Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

hapa alipo - tunamsubiria tu afanye his first move kwanza.

Tik tak tik tak tik tak
Naona yuko busy kwenye vikao vya kimataifa hususan Zimbabwe!I am keeping my fingers crossed so that he can remember walalahoi's frustrations!
Pia tusisahau kuwa Zitto naye yuko around..so incase Mr President is way tooo busy..then should we consult Mr Zitto to see how he can help?
 
Kuna swala Kitila alisema hapa kwapa tusipo halibu mazalia ya rushwa bado watazaliana tu,sasa hii tume na ripot yake inakuja kututia uchungu tu hapa, halafu baada ya hiyo tume what next wata commit to another commitee, baada ya hile ya mwakyembe naye bro Binda kaunda yake basi ndiyo maana wana endelea kucommit mi-sin.
 
Kama sijakosea, ripoti hiyo inatakiwa iwe na information zote from how the whole corruption happened in regard to the contract signing with the Mining Companies...how the deals are unfavorable to the inhabitants pamoja na mapendekezo ya kisheria ya namna ya kutatua matatizo yanayohusiana na sheria za madini.Na pia to see if the contract signers could be brought to justice as long as the committee's findings includes the possibilty of corruption during decission making!If i am wrong naomba nifahamishwe!
 
Hata kama hiyo ripoti inakaliwa we still can do something!
M.wa Kike kwanini Zitto asitueleze kama findings za kamati zinaonyesha kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa?
Sidhani kama atakuwa amekiuka maadili..kwasababu hatutaki atueleze siri za vikao!Bali atueleze kama kulikuwa na mazingira ya rushwa wakati wa kusaini mikataba hiyo!
Hilo litatusaidia kujua kuwa Mh Rais anatakiwa awachukulie hatua wale wote waliohusika na uhusikaji huo wa rushwa wakati wa kusaini mikataba hiyo ya madini.

Jambo ambalo liko wazi ni kuwa sheria zinahitaji marekebisho ili kuweza kutokomeza mianya hiyo iliyotumika!
Hilo haliwezi kumaanisha kuwa wale wote walio itumia mianya hiyo kujinufaisha hawatatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria!
Accountability ni jambo ambalo tutalipigia kelele no matter whats in the report!Hilo liko wazi!
Tunasubiri kuona mambo!
 
Hata kama hiyo ripoti inakaliwa we still can do something!
M.wa Kike kwanini Zitto asitueleze kama findings za kamati zinaonyesha kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa?
Sidhani kama atakuwa amekiuka maadali..kwasababu hatutaki atueleze siri za vikao!Bali atueleze kama kulikuwa na mazingira ya rushwa wakati wa kusaini mikataba hiyo!
Hilo litatusaidia kujua kuwa Mh Rais anatakiwa awachukulie hatua wale wote waliohusika na uhusikaji huo wa rushwa wakati wa kusaini mikataba hiyo ya madini.

Jambo ambalo liko wazi ni kuwa sheria zinahitaji marekebisho ili kuweza kutokomeza mianya hiyo iliyotumika!
Hilo haliweza kumaanisha kuwa wale wote walio itumia mianya hiyo kujinufaisha hawatakiwi kuchukuliwa hatua za kisheria!
Accountability ni jambo ambalo tutalipigia kelele no matter whats in the report!Hilo lio wazi!
Tunasubiri kuona mambo!

Mkuu wangu Mushi,

Najua kwa hakika kuwa hata zitto angependa sana kutoa report ya kamati hiyo hapa ili ikasomwa. Lakini of all pple mimi nisingemshauri afanye hivyo kwa sasa.

Kadri Kikwete anavyochelewa kutoa hii report ndio inaonyesha yeye ni mtu wa namna gani kwenye hili suala. So far bado nalia na Kikwete atoe findings kwenye hii report ili zijulikane.
 
What about majukumu halisi ya kamati hiyo ili tujue kama tuendelee na count down ama la?
Dont you remember how many times tumejaribu kumuomba Mh Zitto aje hapa kutueleza responsibility hasa na madhumuni ya kamati yao?.Tunajua ina kazi ya kutoa mapendekezo ya kisheria!
Je walikuwa pia na majukumu ya kupendekeza hatua za kuchukuliwa dhidi ya wale waliohusika na rushwa kwenye mikataba?
Majukumu ya kamati yakiwekwa wazi haina maana kuwa Zitto atakuwa ametoa siri yoyote ya ripoti ya kamati kabla ya Rais!
Hilo litatusaidia sana!
 
Last time Kikwete alisema kuwa kamati ilishamaliza kazi na imemkabidhi report. So countdown bado inaendelea. Nadhani sio fair kwa Zitto kuja hapa kuongelea hili wakati bado Kikwete hajatoa tamko rasmi.

