Hassan Moyo Mwasisi Muungano alipua jipu Muungano ulivyozunguka Mbuyu

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
images

Shamsha Vuai Nahodha
akila kiapo cha uwaziri Serikali ya Muungano

Moyo, Shamsi wavutana suala la Muungano

Mwanasiasa Mkongwe Zanzibar Hassan Nassor Moyo, amesema kwamba wakati mazungumzo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanafanyika, Msaidizi Mkuu wa Rais wa Kwanza Zanzibar, Salum Rashid alikuwa kwa kinyonzi akinyoa ndevu zake. Tamko hilo amelitoa wakati akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wa viongozi waliopita katika masuala ya Muungano katika semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW) huko Chukwani Zanzibar jana.

Alisema kwamba Rashid, alikuwa Katibu Mkuu (Ikulu) wakati wa uongozi wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Sheikh Abeid Amani Karume, baada ya kumuondoa katibu wake kutokana na kuhudhuria mazungumzo hayo akiwa hajanyoa ndevu zake.

Alisema Aprili 14, 1964 aliyekuwa Rais wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alimwita Rais wa Zanzibar Ikulu ya Dar es Salaam, kufungua mazungumzo ya mpango wa Muungano wa Tanganyika Zanzibar. Hata hivyo alisema baada ya Karume kufika Ikulu alimkuta msaidizi wake amewasili akiwa hajashevu ndevu na kumtaka achukue gari na kwenda kwa kinyonzi. “Baada ya kurudi kutoka kushevu ndevu kwa kinyonzi alikuta wanaendelea ndani na mazungumzo lakini kwa kuzingatia itifaki hakuweza kuingia ndani.”alisema Mzee Moyo.

Alisema kwamba Aprili 22, mwaka huo Mwalimu Nyerere alikuja Zanzibar kukamilisha mazungumzo ya Muungano lakini wasaidizi wake wa muhimu mzee Karume aliwatenga na kuwaweka katika ‘korido’ wakati waziri wake wa Nchi Ofisi ya Rais wakati huo Aboud Jumbe Mwinyi akiwa safari ya kikazi Pemba.

“Baada ya mazungumzo Karume alimwita msaidizi wake Salum Rashid na kumpatia waraka wa muungano amsomee kifungu kwa kifungu na kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ulikuwa umeandikwa kizungu kabla ya kusainiwa”. Hata hivyo alisema Mjumbe wa BLM Khamis Abdallah Ameir, alitaka kufahamu kwa nini mpango huo unafanyika harakaharaka lakini Karume alimuondoa wasiwasi na kuwaeleza wajumbe kama hawataki yupo tayari kumrejeshea makaratasi yake Nyerere lakini Wajumbe wote waliunga mkono mpango wa Zanzibar kuungana na Tanganyika.

Alisema Baraza la Wawakilishi (BLW) lina mamlaka kamili ya kukubali kuendelea kuwepo kwa Muungano au kukataa kwa sababu ni chombo cha wananchi kama Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM). Moyo alisema kwamba chimbuko kubwa la muungano huo ulitokana na hofu ya vitisho vya Zanzibar kupinduliwa iliyokuwa ikitolewa na baadhi ya viongozi kutoka Afrika Mashariki.

Moyo alisema kero za Muungano zimeanza kuibuka muda mrefu na kutoa mfano mwaka 1970 kulitokea kishindo baada ya Zanzibar kupendekeza waraka wa kutaka baadhi ya mambo kurekebishwa katika orodha ya mambo ya Muungano ikiwemo kuondoa Jeshi la Polisi.

Wajumbe waliochangia mada hiyo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, ambaye alivutana kwa muda mrefu kutaka maelezo ya kina, Hamza Hassan Juma, (Kwamtipura) Ismail Jussa ladhu, (Mji Mkongwe) Makame Mbarouk Mshimba (Kitope) Salim Abdalla Hamad, (Mtambwe) na Fatma Mbarouk, (Amani).

