Nadhani tunakubaliana kuwa serikali ya JK ni dhaifu. Hata wakubwa wa CCM na serikali wanakubaliana na hili. Udhaifu wa aina hii unarudisha nchi nyuma na kiongozi ajaye atapata shida sana kusahihisha makosa. Kuna nyufa zimejengwa na kiongozi huyu dhaifu. Swali ni je, udhaifu huu unatokana na nini? Je, ni sifa gani anapaswa kuwa nazo kiongozi ajaye? Je, ni nani anafaa kuwa rais ajaye bila kujali chama? Sioni kama chama kitatufikisha mahali, nadhani tunapaswa kuwa na mtu anayeweza kuongoza bila kujali chama chake. Hebu tuzungumze bila ushabiki, mfumuko wa bei kwa mfano unatuathiri wote, hivyo ushabiki hautusaidii tuitetee nchi