Hata hivyo ni vizuri tukiendelea kumuomba aje labda anaweza kudefy convention wisdom ya kamatis na akamwaga yaliyojiri.
 
Hatakuwa amedefy convention wisdom yoyote ile ya kamati kama akitueleza agenda na madhumuni halisi ya shughuli nzima ya kamati yao hiyo ya rais!
Hilo si ni haki ya wananchi ama?
Naomba tuelimishane kwenye hili!
Navyoona mh rais hawezi kuitoa hiyo ripoti hivi karibuni kwasababu si unakumbuka ya epa?
Zitto kama mwakilishi wetu sisi watu wa kawaida ndio tegemeo letu!
Na principle aliyoionyesha bungeni inahitajika kwenye hili pia!
 
ban_zitto.jpg

Hoja Binafsi ya kuunda kamati teule ya Bunge kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini Karamagi ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais​

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB)​

MHESHIMIWA Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako tukufu, nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…naomba kutoa taarifa rasmi… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba ya madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Disemba, 2005.’ Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.
Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007, nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:
  1. Kuondolewa kwa kipengele katika sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako tukufu.
  2. Kusainiwa kwa mkataba mpya wa madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London, Uingereza, na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo:

a. Kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, ninanukuu: “…kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa bungeni mwaka 2001 kwenye bajeti kikabadilishwa…” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.

Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14 ya 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninanukuu:
‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act.’
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/199 kinazungumzia mrahaba wa madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge?

Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Basili Mramba.

“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
(v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002, nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya madini haitajwi.

Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?

Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya waziri ni ya kweli. Je, kwa nini makampuni ya madini ambayo yameingia mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?

Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini, unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati Teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya serikali na ufisadi.

b. Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.
Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya migodi, mgodi wa Buzwagi ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya sasa ya bei ya dhahabu, uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani.’ Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa, ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.

Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya, ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je, waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?

Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio mgodi.

Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya Barrick Gold Corporation-Global operations-Africa- Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii ninaiambatanisha katika hoja hii.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick, Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninanukuu. ‘A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive EIA approval.’
Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, je, serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na Kampuni ya Barrick? Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?

Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za Kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za Kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je, ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Tulawaka na North Mara?

Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/9, pamoja na mambo mengine kinataka leseni yoyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.

Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa?

Mheshimiwa Spika, sheria ya madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za kiserikali, kama kamati ikimshauri waziri na waziri akakataa ushauri huo, inampasa waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. (1)Je, waziri alifuata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka wa kusaini mkataba huu?

Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. (2)Ni mingapi kati ya mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa mkataba kusaniwa Uingereza? Je, mkataba umeandikwa “signed in London...” au “signed in Dar es Salaam...? (3Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.

Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini wabunge wataamua kwa maslahi ya taifa letu.(4) Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.

…………………………….
KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI
Mh Zitto kwa mara nyingine natoa changamoto.
Nime highlight baadhi ya pointi na kuzipa red numbers ili kuona kama ungeweza kutueleza kama hayo maswali uliyokuwa ukiyauliza kule bungeni uliyafanyia kazi kwenye kamati hiyo ya rais!
Nimejaribu kuona kama ungeweza kutueleza lakini naona umegoma kabisa!
Cha muhimu hata kama usiposema chichote tunaomba tu utuhakikishie kwamba moyo ule ule uliouonyesha kule bungeni ndio ule ule uliokuwa nao kamatini!
Kilio chako cha kamati teule ya bunge kilizimwa na uamuzi wa Mh Rais kuunda kamati!
Kulikuwa na migongano kwamba either ukubali wito huo ama la!
Nilikuwa upande wako hapa jf na kuwahahkikishia wana jf kuwa you have principle based on your own comments!
Tueleze tu kama bado upo upande wa Wananchi!
Akhsante
Jmushi1
 
Ni makusudi yangu kuhakikisha kwamba tunaendelea na mjadala wa kamati ya Rais
Hivyo basi,Mh Zitto akiwa kama mmoja wa wanakamati hao ambaye pia ni wazi kwa kiasi kikubwa;hoja yake ya kamati teule kule bungeni ilichangia maamuzi ya Mh Rais kuiunda kamati hiyo.

