Hamad Chande: Serikali inaandaa Mkakati wa kuwezesha Benki za Wajasiriamali wadogo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 37 leo Mei 31, 2023.



Kuanzishwa kwa Benki ya Vijana ya wajasiriamali
Serikali imesema ipo kwenye hatua ya kuandaa mkakati wa upatikanaji wa mikopo kupitia benki na taasisi ndogo za kifedha itakayotolewa baada ya kuanzishwa kwa taasisi mahsusi itakayosimamia utoaji wa mikopo hiyo kwa kuzingatia makundi maalum ikiwemo vijana.

Makundi mengine ni wanawake, watu wenye ulemavu na wafanyabiashara wadogo ikiwemo Machinga.

Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Hamad H. Chande wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Lucy John Sabu aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanzisha benki ya vijana wajasiriamali.
 
Back
Top Bottom