Hata hivyo Mzee Moyo, alishindwa kujibu maswali mazito ya Nahodha aliyetaka kujua kwa nini nafasi ya Zanzibar kiulinzi na kiusalama iwe nje ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Shamsi alisema kwamba miaka 7 baada ya Mapinduzi Zanzibar kumefanyika majaribio 14 ya kutaka kuinagusha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Semina hiyo imeandaliwa na Baraza la Wawakilishi (BLW) na kudhaminiwa na serikali ya Norway, ambapo pia elimu juu ya Katiba inatarajiwa kutolewa katika majimbo 50 ya Zanzibar.
 
je Mzee Nassor yeye aliingia kwenye mazungumzo hayo? kama hakuingia nadhani na yeye anachosema si cha kuamini sana.
kikubwa hapo ni hati ya mwanzo ya muungano inasemaje na iko wapi? hiyo inaweza tafsiriwa na watu kuupata ukweli
 
Shamsi Vuai ni mjumbe wa BLW (kwa kuchaguliwa), wakati huo huo ni mbunge kwenye bunge la muungano (kwa kuteuliwa)!
 
Hassan Moyo alikuwa mmojawapo wa viongozi wa juu serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Karume alikuwa na mfumo wa kidictata ndio maana hata katibu wake tu alitolewa nje ili wajadili na Nyerere peke yao

Wakati huo huo Karume alikuwa mbumbumbu wa kimombo, alihitaji mtu wa kumtafsiria.
 
Shamsi Vuai ni mjumbe wa BLW (kwa kuchaguliwa), wakati huo huo ni mbunge kwenye bunge la muungano (kwa kuteuliwa)!

Shamsha Vuai ana usongo na Muungano, kwani bila Muungano alishakuwa Rais wa Zanzibar, lakini Muungano hasa wajumbe toka bara walimpitisha Shein. Hilo ni moja wapo kero kubwa la Muungano ambao unawaudhi wazanzibar kuchaguliwa mgombea wao wa Rais wao na wabara.
 
Shamsi Vuai ni mjumbe wa BLW (kwa kuchaguliwa), wakati huo huo ni mbunge kwenye bunge la muungano (kwa kuteuliwa)!

Mjumbe kwa kuchagaliwa sidhani. Nakumbuka (if i may recall) kama alipigwa chini na wananchi uchaguzi uliopita.
 
Very interesting...but I have some faith on Nahodha, weather muungano utakuwepo au utaishia mitini. Wengine wamekaa kama wapiga story zaidi.
 
Mjumbe kwa kuchagaliwa sidhani. Nakumbuka (if i may recall) kama alipigwa chini na wananchi uchaguzi uliopita.

Sidhani kama Vuai alipigwa chini na wananchi wa Zanzibar, kwani alikuwa kipenzi chao sana tu.

Ukweli ni kwamba CCM ilikusudia kumpitisha Shein wa Pemba ili kuvuta watu wa Pemba wampigie kura ili kumgaragaza Maalim seif. Angepitishwa Vuai maana yake Pemba yote ingempigia kura Maalim na ungekuwa mwanguko babu kubwa wa CCM visiwani.

Ikumbukwe kwamba uteuzi wa jina la Mgombea wa Urais Visiwani hupigiwa kura na wajumbe wote wa mkutano Mkuu wa CCM bara na visiwani, wengi wa wajumbe wakiwa ni wa kutoka Bara. Nakumbuka ililalamikiwa mara kadhaa kwamba wabara ndio wanaowachagulia mgombea urais.
 
Muungano wa Tanzania, Haukuja kwa kutania,
Viongozi wake walidhamiria, kuimarisha udugu wa asilia;
Hata uamsho wakilia, na hasan nasor moyo kuwasaidia;
BLW pia likiwasaidia, hapatakua na maridhia;
Juliasi Mwalimu alituambia, na Sheikh Karume alituusia;
Tumeungana kwa nzuri nia, kutengana kutaleta udhia;
Tuuenzi Muungano wetu, Bara na Visiwani PIA.

MIMI nasema kuna KERO ZA MUUNGANO

KERO hizi za MUUNGANO zinahusu ZAnzibar na Zinahusu TaNganyika.

TUZIFANYIE KAZI KERO HIZO

SIO KUVUNJA MUUNGANO

KAMA KUNA KICHAA ANASEMA MUUNGANO UPO UPO TU; HUYO LAZIMA NI MGONJWA WA MIREMBE.

Tuna Miaka 48 ya Muungano

Marais wa Muungano Wanne

Marais wa Zanzibar Saba

Mawaziri Wakuu 12.

