Hatimaye morani wa kimasai waonyesha ishara ya vidole viwili

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
ishara ya vidole viwili inayofanana na herufi V ni ishara inayotumiwa na watu wanaotaka mabadiliko.hapa nchini ishara hii hutumiwa na chama cha chadema ikiwa ni alama rasmi iliyopamba bendera ya chama hiki.

Kwa wale wanaowafahamu wamasai watakubaliana na mimi kwamba ni kabila pekee hapa tanzania au east africa kwa ujumla lisilotaka mabadiliko.
lugha yao,mavazi na mfumo wao wa maisha umepita vikwazo vingi vya mabadiliko.

Leo mgombea ubunge wa arumeru mashariki kupitia chadema ameonekana kukonga nyoyo za morani wa kimasai na kusababisha morani hao kurukaruka, kuinua mikono hewani,kukunja ngumi iliyoacha vidole viwili na hivyo kuunda alama ya mabadiliko.

hatimaye wamasai wamekubali kukombolewa.....!!!

Kwa wachambuzi wa mambo ya saikolojia mtakubaliana na mimi kwamba huu ni ujumbe mkubwa kwa chama tawala huko arumeru.

Naomba mwenye video clip ya taarifa ya habari ya itv leo usiku aiweke ili tujionee uhondo.
 
Mabadiliko hayako mbali hata kidogo!

Hakika pale Arumeru Mashariki mabadiliko ni sasa!

Hakuna lisilowezekana kwa sasa!
 
Ccm wamekuwa wakiwaburuza sana hawa jamaa, wanaanza kuelewa Mungu awajalie
 
Hii ni habari murua sana hata mimi leo nimeona hii itv ilikuwa ni katika kijijij cha Ngabobo..

jamani mnashabikia vidole vya wamasai wakati mnahakika hawatapiga kura! je wako kwenye daftari? hati zao hazijanunuliwa? vidole viwili bila kura ni kujilisha upepo!

 
jamani mnashabikia vidole vya wamasai wakati mnahakika hawatapiga kura! je wako kwenye daftari? hati zao hazijanunuliwa? vidole viwili bila kura ni kujilisha upepo!


Ni kweli...ukombozi kamili upo kwenye kujiandikisha, kuitunza shahada na mwisho kupiga kura...lakini hata hivyo vidole viwili na umati wa watu ishara nzuri ya kuleta mabadiko kama wahusika watatumia fursa kama hizi kuwaelewesha umuhimu wa kupiga kura...!
 
Ni habari nzuri, wamasai wanaishi mfumo wa age set. Basi kuna rika linaloitwa KORIANGA na ndo jeshi la kimasai kwa sasa ndio wameamua kubadilika baada kuchoshwa kazi ya ulinzi.
 
Watapiga kura? Au ndiyo wale wanakimbilia mjini na kuanza kusuka dada zetu kwa kuwapakata miguuni kwao huku wakiwa ....?
 
Back
Top Bottom