Hata nikibaki peke yangu, CCM haifi - Nape

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
Maneno hayo yamesemwa na Nape akiwa huko Bukoba. Sijui alikuwa anafurahisha nafsi au alikuwa anataka kuonyesha kuwa kwa cheo alichonacho hawezi tena kwenda South kuchukua rasimu ya Katiba for CC...!

Source: Taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu ITV
 
Kwa nini ametumia maneno "hata nikibaki peke yangu? Ina maana wameondoka wengi sana au?
 
unabii wa nape unatia mashaka.
hata kama ameonyeshwa kuwa atabaki peke yake ccm hiyo si ni nafasi ya kukisafisha chama badala ya kuridhika na kuharakisha kukiua kama anavyofanya?
 
Hawezi kubakia peke yake, huyo jamaa ni mnafiki. Amejua kuwa itafika wakati fulani CCM itabakia historia ndo maana wakaanzisha CCJ ili muda ukifika wasepe zao.
 
Anabwabwaja huyu ameshakuwa kama robot hajui hata asemalo.
 
Ninahakika kuwa ndugu Nape anajihatarishataji ushauri nasaha.
 
Maskiniii weeeeee magwanda wanamkosesha usingizi kabisa huyu kijana!pole zake.
 
Maneno hayo yamesemwa na Nape akiwa huko Bukoba. Sijui alikuwa anafurahisha nafsi au alikuwa anataka kuonyesha kuwa kwa cheo alichonacho hawezi tena kwenda South kuchukua rasimu ya Katiba for CC...!

Source: Taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu ITV
Nadhani baada ya kumtaja Nape sasa utalala.... Aaaah hahahaa magamba bwana mna tabu sana!
 
Anabwabwaja huyu ameshakuwa kama robot hajui hata asemalo.

Angalia vocha ulopewa na Dr kujadili positive mkutano wenu wa kisanii jangwani isijeisha ikaadhibiwa bure, angalia wote mnajadili Nape badala ya kujadili kwanini mmetumia 500mill na mkutano wenyewe ndo ule, wale vijana mlowanunua kuja na nguo za CCM wamekimbilia wapi?
 
Nadhani baada ya kumtaja Nape sasa utalala.... Aaaah hahahaa magamba bwana mna tabu sana!

Ona, yani watu wa ccm..hawako serious,hawawezi kuwa serious na kamwe hawataweza! Huyu na WJM jinsi wanavyopost hapa ni kichekesho,wanafanya mambo kisharobaro..! Huwez kukuta Mnyika, Makene etc wamepost pumba kama hizi utafikiri ndio wanapevuka, inasikitisha sana. chadema kaza uzi..hawa masharobaro hawana lao.
 
Angalia vocha ulopewa na Dr kujadili positive mkutano wenu wa kisanii jangwani isijeisha ikaadhibiwa bure, angalia wote mnajadili Nape badala ya kujadili kwanini mmetumia 500mill na mkutano wenyewe ndo ule, wale vijana mlowanunua kuja na nguo za CCM wamekimbilia wapi?

Too low propaganda..hivi milioni mia 5 bila kuwepo viti,maturubai kibao,kusafirisha wanachama,posho kwa wahudhuriaji etct kama mnayofanyaga ninyi inafikaje fikaje??. Usilete experience ya ki-ccm hapa..Nazidi kushangaa ilikuwaje ccm ikampa uenezi mtu kama huyu.
 
Angalia vocha ulopewa na Dr kujadili positive mkutano wenu wa kisanii jangwani isijeisha ikaadhibiwa bure, angalia wote mnajadili Nape badala ya kujadili kwanini mmetumia 500mill na mkutano wenyewe ndo ule, wale vijana mlowanunua kuja na nguo za CCM wamekimbilia wapi?

Ndio ujanja(wizi)wenu watu Wa ccm kujenga choo cha matundu manne kwa thamani ya milioni 180?
 
Maneno hayo yamesemwa na Nape akiwa huko Bukoba. Sijui alikuwa anafurahisha nafsi au alikuwa anataka kuonyesha kuwa kwa cheo alichonacho hawezi tena kwenda South kuchukua rasimu ya Katiba for CC...!

Source: Taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu ITV

Ni msimamo mzuri. Tegemeo ni kuwa ni msimamo wenye nia ya dhati.

Kwa maana nyingine ni kuwa Nape ni CCM na CCM ni Nape. Bila CCM hakuna Nape, na bila Nape hakuna CCM.

Wengine mnaweza kuona kuwa ni kama majivuno na kujitukuza, ila kama kweli Nape anaamini hivyo na kusimamia hivyo, hiyo ni haki na halali yake kabisa. Hata Mwalimu alisimamia TANU hivyo hivyo, japo kwa malengo tofauti na haya ya CCM ya sasa.
 
Jamani, ninaomba muelewe kwa makini kuwa, "Kinachomfanya Nape Nnauye Ale, Avae, Alale, ni maneno ya mdomo wake na mara nyingi maneno ambayo hata yeye mwenyewe hayaamini ila akishatumwa aseme hivyo, hana budi ya kutekeleza".

Muoneeni huruma kijana mwenzetu! Siku moja ataokoka na atajivua Gamba tu....!

Lakini kumbukeni ya kwamba, hata KANU ilipokaribia kunyang'anywa madaraka nchini Kenya, "Viongozi wao, Mpaka Dakika ya Mwisho walisema, KANU hakiwezi kuangushwa na vyama kama, PNU na Vingine". Je KANU leo hii kipo madarakani?

Bwana Muhammad Saeed al-Sahhaf, Aliyekuwa Waziri wa Habari na Msemaji wa Serikali ya Aliyekuwa Raisi wa Irak, Marehemu Saddam Hussein walipovamia na majeshi ya Kimarekani, Uingereza, na NATO, hata nusu saa kabla hajakamatwa,alipiga propaganda kuwa, "...Karibu Jeshi la Irak linashinda vita ile..." Je maneno yake yalikuwa ya kweli? Walipigwa hawajapigwa?

Jamani mfa maji, Haaachi.....!

Kaka endelea kula mshahara, endeleza propaganda wasikufukuze kazi...!
 
Back
Top Bottom