Harakati za Maaskofu kujisafisha na kujitenga na 'mabaya ya Magufuli' hazitawasaidia. Waombe radhi na wao

Kipindi cha Nyerere kilikuwa zama nyingine kabisa. Mengi aliyofanya Nyerere yalikubalika na kuendana na harakati za kipindi hicho. Afadhali Nyerere mara kumi, nchi nyingine za kiafrika zilikuwa na marais wabaya na wauaji. Wapinzani walikuwa wanaua kama wanyamana marais walijilimbikizia madaraka na mali kwa faida yao. Kufananisha enzi za Nyerere na Magufuli ni kama unafananisha maji na mafuta.
Uko sawa mkuu
 
Mbona mnajihami sana na waraka wa maaskofu?
Nani amewaambia wataandaa nyaraka?
Au mna magumu mnayapanga kwao ama kwa wafuasi wao hivyo mnajihami mapema?
Acheni hizo,ongozeni watanzania kwa haki na hamtasikia kelele kutoka kokote
 
Si vyema sana kumsema mtumishi wa Mungu na hata mtu mwingine kwa mambo ya hisia hisia tu. Kama ulivyosema una uhakika, basi ni kweli inapaswa uwe nao uhakika, ama ikiwa ni vinginevyo, basi hiyo ni kujitakia dhambi kwa kushuhudia uongo kwamba unao uhakika
Si mpaka wawe watumishi Sasa. Wengine ni matapeli tu wamejificha kwenye utumishi Wa Mungu
 
KWa sisi ambao tulikuwa tunaifuatilia JF wakat wa JK, haya yanayosemwa yan ukweli kiasi. Nitafafanua kama ifuatavyo:
1. Ni kweli kwamba anapochaguliwa rais wa dini/kabila/kanda fulani basi watu wanaoendana na dini/kabila/kanda hiyo hunufaika na mfumo. Mfano, wakat wa JPM, Kanisa Katoliki (na mengine) yalifunga macho na kufaidi mema ya nchi huku wakitetea vitu vingi vilivyopaswa kupingwa. Wasukuma pia walikula maisha, hasa ktk teuzi. Nadhani JPM alitaka watu watakaokuwa upande wake bila kujali makunyanzi. Mfano mwingine ni wakat wa JK, waislam na taasisi zake walikuwa ndo watetez wakuu wa JK-hasa baada ya kupwaya kwa serikali kufuatia kuondolewa kwa Lowassa! Pia harakati za waislamu zilifikia kiwango cha juu sana-Mahakama ya Kadhi na maandamano kuelekea NECTA.

2. Hivyo hii ni tabia yetu, bila kujali dini/kabila au ukanda. Watendaji wanaojipendekeza kwa Mkuu huhakikisha wanapakua nyama nyingi kwa walio karibu na mkuu. Inatokea kwa ridhaa ya rais au hata bila ridhaa yake.

3. Ktk awamu hii ya Mama Samia, jipe miaka 2-3 uone vitimbi vya makanisa pale maslahi yao yatakapoguswa. Pia tegemea harakati za waislam kuongezeka, hasa Shekhe Ponda na wenzake utawaona ulingoni. Cha msingi hapa, Waislam na Wakristo wasichukiane, wajue tu ni upepo unapita wakat taasisi za dini zao zinapigania maslahi. Tuungane wote kupinga ubaguzi na chuki dhidi ya dini nyingine. Mimi nipo nawasubiri wakristo wenzangu wakileta kidomodomo dhidi ya Mama Samia, bila sababu za msingi.
 
Ebana, wewe ni MCHAWI??.

Watanzania kwa mamilioni wamemlilia Magu walikuwa hawaoni huoubaya unao usema.
Watu mataifa mbalimbali wamesema wazi alikuwa ni kiongozi wa kupigiwa mfano kwa uongizi wakizalendo.

Umoja wa mataifa wame mtambua na kuadhimisha siku rasmi.
Rais wetu Mama Samiya amesema amepata wakatimzuri wakujifunza kuchapakazi kupitia hayati Magufuli.

