Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe, Ndugu Frolian Kimaro baada ya malumbano marefu, ambapo mamlaka zinazohusika zilikuwa zimekataa kuipokea.

Katika rufaa hiyo Mgombea Bi. Saguti anapinga, pamoja na masuala mengine, uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa amepita bila kupingwa, huku kukiwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi nchini.

Hadi mwisho wa kupokea rufaa hiyo ulipokuwa unakaribia jioni hii, kwa mara nyingine tena uteuzi wa mgombea huyo wa CHADEMA ulikuwa bado unawekewa vikwazo baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kukataa kupokea fomu hiyo tangu mchana.

Mgombea huyo akiambatana na Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, walifika ofisini kwa msimamizi leo mchana kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo hali iliyoonesha kuwa kuna dalili za kuhakikisha uamuzi wa juzi haubadiliki ili CCM ipite bila kupingwa katika jimbo hilo.

Fomu hiyo na. 12 ilipatikana jana kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya Uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kulazimika kufanya mawasiliano ili kupata fomu hiyo kutokana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe kukataa kutoa.

Chama tayari kimeshamwandikia rasmi Mkurugenzi wa NEC kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe hasa kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu zinazosimamia uchaguzi kwa kukataa kupokea fomu za kugombea za Mgombea wa CHADEMA na vyama vingine huku akimtangaza Mgombea wa CCM kupita bila kupingwa kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Tumaini Makene
 
Kuna Uzi ulifunguliwa hapa ukionyesha kwamba NEC inaunga mkono maamuzi ya mkurugenzi wa Korogwe kumtangaza mgombea wa ccm kupita bila kupingwa.

Sasa huyo kaimu mkurugenzi kapata wapi mamlaka ama maagizo ya kupokea rufaa?

Halafu leo ni sikukuu, sasa huyo kaimu mkurugenzi amefanya maamuzi hayo akiwa nyumbani?
 
Duh......

Hatimaye figisu figisu za CCM zimeshindwa!

Na hatimaye wale "wanaoculude" na CCM nao watajitoa na si wengine Bali ni Wasimamizi wa Uchaguzi+ Polisi+Immigration
 
Kuna Uzi ulifunguliwa hapa ukionyesha kwamba NEC inaunga mkono maamuzi ya mkurugenzi wa Korogwe kumtangaza mgombea wa ccm kupita bila kupingwa.

Sasa huyo kaimu mkurugenzi kapata wapi mamlaka ama maagizo ya kupokea rufaa?

Halafu leo ni sikukuu, sasa huyo kaimu mkurugenzi amefanya maamuzi hayo akiwa nyumbani?
Kwa sheria za uchaguzi, NEC inalazimika kufanya kazi siku zote kuanzia tarehe ya iteuzi mpaka siku ya kutangaza mshindi. Ndiyo maana iwe Jumapili, sikukuu au Jumamosi, siku zote kampeni huendelea na NEC inalazimika kuwa kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe, Ndugu Frolian Kimaro baada ya malumbano marefu, ambapo mamlaka zinazohusika zilikuwa zimekataa kuipokea.

Katika rufaa hiyo Mgombea Bi. Saguti anapinga, pamoja na masuala mengine, uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa amepita bila kupingwa, huku kukiwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi nchini.

Hadi mwisho wa kupokea rufaa hiyo ulipokuwa unakaribia jioni hii, kwa mara nyingine tena uteuzi wa mgombea huyo wa CHADEMA ulikuwa bado unawekewa vikwazo baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kukataa kupokea fomu hiyo tangu mchana.

Mgombea huyo akiambatana na Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, walifika ofisini kwa msimamizi leo mchana kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo hali iliyoonesha kuwa kuna dalili za kuhakikisha uamuzi wa juzi haubadiliki ili CCM ipite bila kupingwa katika jimbo hilo.

Fomu hiyo na. 12 ilipatikana jana kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya Uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kulazimika kufanya mawasiliano ili kupata fomu hiyo kutokana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe kukataa kutoa.

Chama tayari kimeshamwandikia rasmi Mkurugenzi wa NEC kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe hasa kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu zinazosimamia uchaguzi kwa kukataa kupokea fomu za kugombea za Mgombea wa CHADEMA na vyama vingine huku akimtangaza Mgombea wa CCM kupita bila kupingwa kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Tumaini Makene
Makene hapo ni sawa na kuahirisha maumivu tu au ule usemi wa kuanua ngoma juani kama huyo msimamizi ndiye anategemewa kumtangaza mshindi unategemea atamtangaza huyo diwani wetu hata kama atashinda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Uzi ulifunguliwa hapa ukionyesha kwamba NEC inaunga mkono maamuzi ya mkurugenzi wa Korogwe kumtangaza mgombea wa ccm kupita bila kupingwa.

Sasa huyo kaimu mkurugenzi kapata wapi mamlaka ama maagizo ya kupokea rufaa?

Halafu leo ni sikukuu, sasa huyo kaimu mkurugenzi amefanya maamuzi hayo akiwa nyumbani?
Kipindi cha uchaguzi ofisi zinatakiwa kuwa wazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aibu tupu nchi hii
Hawa jamaa wanatia hasira sana,kama hawataki upinzani wapeleke muswada bungeni wabadili katiba/sheria tuwe na chama kimoja tu basi ili tusiwe tunapoteza mabilioni ya pesa kwenye uchaguzi hewa,watu wamekuja kuleta fomu tangia saa nne asubuhi,mkurugenzi hayupo anapigiwa simu analeta tantalila/bla bla bla unafika mda unajitokeza ukiwa na madifenda utafikiri unasindikiza fedha za posho jeshini na kusema mda umeisha,It is B.S
 
Back
Top Bottom