Hatimaye rama mla watu na mama yake wameachiwa huru

Fruit

Senior Member
Jan 1, 2013
193
54
KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake Khadija Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu) alifanya kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla Watu, ataendelea kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru watu wengine. Rama alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha mtoto Salome.
 
RAMAMLAVICHWA4.jpg

Aisee
 
anatakiwa amle hakimu kwanza......kumbe sehemu aliyostahili ilikuwa ni hospital na si jela... tanzania bwana.
 
Hat bila kuambiwa, kwa kumwangalia Rama utaona tu kuwa hakuwa na akili timamu. Ila ilishangaza sijui hata kwa miaka yote karibia au mitano alipata huduma ya ugonjwa wa akili. Pole wazazi na ndugu za mtoto Salome. Ila kwa wazazi wote kama una mtoto wako na unaona akili si nzuri ni bora ufanye taratibu apelekwe hospital kwa faida ya familia na jamii kwa ujumla. Ila hakika alitumikia jela sana na mama yake sijui wataanzia tena maisha wapi maana imewavuruga kabisa. Mume sijui atakuwa ameshaoa tayari. My Godness.
 
ingekua zama hizi za udini tingeshamuhukumu Rama kwa dini yake

maajabu yote haya ya Tz kuvunja rekodi ya Dunia yametokea awamu ya nne ya urais....
Wanafunzi kuchora mazombi na mashahiri ya muziki kwenye mtihani wa taifa,

Darasa la 7 kufaulu bila hata ya kujua kuandika,

Twiga kupanda ndege.

Kontena la wizi lenye pembe za ndovu kukutwa china halina mmiliki. N.k
 
Hat bila kuambiwa, kwa kumwangalia Rama utaona tu kuwa hakuwa na akili timamu. Ila ilishangaza sijui hata kwa miaka yote karibia au mitano alipata huduma ya ugonjwa wa akili. Pole wazazi na ndugu za mtoto Salome. Ila kwa wazazi wote kama una mtoto wako na unaona akili si nzuri ni bora ufanye taratibu apelekwe hospital kwa faida ya familia na jamii kwa ujumla. Ila hakika alitumikia jela sana na mama yake sijui wataanzia tena maisha wapi maana imewavuruga kabisa. Mume sijui atakuwa ameshaoa tayari. My Godness.

Ukiangalia dini{UISLAMU} mzee atakuwa kaoa wake 4 wengine!
Pole mama Rama.
 
maza kama kavaa kanga ya sisiemu
Mkuu hizi khanga na t-shirts si ndizo SSM wanadanganyia maskini wa Tanzania kuwa ndiyo maisha bora? Ukimwangalia tu huyu mama na mwanae unaona tu ni kati ya wale watanzania ambao hawana uhakika wa kula milo mitatu kwa siku, angalao!!!! So poor, so weak, but ukifika uchaguzi akipata khanga, kofia, na fulana bila kusahau wali wa maharagwe basi anajua utajiri ameupata. Watanzania wanatakiwa wawe na elimu ya kutosha kuwa uchaguzi ni kitu muhimu na unatakiwa uchague kiongozi atakayeweza kukufikisha mahali fulani kimaendeleo na si kuangali vitu temporary kama nilivyotaja.
 
  • Thanks
Reactions: ilu
Back
Top Bottom