Hana mikono/miguu lakini anaendesha gari........

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Hii ni video maalumu kwa wale wote walioanza kuweka vimaneno vya kishamba humu ndani.

Sintawataja ila wanajijuwa na wanafahamu kabisa hayo maneno wameyaandika wapi.

Wamekuja na vijiswali vya kujifanya wanafahamu sana kumbe hawajui kitu.

Haya sasa, angaalieni hii video na tusikie mtasema nini....... Anaitwa Barbara Guerra.



Ukisiliza 1:40, inasemwa wazi kabisa kuwa, gari halina modifiication yoyote kwa ajili ya Vilema (Disabled).


Mwingine huyu hapa, now what????
 
Last edited by a moderator:
Hujaeleweka Mkuu wangu. Hivi neno, Kilema/Vilema lina ubaya? Au ulimaanisha kuweka herufi kubwa?

Fanya ed. ya ile nomino inayoanza na vi-, tafadhali. Last but one para
 
Sikonge,

bila kuficha hisia video ya huyo dada imenitoa machozi, ama kweli hujafa hujaumbika

Sikonge;3140863]Hii ni video maalumu kwa wale wote walioanza kuweka vimaneno vya kishamba humu ndani.

Sintawataja ila wanajijuwa na wanafahamu kabisa hayo maneno wameyaandika wapi.

Wamekuja na vijiswali vya kujifanya wanafahamu sana kumbe hawajui kitu.

Haya sasa, angaalieni hii video na tusikie mtasema nini....... Anaitwa Barbara Guerra.



Ukisiliza 1:40, inasemwa wazi kabisa kuwa, gari halina modifiication yoyote kwa ajili ya Vilema (Disabled).


Mwingine huyu hapa, now what????
[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
Kwani sheria za udereva zinasemaje kuhusu walemavu?
 
RAL,

Nafikiri ni kumshukuru Mungu kwa kumpa huyu dada uwezo wa kufanya mambo kwa kutumia miguu na si mikono.

Ndiyo maana wanasema binadamu ana SIX SENSE ila hiyo ya sita huwa imejificha sana. Mtu ikibidi kuitumia, basi unaweza kuiamsha na ukaanza kuitumia. Ndiyo maana watu wanasema ukikutana na Steve Wonder mara kadhaa, atakukariri hatua zako na unapokuja tu kwake, atakuita jina.

Wa-Asia hasa wacheza Martial Arts, huwa wanaziamsha hizi hisia na anaweza kupigana na wewe hata kama amefumba macho. Pia wanaweza kujua kama kuna fujo, mtu gani ni hatari na yupi si hatari. Steven Segal amekuwa mtu anayewafundisha Polisi wenzake jinsi ya kung'amua vitu kama hivyo.

Nafikiri inabidi kuwatia moyo hata vilema wengine kuwa akiwa kilema si mwisho wa dunia. Anaweza kufanya kila kitu na hata kuwazidi walio wazima. Kuna yule Profesa nimemsahau, anayeongea kwa kutumia misuli ya uso. Jamaa ni mkali mno na heshima juu kama Msomi na uprofesa wake wa darasani.

Kuna dada mwingine nilimsoma, yupo Sweden na yeye anafanya kila kitu kwa miguu tu. Ila yeye ilikuwa ni makosa ya dawa za kuzuia mimba zilizotengenezwa miaka ya 60 na kampuni ya German. Akina mama wote waliotumia hizo dawa na baadaye kuacha ili washike mimba, wengi walizaa watoto vilema.

kilema kibaya na ambacho mtu inabidi ulie ni KILEMA CHA AKILI.
 
Back
Top Bottom