JAMANI
 
Vuai aligombea uwakilishi bana! nafikiri jimbo la mwanakwereke jambo ambalo limawakera wazanzibar kweli kwa kuonyesha uchu wa madaraka/waziri kiongozi hadi uwakilishi!
 
karume alikuwa sahihi kumwambia msaidizi wake akanyoe ndevu kwani hata vurugu za sasa hivi zinasababishwa na watu wasionyoa ndevu
kama msaidizi wake alipewa kazi ya kutafsiri ni wazi alikuwa na uwezo wa kutoa maoni kwa kile alichokishuhudia kwani bado mkataba ulikuwa haujasainiwa mi nawashauri wazanzibar wasizunguke sana kama hawataki muungano wajitoe kelele zote za nini
 
Utetezi wako unaweza kuwa sawa na pia una mapungufu kadhaa katika kutoa taswira ya hali ya Muungano.

Hali ya Muungano wa Tanzania ni sawa na shamba ukishalilima na kupanda miche unakaa tu na kusubiria mazao kukomaa bila kuangalia mambo mengine ambayo yanaweza kusitisha ukuaji na upatikanaji wa matunda yanayotazamiwa.

Kupalilia shamba, kung'oa magugu, na kuua wadudu au kulinda wanyama waharibufu ni mambo muhimu katika kulinda shamba lako lizalishe matunda stahiki.

Matatizo mengi yaliyotikea na yanayotokea na kuwa kero zisizovumilika kwa wakati huu ni kutokana na kasoro ambazo zimelalamikiwa miaka kadhaa na kuzikwepa kuzitatua, leo ni donda ndugu. Hii ni kutokana na funikafunika.
 
Vuai aligombea uwakilishi bana! nafikiri jimbo la mwanakwereke jambo ambalo limawakera wazanzibar kweli kwa kuonyesha uchu wa madaraka/waziri kiongozi hadi uwakilishi!

Sorry, Shamsha Vuai Nahodha alikuwa mmojawapo candidate wa Urais Visiwani Zanzibar pamoja na Makamu wa Rais wa sasa Serikali ya Muungano.

Kama unakumbuka Kule Dodoka kwenye Mkutano Mkuu wa CCM kuteua wagombea urais Zanzibar na Muungano, Shamsha Vuai alisindikizwa na Rais wa zamani wa Zanzibar Komandoo ikiwa ni nadra sana Komandoo kutua Dodoma tangu amalize muda wake wa utumishi wa urais Zanzibar.

Pata shika ilikuwa Dodoma ambapo Wazenj walizidiwa kete na wabara kwa hoja kwamba kupigia kura wagombea kulifanywa na wajumbe wote wa bara na visiwani huku wajumbe wa bara wakiwe wengi kuliko wa visiwani.

Bara walimfahamu zaidi Shein na walifanya kila kinachowezekana kumpisha huyu kwani wagombea wengine walionekana kuwa hawako karibu zaidi na bara na pengine wanaweza kuibua yanayoshindiliwa na serikali ya Muungano kuhusu matatizo ya Muungano. Shein alionekana atakuwa tayari kulipa fadhila kwa kuwa msikivu na mtulivu kuliko akina Vuai.
 
karume alikuwa sahihi kumwambia msaidizi wake akanyoe ndevu kwani hata vurugu za sasa hivi zinasababishwa na watu wasionyoa ndevu
kama msaidizi wake alipewa kazi ya kutafsiri ni wazi alikuwa na uwezo wa kutoa maoni kwa kile alichokishuhudia kwani bado mkataba ulikuwa haujasainiwa mi nawashauri wazanzibar wasizunguke sana kama hawataki muungano wajitoe kelele zote za nini

Tatizo la wasio na elimu mara nyingi katika kuongoza hutumia zaidi mamla kuliko argument. Karume alikuwa na mfumo wa kiutawala wa kiimla na wa kisultani. Muungano ulikuwa niridhaa yake na Nyerere kwa kuahidiwa kuwa anatakuwa Makamu wa Rais akiwa na nguvu za kisiasa hadi bara ikamfanya Karume aingie kichwa kichwa.
 
Hakuna hata moja lisiloweza kutatulika na lililofikia hadi kusema uvunjike.

Hilo halipo

na huo kamwe sio utetezi wangu, ni mtazamo

juliasi

na abedi

lazima tuwaenzi

utetezi wako unaweza kuwa sawa na pia una mapungufu kadhaa katika kutoa taswira ya hali ya muungano.

