Elections 2010 Hatima ya wafanyakazi serikalini Dr. Slaa akishinda ni ipi?

schulstrasse

Senior Member
May 31, 2010
108
0
Nini hatima ya wafanyakazi serikalini endapo CHADEMA itashinda??manake naona kama kuna wizara na vitengo vitafutwa kwenye serikali mpya ya chadema, nini hatima yetu au wasi wasi wangu tuu??
 
Yakitokea mabadiliko wafanyakazi wanaweza kupewa majukumu mengine. Hivi Chamema wanazungumzia sera ya 'redundancy?' Mi nadhani wanataka kupunguza matumizi kwa ngazi za juu (vigogo) kwa hiyo kama una ndugu zako vigogo wanaweza kupewa kazi za aina nyingine. Cha muhimu ni kwamba na sisi tuone INAWEZEKANA kwa vyama kubadilishana madaraka na tusiwe na FEAR OF THE UN KNOWN. Nchi nyingi zimepitia hatua kaam hii kwa hiyo ni jambo linalowezekana
 
Sijui, Lakini my Third eye tells me That, This is a big point. hapa napo kura zitapotea.
 
Nini hatima ya wafanyakazi serikalini endapo CHADEMA itashinda??manake naona kama kuna wizara na vitengo vitafutwa kwenye serikali mpya ya chadema, nini hatima yetu au wasi wasi wangu tuu??

Kasikilize tena ajasema Ajira zitafutwa, Kasema wizara zitafutwa na kuundwa Mpya, Ila kama wewe ni MFANYAKAZI WAKUTEULIWA POLE SANA, TAFUTA AJIRA NYINGINE MAPEMA.
 
Kasikilize tena ajasema Ajira zitafutwa, Kasema wizara zitafutwa na kuundwa Mpya, Ila kama wewe ni MFANYAKAZI WAKUTEULIWA POLE SANA, TAFUTA AJIRA NYINGINE MAPEMA.

Kweli kuongeza tija na kuleta ufanisi kuna gharama zake lakini naiona redundancy kwenye ngazi za wateule pekee.
 
no sie tumeajiriwa juzi juzi tu na wizara yenyewe ipo kwenye hati hati, i love chadema and i want changes ila kila nikifikiria what will happen to my job nakuwa kwene dilemma, serious.
 
Jana kwa madhahro aliwagusia kwa kuwaambia kuwa mishahara yao itakwenda sambamba na mfumuko wa bei ili waweze mudu gharama za maisha
 
Nini hatima ya wafanyakazi serikalini endapo CHADEMA itashinda??manake naona kama kuna wizara na vitengo vitafutwa kwenye serikali mpya ya chadema, nini hatima yetu au wasi wasi wangu tuu??

Wafanyakazi wala wasiwe na wasiwasi, kama wewe ni mwajiriwa Permanent and Pensinable huwezi kupunguzwa kazi hata siku mmoja, kinachofanyika Wizara zinabadilishwa na wafanyakazi huhamishwa tu kutoka idara ingine kwenda ingine kama ilivyokuwa kwa Wizara ya Ushirika na Masoko ilipofutwa na Wizara ya Kilimo ilivyowahi vujwa ikaingina chakula na upande maji, na pia kama ilivyokuwa kwa Wizara ya Elimu ya Juu ilivyobadilishwa hakuna aliyepoteza kazi. Wanaokumbwa na Tatizo hilo huwa ni Mkatibu wakuu na Mawaziri wanaoteuliwa na wala siyo wataaalam.

 
Nini hatima ya wafanyakazi serikalini endapo CHADEMA itashinda??manake naona kama kuna wizara na vitengo vitafutwa kwenye serikali mpya ya chadema, nini hatima yetu au wasi wasi wangu tuu??

Chadema ni chama kama vyote vya Tanzania 'HAVINA MIKAKATI AU SERA"
 
Nini hatima ya wafanyakazi serikalini endapo CHADEMA itashinda??manake naona kama kuna wizara na vitengo vitafutwa kwenye serikali mpya ya chadema, nini hatima yetu au wasi wasi wangu tuu??

