Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,743
Katika vitu tulivyofail Africa ni kujiongoza wenyewe, kila unaemuamini anaharibu tu, kuna ka shida huku.
MKUU, kwani shida ni ndogo - ni kubwa sana mkuu! Sasa sijui tatizo ni kutojiamini, mindset, kupenda penda matanuzi na vyeo - inasikitisha sana!
Jaribu kuwasikiliza mikakati yao ya kufufua viwanda sijui kujenga vipya, wanaonekana hawana strategy yoyote viwanda vipi vipewe kipaumbele kwanza - hii in hatari sana, ukiwasikiliza sana unakuwa na wasi wasi kama kuna litakalo tekelezwa kwa ufanisi - majigambo yamezidi mno hata Marshal plan ya kuijenga upya Ulaya baada ya vita vya pili haikuwa hivi - Dk.Magufuli awe makini sana hasa hasa kwa wale ambao wanaonekana wana majibu on their fingertips kuhusu ifufuaji wa viwanda vyetu - utasikia mengi mengine ambayo ni too good to be true which's TRUE, kaeni na Wachina ,WavietNam na Wathailand wasikilizeni walitumia strategy gani katika masuala ya viwanda vidogo na vikubwa.