Hali ya muungano wa tanzania ni sawa na shamba ukishalilima na kupanda miche unakaa tu na kusubiria mazao kukomaa bila kuangalia mambo mengine ambayo yanaweza kusitisha ukuaji na upatikanaji wa matunda yanayotazamiwa.

Kupalilia shamba, kung'oa magugu, na kuua wadudu au kulinda wanyama waharibufu ni mambo muhimu katika kulinda shamba lako lizalishe matunda stahiki.

Matatizo mengi yaliyotikea na yanayotokea na kuwa kero zisizovumilika kwa wakati huu ni kutokana na kasoro ambazo zimelalamikiwa miaka kadhaa na kuzikwepa kuzitatua, leo ni donda ndugu. Hii ni kutokana na funikafunika.
 
Hakuna hata moja lisiloweza kutatulika na lililofikia hadi kusema uvunjike.

Hilo halipo

na huo kamwe sio utetezi wangu, ni mtazamo

juliasi

na abedi

lazima tuwaenzi

Ni kweli hakuna lisilowezekana kutatulika, lakini je tunapokwepa kuzitatua kero hizo za Muungano tusingefikia kiwango cha leo. Tatizo ni kukwepa matatizo na kuyafunikafunika kusubiria watakaofuata ndio watakaoyatatua na ndio mbio za kupokezana vijiti kila anayefuata nakwepa kutatu hadi kufikia uozo wa donda ndugu kutovumilika.

Karume na Nyerere historia itawaenzi, lakini si kigezo cha kuacha kutatua matatizo na kurekebisha kasoro zake.
 
karume alikuwa sahihi kumwambia msaidizi wake akanyoe ndevu kwani hata vurugu za sasa hivi zinasababishwa na watu wasionyoa ndevu
kama msaidizi wake alipewa kazi ya kutafsiri ni wazi alikuwa na uwezo wa kutoa maoni kwa kile alichokishuhudia kwani bado mkataba ulikuwa haujasainiwa mi nawashauri wazanzibar wasizunguke sana kama hawataki muungano wajitoe kelele zote za nini

Kichekeso kisicho cha kawaida kumtoa mtu kikaoni kwa ajili ya kunyoa ndevu wakati kikao kinaendelea, dalili tosha ya kukosekana ustaarabu na kuendesha mambo kisultani. Kwa nin hawakumsubiri arudi baada ya kunyoa ndevu ndopo kkao kiendelee? Maana yake ilikuwa mbinu ya kumwondoa asijue nini kinaendelea katika mazungumzo yao na Nyerere.
 
If the truth be told wenye CCM are not passionate about the union they are passionate about protecting the status quo, that is bound to be severely shaken should the union break-up. CCM wili loose relevance or put more poignatly nnje ya muungano hamna CCM ipo TANU na ASP at best. If wenye CCM were Pan Africanist at heart how do you explain their dogged resistance to establishment of EA federation?
 
If the truth be told wenye CCM are not passionate about the union they are passionate about protecting the status quo, that is bound to be severely shaken should union break. CCM wili loose relevance or put more poignatly nnje ya muungano hamna CCM ipo TANU na ASP at best. If wenye CCM were Pan Africanist at heart how do you explain their dogged resistance to establishment of EA federation?

Una point nzuri. Kuanzishwa kwa CCM ilikuwa ni njia ya kuzika ASP na TANU ili kuziba zaidi matatizo yaliyokuwa yanajitokeza katika utendaji wa serikali ya vyama tofauti kutoka nchi zilizoungana. Tatizo lililobadilika ni kuwa na bendera moja ya chama cha siasa wakati Zanzibar ingali ni ASP. Maana ya Muungano ilikuwa kufanya taifa moja, lakini kwa namna moja au nyingine waliodhoofisha zaidi Muungano ni wazanzibar ambao wanataka haki kimataifa.
 
images

shamsha vuai nahodha
akila kiapo cha uwaziri serikali ya muungano

moyo, shamsi wavutana suala la muungano

mwanasiasa mkongwe zanzibar hassan nassor moyo, amesema kwamba wakati mazungumzo ya muungano wa tanganyika na zanzibar yanafanyika, msaidizi mkuu wa rais wa kwanza zanzibar, salum rashid alikuwa kwa kinyonzi akinyoa ndevu zake. Tamko hilo amelitoa wakati akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wa viongozi waliopita katika masuala ya muungano katika semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi (blw) huko chukwani zanzibar jana.

