijakuelewa kwamba unanipa taarifa? unaniaga? au unaomba ruhusa?"

Annie: "Yote majibu"

Nikahisi huyu atakuwa ananipima halafu bado atakuwa na kinyongo juu ya kile kilichotokea jana, Nikamwambia "Sitaki uende hiyo kazi kama ni kazi utafanyia hapa hapa Dar"

Annie: "BM tuongee kama watu wazima, usije ukawa unanipotezea muda nikaja kujutia hizi chance ninazozipoteza Sasa hivi kwaajili yako"

BM: "Mm natoka nikirudi tutaongea vizuri, lakini jua tu hiyo kazi hakuna kwenda"

Nikatoka nikaenda kwa sister kuwacheki madogo na kuweka mambo mengine sawa, Ilivyofika jioni nikaibuka Kinondoni kwa mshkaji wangu, kama kawaida chimbo letu ni Kitambaa cheupe tukachill pale na story mbili tatu

Sasa huyu mwanangu wa dhahabu Kila kinachojiri kwenye maisha yangu lazima nimshirikishe, si nikamu hadithia lile sebene lilinitokea Jana simu kujipokea kwenye gari halafu Annie kusikia sauti ya mwanamke (Caryn)

BM: "Jana usiku kaja kama anataka kufumania Leo Asubuhi ananiambia anataka kwenda Mwanza anadai sijui kapata kazi huko"

Mshkaji: "Wewe ukamjibuje sasa"

BM: "Nitamjibu vipi Sasa zaidi ya kumkatalia"

Mshkaji: "Dah! ila we mwanangu sikufichi unafeli sana, unashindwa kutumia akili yako faster kuendana na mazingira"

BM: "Ebu funguka sijakuelewa"

Mshkaji: "Labda nikuulize wewe, likizo yako inakaribia kuisha umeamuaje kuhusu kazi?"

BM: "Kazi nitapiga kama kawa, nitajua jinsi ya kumpanga yule mtoto (Accountant)"

Mshkaji: "Sasa acha nikupe mchoro mzima, hii ni kama ramani na uko vitani ukikosea kuisoma hii ramani unajikuta kwa adui na kumbuka huna siraha"

Itaendelea
 
Mbona ameshatoa ufafanuzi.....Alisema aliandika booonge la gazeti lakini kwa bahati mbaya kwenye notepad aliposave ikajifuta

Kwahyo inampa uvivu,na ameamua kuandika vipande vichache na kuvipost kila anapopata muda
Tutaendanae hivyo hivyo kwa upole,hatuna namna
 
mmash umekuja peke yako huku hatujashtuana ndugu?! Niliiacha kwanza episodes ziwe nyingi ndio nijinafasi, nimeambulia mbili tu haha. Sio mbaya kama ilijifuta kwenye notepad yake.
Vipi lakini kwema?
Shwari mkuu,pole bana,mi nikajua tuko pa1 kumbe ulikua hujatia timu,....ila hujachelewa mzigo ndo kwaanza umeingia
 
Ila huo mkasa wa michelle na caryn umeurudia tena na ushawahi kuusimulia
 
Back
Top Bottom