Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 75
Ni mke mwema aliyetulia na kutekeleza vema majukumu yake ya ndoa. Tatizo lake anaposafiri kwenda nyumbani hawezi kupiga simu wala kutuma message mpaka atafutwe. Licha ya kulalamikiwa mara kadhaa ameshindwa kubadilika na kuna wakati alisema "mimi nakuwa na uhakika uko salalama". Yuko nyumbani kwa sasa na jana asubuhi alipata taarifa za mume kuugua lakini mpaka sasa hivi hajapiga simu kuulizia hali ya mume inaendeleaje. Nini kifanyike?