alisema kwamba rashid, alikuwa katibu mkuu (ikulu) wakati wa uongozi wa rais wa kwanza wa zanzibar, hayati sheikh abeid amani karume, baada ya kumuondoa katibu wake kutokana na kuhudhuria mazungumzo hayo akiwa hajanyoa ndevu zake.

alisema aprili 14, 1964 aliyekuwa rais wa tanganyika mwalimu julius kambarage nyerere, alimwita rais wa zanzibar ikulu ya dar es salaam, kufungua mazungumzo ya mpango wa muungano wa tanganyika zanzibar. Hata hivyo alisema baada ya karume kufika ikulu alimkuta msaidizi wake amewasili akiwa hajashevu ndevu na kumtaka achukue gari na kwenda kwa kinyonzi. "baada ya kurudi kutoka kushevu ndevu kwa kinyonzi alikuta wanaendelea ndani na mazungumzo lakini kwa kuzingatia itifaki hakuweza kuingia ndani."alisema mzee moyo.

alisema kwamba aprili 22, mwaka huo mwalimu nyerere alikuja zanzibar kukamilisha mazungumzo ya muungano lakini wasaidizi wake wa muhimu mzee karume aliwatenga na kuwaweka katika ‘korido' wakati waziri wake wa nchi ofisi ya rais wakati huo aboud jumbe mwinyi akiwa safari ya kikazi pemba.

"baada ya mazungumzo karume alimwita msaidizi wake salum rashid na kumpatia waraka wa muungano amsomee kifungu kwa kifungu na kutafsiri kwa lugha ya kiswahili kwa sababu ulikuwa umeandikwa kizungu kabla ya kusainiwa". Hata hivyo alisema mjumbe wa blm khamis abdallah ameir, alitaka kufahamu kwa nini mpango huo unafanyika harakaharaka lakini karume alimuondoa wasiwasi na kuwaeleza wajumbe kama hawataki yupo tayari kumrejeshea makaratasi yake nyerere lakini wajumbe wote waliunga mkono mpango wa zanzibar kuungana na tanganyika.

alisema baraza la wawakilishi (blw) lina mamlaka kamili ya kukubali kuendelea kuwepo kwa muungano au kukataa kwa sababu ni chombo cha wananchi kama baraza la mapinduzi zanzibar (blm). Moyo alisema kwamba chimbuko kubwa la muungano huo ulitokana na hofu ya vitisho vya zanzibar kupinduliwa iliyokuwa ikitolewa na baadhi ya viongozi kutoka afrika mashariki.

moyo alisema kero za muungano zimeanza kuibuka muda mrefu na kutoa mfano mwaka 1970 kulitokea kishindo baada ya zanzibar kupendekeza waraka wa kutaka baadhi ya mambo kurekebishwa katika orodha ya mambo ya muungano ikiwemo kuondoa jeshi la polisi.

wajumbe waliochangia mada hiyo ni waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, shamsi vuai nahodha, ambaye alivutana kwa muda mrefu kutaka maelezo ya kina, hamza hassan juma, (kwamtipura) ismail jussa ladhu, (mji mkongwe) makame mbarouk mshimba (kitope) salim abdalla hamad, (mtambwe) na fatma mbarouk, (amani).

hata hivyo mzee moyo, alishindwa kujibu maswali mazito ya nahodha aliyetaka kujua kwa nini nafasi ya zanzibar kiulinzi na kiusalama iwe nje ya muungano wa tanganyika na zanzibar. Shamsi alisema kwamba miaka 7 baada ya mapinduzi zanzibar kumefanyika majaribio 14 ya kutaka kuinagusha serikali ya mapinduzi ya zanzibar. Semina hiyo imeandaliwa na baraza la wawakilishi (blw) na kudhaminiwa na serikali ya norway, ambapo pia elimu juu ya katiba inatarajiwa kutolewa katika majimbo 50 ya zanzibar.

hapa nadhani watu wanahasira ya juzi kupigwa waislam wenzao. Nchimbi anatumia vibaya madaraka yake
 
Back
Top Bottom