Ni wazi kwamba kamati hii imeundwa mara baada ya mzozo kuwa mkubwa,mzozo ambao wakina Zitto waliuanzisha kule bungeni kutokana sakata la "UFISADI"? na mikataba mibovu ya madini.
Nimeamua kum"quote"Mh Zitto pale alipokuwa akisisitiza ni kwanini ali"walk out"kule bungeni pale alipoibua issue hii kule bungeni, na sababu aliyoitoa ni ya kwamba yeye ni mtu mwenye "PRINCIPLE"ambapo yeye mwenyewe aliwarahisishia wasomaji kwa kuwapa definition sahihi kwamba ni"MISIMAMO ISIYOYUMBA"

Kwa maana nyingine ni kwamba;alikuwa radhi kuyatema maslahi yake binafsi kama vile posho na mishahara,kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wote!thats a principle,hakubadili msimamo..na ndio maana nafikiri CHADEMA wanamuaminia baba lao Mh Zitto kwamba atarepresent maslahi ya taifa,hata humo kamatini.
Natumia fursa hii kuwaalika wana forum wote kuchangia wakati huu ambapo CHADEMA wameshatoa msimamo wao kuwa wanamsapoti Mh ZittoHivyo ni wazi kwamba kazi inaanza mara moja.

Tunatumia pia fursa hii kumshawishi Mh Zitto aendelee kuwa mtu mwenye principle kama ambavyo tume mquote,na kwamba tunafuatlia kwa makini kwani bado hatujajua kazi halisi watakayoifanya.

Hivyo basi tunaomba aendelee kuwa na principle ileile aliyokuwa nayo huko bungeni pale atakapoanza kazi humo "KAMATINI"Tumejaribu mara nyingi kuona kama Mh Zitto angewasili hapa jamvini ili kulonga na wana jf kwamba ni nini haswa anachokwenda kufanya humo kamatini,kwakuwa hakufanya hivyo..then basi mjadala unaanza na tunategemea kuwa tutaendelea kuchangia kuanzia sasa hadi hapo kamati hiyo itakapo wasilisha ripoti yake kwa Mh Rais.

Thread hii sijaifunga,kwani bado sijajua tarehe kamili kamati hiyo itakapo"wrap up"na kuwasilisha kwa mkuu matokeo ya hiyo "assignment yao"Haya tena wana forum..mchango wenu,na pia changamoto kwa mbunge wetu huyu kijana,machachari,mwenye uchungu na maslahi ya wananchi na taifa lake kwa ujumla..!unakaribishwaMh Zitto uje utueleze kama bado wew ni mtu mwenye "PRINCIPLE".

Mh Zitto..
Posting ya kwanza siku thread hii ilipofunguliwa mara baada ya mjadala wa kamati kwisha na kukubaliana kwa pamoja kuwa wewe ni mwakilishi wetu huko kamatini!
 
Kamati Maalum ya kupitia mikataba ya madini bado kukabidhi ripoti
Na Kizitto Noya

KAMATI Maalum ya kupitia upya mikataba ya madini haijakabidhi ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete tangu ilipokamilisha kazi yake Aprili 10, mwaka huu.

Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Mark Bomani zimesema kuwa mpaka sasa ripoti hiyo haijamfikia Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa Jaji Bomani baada ya kumaliza kazi ya kuandaa ripoti hiyo, kamati imeomba miadi ya kukutana na rais Kikwete ili ikamkabidhi ripoti hiyo na sasa inasubiri wito wake kwa ajili ya makabidhiano hayo.

"Ni kweli kazi imekamilika, lakini sijaikabidhi, nimeomba kukutana na Rais ili nimkabidhi. Nasubiri wito wake," alisema Jaji Bomani.

Kazi ya kuangalia upya mikataba ya madini imeichukua kamati hiyo yenye wajumbe kumi moja miezi sita kuikamilisha badala ya miezi mitatu kama alivyoelekeza Rais Novemba 13, mwaka jana alipoiunda kamati hiyo.

Mbali na Bomani, wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera katika Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Rais Kikwete alitaka kamati hiyo pamoja na mambo mengine kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Rais pia aliitaka kamati hiyo kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo ya kuboresha mikataba ya madini.

Kuundwa kwa Kamati hiyo kulifuatia hoja binafsi ya Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, nchini Uingereza na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi mwaka jana.
 
Mh Zitto kwa mara nyingine natoa changamoto.
Nime highlight baadhi ya pointi na kuzipa red numbers ili kuona kama ungeweza kutueleza kama hayo maswali uliyokuwa ukiyauliza kule bungeni uliyafanyia kazi kwenye kamati hiyo ya rais!
Nimejaribu kuona kama ungeweza kutueleza lakini naona umegoma kabisa!
Cha muhimu hata kama usiposema chichote tunaomba tu utuhakikishie kwamba moyo ule ule uliouonyesha kule bungeni ndio ule ule uliokuwa nao kamatini!
Kilio chako cha kamati teule ya bunge kilizimwa na uamuzi wa Mh Rais kuunda kamati!
Kulikuwa na migongano kwamba either ukubali wito huo ama la!
Nilikuwa upande wako hapa jf na kuwahahkikishia wana jf kuwa you have principle based on your own comments!
Tueleze tu kama bado upo upande wa Wananchi!
Akhsante
Jmushi1

