Hatari cheti feki wanarudishwa kazini

Taarifa yako ni ya kusadikika. Hebu jaribu kuandika kwa weledi ili hata wavivu wa kufikiri kama wewe waelewe. Nikiwa kama mtumishi wa serikali napenda kukufahamisha kwamba wakati wa zoezi la vyeti feki kulikuwa na nafasi ya kukata rufaa. Waliokata rufaa na kuwasilisha utetezi walirudishwa kazini. Na zoezi bado linaendelea.
 
Kwa mtazamo wangu mtu aliyeghushi cheti na aliyeghushi taaluma ni lazima watofautishwe. Kuna tu hajasomea taaluma husika ila kachukua cheti cha mwingine na kujifanya ni mwanataalamu wa fani fulani, huyu ni mtu hatari na anastahili hata kushitakiwa.

Kuna mwalimu alifundisha kwa miaka 28 mwezi mmoja kabla ya kustaafu ikasemwa alighushi cheti. Akafukuzwa kazi na mafao yake akanyimwa.

Kesi za vifo ni nyingi sababu ya stress za jinsi ya kukabili maisha mapya,Waislamu huwa Na hekima kidogo jinsi ya kudili Na ishuu
 
Hujamwelewa. Ikiwa ni hivyo, hata hapo ulipo unaweza tendewa sivyo, hutalalamika? Utahamia shughuli nyingine kienyeji tuu? Kubwa tuheshimu haki za wengine, haya ni mapito. Kuna watu wamefanyiwa vetting mbalimbali, mabosi vihiyo wamewaangusha!
Labda sijamwelewa kweli. Nimedhani anahoji watu kurudishwa kazini ilihali wapo wenye vyeti wapo mtaani ndo Nikasema afute mawazo kuwa kuna Mtu amekalia riziki ya mwingine. Apambanie riziki yake bila kutaka wengine wapoteze kwanza.
 
Si kweli hata kama wametumia vyeti si vyao Lkn wamekaa darasani Na Huwezi ufeki utaalamu.Huwezi ufeki ualimu,udaktari,uinjinia,udereva nk cheti ni makaratasi.Nchi zilizoendelea huwa awahangaiki Na vyeti Bali output ya MTU.
Wee cheti feki nini? Sasa tutajuaje mtu anajua kama kwanza sio kupata taaluma na kutihaniwa.
 
Nadhani hujamsikiliza vizuri Mh Naibu Waziri, ni hivi katika lile zoezi,kuna watu walikata rufaa hivyo serikali ilipitia rufaa zao wakabaini kuna watu 4,160 walionewa hivyo kurudishwa kazini acha kupotosha watu ndugu jiangalie na upotoshaji wako sio mzuri sana na sijui unafanya hivi kwa lengo gani?
Kama wote hao waliondolewa kimakosa basi zoezi halikufanyika kwa umakini. Kuna mtu hapo kasema kuna watu walipoteza maisha kwa mshituko...ungesoma vizuri uzi kwanza sio kukurupuka.
 
Labda sijamwelewa kweli. Nimedhani anahoji watu kurudishwa kazini ilihali wapo wenye vyeti wapo mtaani ndo Nikasema afute mawazo kuwa kuna Mtu amekalia riziki ya mwingine. Apambanie riziki yake bila kutaka wengine wapoteze kwanza.
Mkuu, kuna watu awamu hii wanasumbua sana na wanaharibu cv za wengine waliofanya makubwa ambapo hata robo yake hawatafikia. Ukichungu,a vzr, nda hao wasio na vyeti au vyeti feki. Mfano, mtu anakutukana, unampoteza hadharani, ukiulizwa unakana. Swali, kazi ya mahakama nini? Unganisha jambo dogo kama hilo na hoja ya vyeti kiufanisi.
 
Ilitokea wengine majina yalikuwa yamefanana hivyo wakastopishwa
Lakini likafanyika zoezi la utambuzi mwenye cheti original akapeleka wizarani wakahakikiwa na kurudishwa kazin
 
1090677


NAIBU Waziri wa Nchi, O si ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa amesema watumishi 4,160 walioondolewa katika mchakato wa kuwaondoa wenye vyeti feki wamebainika kuondolewa kimakosa au kwa uonevu na wamerejeshwa kazini.

Dk Mwanjelwa aliyasema hayo bungeni jana wakati wa kujibu swali la Mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Manyinyi (CCM) na kuongeza kuwa kati ya watumishi waliorejeshwa kazini, watumishi 3,057 ni watendaji wa vijiji, mtaa na kata.

Katika swali lake, Manyinyi alisema serikali katika kuhakikisha inapata watumishi bora wenye sifa, iliamua kuwaondoa watumishi wasio na sifa pamoja na wenye vyeti feki, hivyo alitaka kujua ni kwanini serikali isiunde timu maalumu ili ipitie kila halmashauri kupitia taarifa juu ya zoezi hilo ili haki itendeke hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kwenda wizarani.

Pia alitaka kujua kama serikali haioni kuwa watumishi waliojiendeleza kielimu zaidi ya darasa la saba na wameondolewa kwa kosa la udanganyifu kuwa ni bora kuliko ambao hawajajiendeleza.

Akijibu maswali hayo, Dk Mwanjelwa alisema katika zoezi hilo watumishi 15,189 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mshahara.

Alisema baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi na vyanzo vingine kuhusu watumishi kuondolewa kimakosa au kwa uonevu katika orodha ya mishahara, serikali imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa karibu ikiwa ni pamoja na kuunda timu za ufuatiliaji wa utekelezaji wa zoezi hilo.
 
Hili jambo bado lina ukakasi, unakuta mtu darasa la saba kapitia mgambo na kuhitimu vizuri kama askari Mgambo na serkali iliwafundisha kwa nia njema, leo kwa kuwa hana cheti cha form iv amefukuzwa kazi, lakini hawa mgambo ni wa muhimu, nashauri waliokuwa mgambo wangefikriiwa kwa kurejeshwa kazini.
 
Wale waliotahiniwa halafu kazi zinawashinda inakuwaje?? Kuna watu wamemaliza Chuo Kikuu hata kuandika barua za kuombea kazi hawawezi.
Acha kujifariji. Elimu inapatikana vyuoni na kuhitimu kwa kufaulu mitihani. Kiwango kama sio bora ni tatizo tofauti ila mfumo wa vyeti kuthibitisha elimu ya mtu huwezi kuepa.
 
Back
Top Bottom