Hatimaye CCM walitwaa Jimbo la Nassari, John Pallangyo apita bila kupigwa

Wacha ukorofi wako best

BTW hebu nieleweshe mwenzio maana niko outdated,inamaana huyo ndo kashakua mbunge mteule anasubiri tu kuapishwa ama tusubiri kampeni as usual?

Tatizo huu uzee unanijia kwa speed ya mwanga wa radi nakua mzito kuelewa lol

Yap, huyo ndio kapitishwa, na mgombea wangalau ambaye angeweza kuleta ushindani ni wa cdm na cdm wamejitoa. Hao wa vyama vingine wamepewa hela wajaze fomu kwa kukosea ili huyo mgombea wa ccm apite bila kupingwa. Hivyo hakuna kampeni kwani hata ccm hawataki uchaguzi maana wanajua watafedheheka kwani watu wamepuuza kwenda kupiga kura, hivyo wanaona aibu idadi kuwa ndogo kuwa ni majibu tosha kwamba hawakubaliki.

Kimya sana siku hizi, nini shida best?
 
Mimi jinsi Nasari alivyonichefua sijaumia..ngoja akalee mke vzr

Ni KWELI kabisa, ila kwa upande mwingine, hakuna kitu muhimu kama familia. Familia kwanza, mengine baadaye. HATA maandiko yanasema asiyewatunza walio wa kwake, huyo ni mbaya KULIKO asiye amini.
 
John Pallagyo aliyekuwa anagombania Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM amepita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa, Msimamizi wa Uchaguzi, Emmanuel Mkongo ametangaza

Jimbo la Arumeru Mashariki lilitangazwa kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADAMA, Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge kwa kutokuhudhuria Mikutano mitatu ya Bunge

Nassari baada ya kuvuliwa Ubunge alifanya taratibu za kwenda Mahakamani na kufungua shauri la kuomba kufungua kesi ya msingi ya kumtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kutengua uamuzi wake lakini jitihada zake ziligonga mwamba
======

Arumeru. Mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pallagyo amepita bila kupigwa katika nafasi hiyo baada ya wagombea wenzake 10 kushindwa kukidhi vigezo.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Emmanuel Mkongo amesema hayo Leo Ijumaa Aprili 19, 2019 wakati akitangaza matokeo baada ya upitiaji wa fomu zilizowasilishwa .

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Akizungumza baada ya mkurugenzi kumtangaza kuwa kapita bila kupingwa, pallagyo, amekishukuru chama chake kwa kumuamini na amesema atahakikisha anafuata nyayo za Rais John Magufuli katika utendaji kazi.

“Pia nitamkumbusha Rais ahadi yake aliyoitoa ya ujenzi wa barabara ya kilometa tano za lami jimboni humo na nitahakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano ndani ya muda mfupi,” amesema.

Naye Mmoja wa wagombea kutoka chama cha Demokrasia Makini, Saimon Ngilisho ameunga mkono uamuzi huo huku akikiri kukosa wadhamini kutokana na wananchi kukatishwa tamaa na wapinzani kujiuzulu kabla ya muda wao kufika, hivyo kusababisha kukosa sifa za kugombea.
Ni sawa sawa na kunsifu baba yako ni bigwa wa mashindano ya kunywa pombe. Hizi ni zile sifa ambazo zinarudisha nchi yako nyuma lakini hujui kwasababu ya kulewa siasa.
 
POLITICAL HYPOCRISY
 
Duu! Hii ndiyo aina mpya ya demokrasia ya Tz chini ya mtakatifu jiwe! R.I. P demokrasia
 
Huyu Bwana wa Demokrasia Makini pamoja na hao wenzake 10 ambao wameshindwa kujaza fomu ipasavyo nao wanataka kuongoza wananchi badala ya kuhangaika kujiongoza wao wenyewe ili wawe na weledi angalau wa kutosha hata wa kujaza hizo fomu. Yaani, hawa wanasiasa ni pasua kichwa. Maana unatamani kuajiriwa ili hali basics za kupata ajira hawataki kuzijua. Hii ni zaidi ya ushirikina
John Pallagyo aliyekuwa anagombania Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM amepita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa, Msimamizi wa Uchaguzi, Emmanuel Mkongo ametangaza

Jimbo la Arumeru Mashariki lilitangazwa kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADAMA, Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge kwa kutokuhudhuria Mikutano mitatu ya Bunge

Nassari baada ya kuvuliwa Ubunge alifanya taratibu za kwenda Mahakamani na kufungua shauri la kuomba kufungua kesi ya msingi ya kumtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kutengua uamuzi wake lakini jitihada zake ziligonga mwamba
======

Arumeru. Mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pallagyo amepita bila kupigwa katika nafasi hiyo baada ya wagombea wenzake 10 kushindwa kukidhi vigezo.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Emmanuel Mkongo amesema hayo Leo Ijumaa Aprili 19, 2019 wakati akitangaza matokeo baada ya upitiaji wa fomu zilizowasilishwa .