Mushi,
Niliwahi kuonya hapa mtandaoni kuwa hizi safari-safari anazopewa Zitto zinaweza zikawa zimefungiwa ndoana kumnasa mheshimiwa. Tokea amalizane na kamati ya madini, Mh. Zitto amekuwa kimya sana. Kuna wabunge wengi vijana tulio nao sijui US embassy walitumia kigezo gani ili kumpata Zitto kuja training USA. Natumaini ninayosema sio utabiri wa kweli maana kama ikawa kweli, itawafadhaisha sana vijana wengi.
 
Nipo na wananchi na nitaendelea kuwa na wananchi. Siwezi kutoa taarifa za kamati kabala ripoti haijakabidhiwa. Vuta subira. Inabidi nitumie busara na hekima. Tusubiri ripoti. Tuemjibu maswali mengi zaidi ya hayo maana hatukuangalia Buzwagi tu, bali mikataba yote na kutoa mapendekezo ili nchi ifaidike na madini yetu.
 
Mushi,
Niliwahi kuonya hapa mtandaoni kuwa hizi safari-safari anazopewa Zitto zinaweza zikawa zimefungiwa ndoana kumnasa mheshimiwa. Tokea amalizane na kamati ya madini, Mh. Zitto amekuwa kimya sana. Kuna wabunge wengi vijana tulio nao sijui US embassy walitumia kigezo gani ili kumpata Zitto kuja training USA. Natumaini ninayosema sio utabiri wa kweli maana kama ikawa kweli, itawafadhaisha sana vijana wengi.

Sijui unawaza nini? Sikuelewi. Ila tu ujue kuwa sijawahi kuwa msaliti na mimi ni mtu mwenye misimamo isiyoyumba. Safari hii kuna wengi tu ambao wamewahi kuja. Mnyika alikuja mwaka 2006, kabla yangu, sasa sijui yeye ilitumika vigezo gani. Nadhani tuache utabiri
 
Mushi,
Niliwahi kuonya hapa mtandaoni kuwa hizi safari-safari anazopewa Zitto zinaweza zikawa zimefungiwa ndoana kumnasa mheshimiwa. Tokea amalizane na kamati ya madini, Mh. Zitto amekuwa kimya sana. Kuna wabunge wengi vijana tulio nao sijui US embassy walitumia kigezo gani ili kumpata Zitto kuja training USA. Natumaini ninayosema sio utabiri wa kweli maana kama ikawa kweli, itawafadhaisha sana vijana wengi.

Kwa sababu Zitto anafanya kazi nzuri kuliko hao vijana wengine unaowataja.

Get it?
 
Kamati Maalum ya kupitia mikataba ya madini bado kukabidhi ripoti
Na Kizitto Noya

KAMATI Maalum ya kupitia upya mikataba ya madini haijakabidhi ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete tangu ilipokamilisha kazi yake Aprili 10, mwaka huu.

Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Mark Bomani zimesema kuwa mpaka sasa ripoti hiyo haijamfikia Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa Jaji Bomani baada ya kumaliza kazi ya kuandaa ripoti hiyo, kamati imeomba miadi ya kukutana na rais Kikwete ili ikamkabidhi ripoti hiyo na sasa inasubiri wito wake kwa ajili ya makabidhiano hayo.

"Ni kweli kazi imekamilika, lakini sijaikabidhi, nimeomba kukutana na Rais ili nimkabidhi. Nasubiri wito wake," alisema Jaji Bomani.

Kazi ya kuangalia upya mikataba ya madini imeichukua kamati hiyo yenye wajumbe kumi moja miezi sita kuikamilisha badala ya miezi mitatu kama alivyoelekeza Rais Novemba 13, mwaka jana alipoiunda kamati hiyo.

Mbali na Bomani, wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera katika Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Rais Kikwete alitaka kamati hiyo pamoja na mambo mengine kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Rais pia aliitaka kamati hiyo kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo ya kuboresha mikataba ya madini.

Kuundwa kwa Kamati hiyo kulifuatia hoja binafsi ya Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, nchini Uingereza na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi mwaka jana.

Hii sasa inatisha,

kamati ilitakiwa kumaliza kazi mwezi wa tatu, ikaomba muda hadi tarehe 10 mwezi wa nne, na huu ni mwezi wa tano bado hakuna kitu.

Navuta pumzi kabla ya kuanza kushout hapa kuwa I told you so!!!! gademu!
 
Back
Top Bottom