HAPANA KWA mpango maalum wa afya ya msingi

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Kwa muda mrefu sasa wadau na wanazuoni mbalimbali wamekua wakipinga mpango uliozaa shule za kata.serikali kwa upande wake imekuwa ikisifia mpango huu lakini imeumbuka baada ya matokeo ya kidato cha nne 2010 kuonyesha ni asilimia 11 tu ya wanafunzi ndio wenye sifa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano au vyuo vya ufundi na ualimu.wengi wa waliofeli wametoka kwenye shule za KATA.
Kwa upande mwingine serikali inaendelea na maandalizi au iko kwenye hatua za mwanzo za utekelezaji wa MPANGO MAALUM WA AFYA YA MSINGI(MMAM).inavyoelekea hapa tutakua na kituo cha afya au dispensary kila KATA.
Kwa maoni yangu huu ni uzumbukuku mwingine ambao madhara yake tutayaona baada ya miaka 5.sioni haja ya kuwa na dispensary kila kata wakati hospitali za mikoa hazina dawa,vifaa na wataalamu wa kutosha.kazi zinazofanywa na watu wa afya ni wito,mpango huu utasababisha mtu yoyote mwenye wito na asiye na wito,wajinga na werevu kujiunga na fani ya afya.hapa ndipo tunapotangaza maafa ya kizazi chetu. Serikali ijifunze kwenye elimu na iachane na mpango huu wa 'kisiasa' badala yake iboreshe hospitali zilizoko ikianza na muhimbili national hospital.
Watanzania,wanajf tuungane kuukataa mpango wa afya ya msingi kwani hautakua na tija.

NAWASILISHA...
 
Back
Top Bottom