Mashehe, Maaskofu, Wachungaji nk.nk.
Wanaheshimu mchangowake kwa taifa na kumuombea kwa Mungu apumzike kwaamani.
Wewe unajaribu kumchafua, nakuuliza tena hivi wewe ni MCHAWI???.

Hujui kwamba sauti ya wengi ni sauti ya mungu WEWE Ni MCHAWI????.
Acha ujinga
 
Mkuu, haters wa Magufuli hawakubali siku iishe bila kumtaja. Ndiyo sababu kila mara huja na vibandiko vya kijinga jinga hapa ilimradi tu wamtaje Hayati roho zao zisuuzike. Siwalaumu, jamaa ni gwiji. No wonder ataishi vichwani mwao "milele".

Kama huyu aliyeleta mada. Ukijiuliza ni kwa namna gani hao maaaskofu au watu wa dini wanataka kujitenga na awamu ya Gwiji unashindwa kuelewa. Nyumbu wanahangaika na mzimu wa JPM kuliko hata sie wafuasi wake.
He was a dictator full stop
 
Kwanini unazungumzia kanisa pekee huku ukiacha Vyuo, wasomi, vyama vya wafanyakazi ??

Na kwanini huzungumzii BAKWATA ???

Ni nani alisimama kukemea wakati hayo madhambi yote yakifanyika ??

Na kwanini unalazimisha Maaskofu ndio wasimamame, wasipokemea unaumia???
images (21).jpeg

Hawa ndio aina ya wasomi nchi iliwapata awamu ya 5
 
Mbona mnajihami sana na waraka wa maaskofu?
Nani amewaambia wataandaa nyaraka?
Au mna magumu mnayapanga kwao ama kwa wafuasi wao hivyo mnajihami mapema?
Acheni hizo,ongozeni watanzania kwa haki na hamtasikia kelele kutoka kokote
Kwa kuwa hatutaki unafiki tena
 
Ni washenzi tuu hao watu wenu mnaowaita viongozi wa dini wakati ni waganga njaa

Ila nimecheka yaani Nyerere ndio alifanya maamuzi ya ajabu hayo? Aisee ni shida kumbe ndiko mwendazake alikoiga staili
 
Nilikutana na mwalimu wangu fulani wa seminari ambaye sasa ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki fulani, tuliongea mengi mno kuhusu Magufuli administration na akaniambia wengi walikua kwenye Payroll ya JIWE na aliwapa maposho mazito kuliko wabunge ili wanyamaze.

Wapo waliokataa kutokuuza utu wao na wengi walikubali na kukaa kimya.

Magufuli aliendesha nchi kama vile Mussolini wa Fascism aisee.

Naandaa uzi nauweka kibindoni kusubiri wale maaskofu kama watanyanyuka tena kwa Samia au wataendelea kunyamaa.
Duu kweli Kazi ilikuwepo ,sijui Limagu lilikuwa linawaza nn, afadhari Mungu katusikia maana huyo jamaa duu
 
Hujaelewa nini hapo?
Mleta mada anasema kabla ya uhuru kanisa lilikuwa bega kwa bega na mkoloni likimpinga Nyerere. Baada ya uhuru, kanisa likawa bega kwa bega na Nyerere dhidi ya watu huru.

Hitimisho lake ni kuwa;
Kanisa=Mtawala=Unafiki
Mleta mada amechamganya uwongo na ukweli. Siyo kweli kuwa kanisa lilimpinga Mwalimu katika harakati zake za kutafuta uhuru. Bali kanisa lilimsaidia sana Mwalimu Nyerere katika harakati zake.

1) Air ticket ya mwalimu na gharama zake zote za kwenda UN zilichangiwa na Mzee Mbowe, Rupia na sehemu kubwa ilitolewa na Kanisa Katoliki.

2) Mwalimu Nyerere alipoambiwa achague moja, kazi ya uwalimu au TANU, aliingiwa na kigugumizi, achague nini, akijua kuwa akiacha uwalimu atashindwa kuihudumia familia yake. Kanisa Katoliki ndiyo lilimpa nguvu ya kuchagua uongozi wa TANU maana waliamua kuichukua familia yake na kuihudumia. Familia ya Mwalimu ikaenda kuishi Tosamaganga, kwa wamisonari Wakonsolata (waitaliano).
 