Acha kuwatia watu hofu bwana. Sera ya CHADEMA si kupunguza wafanyakazi bali kuondoa mlolongo wa political appointee kama vile milolongo ya Ma-Naibu Mawaziri na kadhalika na vile vile kupunguza milolongo ya Ma-Wizara amabazo nyingine zimekuwa hazina tija tena kwa Wananchi bali kuzidisha gharama za uendeshaji wa serikali siku hata siku.
Hivyo usije kushangaa kuona Wizara kama vile ya Afrika Mashsariki iki unganishwa katika kitengo cha Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa. Au Wizara ya Elimu na Wizara ya Sayansi na Elimu ya juu kuwa chini ya Wizara moja. Na hii itasadia kuwafanya ma PS ,Camissioner na Director wa Idara kule Ma Wizarani kuwa na Watendaji wa moja kwa moja (yaani Chief operation officers) kwa shughuli za kila siku. Kwa kuongeza kwa mfumo huu inakuwa ni rahisi kupima utendaji wa hawa ma aafisa mmoja mmoja badala kama hali ilivyo sasa ambapo watu wote waangalia Waziri mmoja tu.
 
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi,katiba ya chadema pamoja na Dr.slaa wamesema wanataka kupunguza uongozi wa kisiasa na kuongeza uongozi wa kiutendaji,badala ya kuwa na mawaziri 3 kwenye wizara moja ambao wengine wanaishia kufungua warsha na semina na kujibu maswali bungeni,tuwe na watendaji[professinals]kama wafanyakazi na wakuu wa vitengo na wakurugenzi ambao watawajibika moja kwa moja kama hawataweza kufikia malengo,hivyo ni faraja kwamba nafasi za kazi,vyeo na madaraka yataongezeka kwa wafanyakazi na ajira pia zitaongezeka.
 
Ni vizuri umeleta wasiwasi wako hapa. Usiwe na wasiwasi tena na kazi yako, we ifanye kwa bidii zote kabisa. Lakini kama ni post ya kisiasa kama mkuu wa wilaya, mkoa nk, hapo nakushauri utafute ajira nyingine tu.
 
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa JK na CCM yake walivikuza vitengo na idara za serikali kuwa Wizara ili kuwahonga baadhi ya wanasiasa kwa minajili ya kupata ulaji hilo sasa litakoma kwa kuzipunguza wizara lakini haimaanishi ya kuwa kuna redundancy hata kidogo.............

Watakaoathirika ni wale walio katika nafasi za juu ambao ndiyo chanzo cha mfumuko wa ubadhirifu serikalini lakini siyo watumishi wa ngazi za chini ambao wataendelea na shughuli zao bila ya bughudha hata chembe na wategemee kubana matumizi huko kutajenga mazingira ya wao kupata nyongeza ya mishahara ambayo ilikuwa inatumika kubeba zigo la kugharimia wakubwa ambao si lolote wala chochote lile kwenye uzalishaji..
 
Alisema atappoint mtu kulingana na uwezo wake , uadilifu , na uchapakazi wake akitanguliza maslahi ya umma kwanza. Viongozi wa Mashirika ya Umma kama vile NHC, PPF, NSSF, TANESCO, TANAPA , AICC na mengineyo watachaguliwa kwa vigezo vitakavyowekwa sio uswahiba. Mashirika haya yamekuwa yakiendeshwa kibabe babe na kuwanyima wananchi haki . Mfano NHC inayodeal na nyymba za kuishi.Siku hizi wamekuja na sera za kibishara wakasahau madhumuni ya kuanzishwa kwake hivyo kuwafanya wapangaji wajipinde sana na mwisho wa siku Wahindi tu ndio wanafaidi.Hii haikubaliki. Wengine wamekuwa wakitoa fedha kufadhili ccm na viongozi wake kinyume na sheria. Haya yote yatakwisha.

Nyumba bora ni pamoja na sera bora za nyumba ikiwemo nyumba za kupangisha.Sio Mwenye nyumba acharge kodi kwa dola wakati hatuna dola .
 
Kwani issue ni nini? nadhani ni woga tu. Wajua watu kukubali mabadiliko ni ngumu sana. Hata kama kutakuwa na wizara zitafutwa au la je hilo litakuwa ni jambo jipya? Mbona ktk awamu zilizotangulia kumekuwa na kuundwa, kuvunjwa/kuunganishwa etc kwa wizara!!

Nakushauri uwe positive zaidi.Lengo la kuwa na mabadiliko ya uongozi ni kuwa na undeshaji tofauti. Vinginevyo kusingekuwa na haja ya kubadili uongozi. Mambo yangekuwa yanabaki kama yalivyo.
 
Thanks a lot kwa kuelimishwa manake serikali mpya mambo mapya, sisi ni wataalam wa kawaida tu sema tupo more specialized kwenye hicho kitengo nyeti wizarani na if kitafutwa na serikali ya Slaa, huo ndio ulikuwa wasi wasi wetu. But i have understood.

VOTE FOR CHADEMA
 
Back
Top Bottom