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Akizungumza baada ya mkurugenzi kumtangaza kuwa kapita bila kupingwa, pallagyo, amekishukuru chama chake kwa kumuamini na amesema atahakikisha anafuata nyayo za Rais John Magufuli katika utendaji kazi.

“Pia nitamkumbusha Rais ahadi yake aliyoitoa ya ujenzi wa barabara ya kilometa tano za lami jimboni humo na nitahakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano ndani ya muda mfupi,” amesema.

Naye Mmoja wa wagombea kutoka chama cha Demokrasia Makini, Saimon Ngilisho ameunga mkono uamuzi huo huku akikiri kukosa wadhamini kutokana na wananchi kukatishwa tamaa na wapinzani kujiuzulu kabla ya muda wao kufika, hivyo kusababisha kukosa sifa za kugombea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha ....Hiyo ndio tofauti ya mgombea halali na wakuchaguliwa na Ccm, mgombea aliye pitishwa na wananchi huwa anawashukuru wananchi ila huyu anakishukuru chama na Magu......com hoyeee
 
Nilitegema hili lililotokea, ila mwenye akili aambiwi fikilia na mwenye macho aambiwi tazama.

Mwanzo wa utungu huwa ni maandalizi ya kupokea kitu kinyemi.
 
Hahaha ....Hiyo ndio tofauti ya mgombea halali na wakuchaguliwa na Ccm, mgombea aliye pitishwa na wananchi huwa anawashukuru wananchi ila huyu anakishukuru chama na Magu......com hoyeee
Ni ukweli ulio wazi kuwa hakupigiwa kura na mwananchi hata moja, sasa atawashukuru vipi wananchi kama wote walimnyima kura? Anaingia bungeni kumwakilisha dikteta uchwara na vifaranga vyake huko Lumumba hivyo lazima shukhrani zielekezwe huko.
 
Huu nao utaitwa ushindi wa kishindo. Duh this is Tanzania bhana. Nchi yenye maajab daily.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mnakwepa kulaumu chanzo cha tatizo badala yake mnalaumu mgombea wa CCM. Lawama zote ni kwa Nasari. Kama kafika bei au kweli alikuwa na matatizo ya kifamilia bado lawama ni zake. Hata kama alikuwa na matatizo ya kifamilia lakini alijua utaratibu ukoje. Hata kama alikuwa na matatizo ya kifamilia huwezi kukosa mikutano mitatu ya bunge japo kuja kusaini na kusepa au kuandika barua kwa spika mapema pengine hata kabla ya vikao vya bunge kuanza. MCHUMA CHANGA HULA NA WA KWAO!
 
John Pallagyo aliyekuwa anagombania Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM amepita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa, Msimamizi wa Uchaguzi, Emmanuel Mkongo ametangaza

Jimbo la Arumeru Mashariki lilitangazwa kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADAMA, Joshua Nassari kuvuliwa Ubunge kwa kutokuhudhuria Mikutano mitatu ya Bunge

Nassari baada ya kuvuliwa Ubunge alifanya taratibu za kwenda Mahakamani na kufungua shauri la kuomba kufungua kesi ya msingi ya kumtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kutengua uamuzi wake lakini jitihada zake ziligonga mwamba
======

Arumeru. Mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pallagyo amepita bila kupigwa katika nafasi hiyo baada ya wagombea wenzake 10 kushindwa kukidhi vigezo.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Emmanuel Mkongo amesema hayo Leo Ijumaa Aprili 19, 2019 wakati akitangaza matokeo baada ya upitiaji wa fomu zilizowasilishwa .

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Akizungumza baada ya mkurugenzi kumtangaza kuwa kapita bila kupingwa, pallagyo, amekishukuru chama chake kwa kumuamini na amesema atahakikisha anafuata nyayo za Rais John Magufuli katika utendaji kazi.

“Pia nitamkumbusha Rais ahadi yake aliyoitoa ya ujenzi wa barabara ya kilometa tano za lami jimboni humo na nitahakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano ndani ya muda mfupi,” amesema.

Naye Mmoja wa wagombea kutoka chama cha Demokrasia Makini, Saimon Ngilisho ameunga mkono uamuzi huo huku akikiri kukosa wadhamini kutokana na wananchi kukatishwa tamaa na wapinzani kujiuzulu kabla ya muda wao kufika, hivyo kusababisha kukosa sifa za kugombea.
 
Subiri wajuz wa mambo

Back
Top Bottom