Wanaojua history ya nchi hii wanajua jinsi
Wakoloni walivyotumia makanisa kueneza ukoloni na kudhibiti harakati zozote zile za wazalendo kutafuta Uhuru...

Hata Nyerere hakupewa sapoti yeyote na makanisa zaidi ya kupigwa vita..
But baada ya Uhuru walifanikiwa mno
Kubadili historia ..wakafuta history Yao mbaya ..na ndo maana tukawa na history ambayo ina matobo matobo..
Haileti majibu hata sasa ukiuliza..

Wakati wa Nyerere pia kanisa lilikuwa bega na bega Nyerere ..
Nyerere alifuta vyombo vya habari binafsi
Nyerere alifuta demokrasia ya vyama vingi
Nyerere akapiga marufuku kukosolewa wala kuulizwa ..
Baadhi ya maamuzi ya Nyerere ya ajabu Hadi Leo hakuna anaeweza kujibu
Mfano kuunga mkono waasi wa Nigeria
Against OAU na nchi zote za Africa..

Na lile la kungo'a reli iliyokuwa inakwenda mikoa ya kusini....

Kanisa kipindi chote hakuna tamko wala waraka wa kukemea chochote zaidi
Ya kuja kuanza mchakato wa kumfanya awe 'mwenye heri' baada ya Nyerere kufa..

Wakati wa Magufuli kanisa limerudia Tu
Exactly walichofanya Kwa Nyerere..
'Blind support ' ya asilimia Mia moja
Na kuhakikisha hakuna resistance ya chochote hata kama katiba inavunjwa
Au harakati za kuibadilisha ili atawale milele...

Blind support wakati Tundu Lissu anapigwa risasi
Blind support wakati watu wasiojulikana wana terrorize watu ..
Watu wanatekwa...n.k..
Only kuja kuamka wakati wa Cororna when its too late . ..

Sasa harakati za kujisafisha na kujitenga na mabaya ya utawala wa awamu ya tano
Zimeanza...
Binafsi naona wakiwa honest wanatakiwa kuomba radhi hadharani kabla ya kujipa
Nafasi ya kumkosoa na kumpa matamko na nyaraka Rais Samia....nna uhakika watafanya hivyo...
Kati ya viongozi wa kwanza katika Nchi hii kuchochea machafuko watakuwa ni viongozi wa Kanisa maana ni wanafiki kupita kiasi maana kila anapotawala Rais muislamu matamko ya kila Jpili hayapungui na tutaona kila aina za nyaraka(Waraka)

Lakini akitawala Rais mkristo wapo kimyaaa kama hawapo hata kama Rais huyo ni dikteta na fisadi sasa kipindi hichi cha Mama tunaomba wakae kimya kama wanavyokaa kimyaa Bakwata kipindi anapotawala Rais si Muislamu

Hali hii Kanisa wakiiendeleza si tu inakera kwa wale wasio waislamu ila ikiendelea kuachwa itasababisha chuki kali za kidini na kusababisha uvunjifu wa amani
 
Nilikutana na mwalimu wangu fulani wa seminari ambaye sasa ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki fulani, tuliongea mengi mno kuhusu Magufuli administration na akaniambia wengi walikua kwenye Payroll ya JIWE na aliwapa maposho mazito kuliko wabunge ili wanyamaze.

Wapo waliokataa kutokuuza utu wao na wengi walikubali na kukaa kimya.

Magufuli aliendesha nchi kama vile Mussolini wa Fascism aisee.

Naandaa uzi nauweka kibindoni kusubiri wale maaskofu kama watanyanyuka tena kwa Samia au wataendelea kunyamaa.

Mkuu hao maaskofu tunawasubiri kwa hamu wakifungua mdomo ndio watatujua. Viongozi wa dini kadhaa waliojitenga na udhalimu tunawafahamu Askofu Bagonza, Sheikh Ponda, Askofu Mwamakula, askofu Shoo na Askofu Niwemugizi. Hawa walijitenga wazi wazi na dhalimu. Hao wengine waendelee kukaa kimya.
 
Back
Top Bottom