Halima Mdee amtaka Rais Magufuli ataje posho na marupurupu anayolipwa

dadoliz

Member
Jul 27, 2015
59
40
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee. Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.

Chanzo: Mtembezi
 
“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee.
Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.
“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,”alisema Mdee.
Mbunge wa Jimbo la Ndanda katika Wilaya ya Masasi, Cecil Mwambe alidai katika mkutano huo kuwa wananchi wa Mtama wamekosa mwakilishi wa kuwasemea matatizo yao, hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na mbunge wao, Nape Nnauye kukosa uwezo wa kusimama bungeni kuisema Serikali.
“Mtama mmekosa mwakilishi, hapa kuna tatizo la korosho na mbunge aliyepo anashindwa kulisemea, hivyo mtabaki hivyo hivyo bila kutatua tatizo lenu kwa kipindi cha miaka mitano,” alidai Mwambe.

Source: MPEKUZI |Tanzania Entertainment News,Politics News ,Celebrity Gossip and Live Updates
Mbunge wa mkanyageni anawapiga kura 3000 na kaya zisizozidi 150 nae anavuta millioni kumi! achilia mkopo wa gari jimbo analoweza kulizungukia kwa miguu akalimaliza kwa siku moja.
 
Napata wasiwasi pale magufuli aliposema yeye binafsi,makamu wa rais na waziri mkuu watakuwa wanachangia sh 6 milioni kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya elimu kwa mkoa wa dar es salaam.sasa kama analipwa 9.5 milioni pekee si rahisi kuchangia 6 milioni.labda kama ana marupurupu mengi zaidi.dah....ama kweli CCM ni ile ile.
 
Napata wasiwasi pale magufuli aliposema yeye binafsi,makamu wa rais na waziri mkuu watakuwa wanachangia sh 6 milioni kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya elimu kwa mkoa wa dar es salaam...
Unapata faida gani kupotosha ukweli. Ni wapi Magufuli alisema maneno hayo? Ukiitwa mpumbavu unaanza kupiga mayowe oh wananionea. Nyumbu wewe.
 
Huyu Halima keshaanza kuchanganyikiwa, si aende kwa mwenyekiti wa kamati ya Budget amwonyeshe randama ya Budget ya Ikulu, kama mbunge anauliza mshahara wa mtumishi wa umma basi kunatatizo kubwa huko bungeni.
 
Napata wasiwasi pale magufuli aliposema yeye binafsi,makamu wa rais na waziri mkuu watakuwa wanachangia sh 6 milioni kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya elimu kwa mkoa wa dar es salaam.sasa kama analipwa 9.5 milioni pekee si rahisi kuchangia 6 milioni.labda kama ana marupurupu mengi zaidi.dah....ama kweli ccm ni ile ile.
Kwani 9+ - 6 inabaki ngapi?
 
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee. Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.

Chanzo: Mtembezi
Halima atuambie mshahara wa mwenyekiti wake kwanza
 
Duuuh.... Mdee kavurugwa. Lakini ndio sahihi hivyo kama mtumishi mkuu wa uma yeye na wenzake tunahitaji kujua mapato yao wanayolipwa na serikali na ndio transparency hiyo tunayoitaka...
 
Back
Top Bottom