Hakuna umuhimu wa ndoa karne hii kwa sababu hizi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
HAKUNA UMUHIMU WA NDOA KARNE HII KWA SABABU...

Na, Robert Ng'apos Heriel

Hakuna umuhimu wa ndoa katika Karne hii Kwa sababu;

1. THAMANI YA MWANAMKE IMESHUKA NA INAKARIBIA KUTOWEKA
Unapozungumzia Ndoa unamzungumzia Mwanamke, kadiri mwanamke anavyokuwa na thamani ndivyo thamani ya ndoa nayo inakuwa na thamani. Mwanamke yupo Kama Mratibu Mkuu wa Ndoa. Kushuka Kwa hadhi ya wanawake Duniani kunatokana na wao KUJIRAHISISHA. Kadiri mwanamke anavyopewa Uhuru ndivyo thamani yake inazidi kuporomoka, ni hakika itatoweka kabisa. Lengo la sheria za kubinya Uhuru wa mwanamke tangu zamani ni kulinda thamani yake. Uhuru uliopitiliza wa wanawake utazidi kushusha utu wa mwanamke.

2. KUPOROMOKA KWA BIASHARA YA UMALAYA

Kuporomoka kwa biashara ya umalaya kutokana na wanawake wengi kugawa uchi kiholela Umalaya na ndoa ni mambo yanayoenda sambamba. Ndoa ikiwa na thamani basi na umalaya utakuwa na thamani. Katika tafiti zangu za kiuchunguzi, Bei ya kununua Malaya miaka ya 2011 ilikuwa juu ukilinganisha na Mwaka 2020. Malaya alikuwa akinunulia miaka hiyo 10,000 -20,000 Kwa Bao moja Maeneo ya kawaida Kama Sinza Mori, Ambiance n.k. lakini kutokana na wanawake wengi kujirahisi na kugawa penzi kiholela hali inayopelekea umuhimu wa ndoa kutokuonekana, hii imefanya biashara ya Umalaya kuanguka, Kwa sasa unaweza pata Malaya Kwa bei ya 2000 -8000. Mke wa ndoa Kwa sasa Hana ubavu wa kumbabaisha mume wake kwani akimnyima tendo, basi huko barabarani na mitandaoni wanawake Buku wanamsubiri Wampe penzi.

Hata hivyo umalaya siku hizi unafanywa hata na Wake za watu Hali inayowakatisha tamaa WAOAJI. Umalaya unapofanywa na wanawake wengi unafanya soko kudondoka na bei kushuka chini. Kama wanawake wangekuwa na AKILI basi Jambo la Kwanza kabisa kulipigania lilikuwa ni THAMANI zao, kupitia kudhibiti ongezeko la Umalaya. Hii ingeongeza thamani mara elfu kuliko kupiganka vitu visivyo na maana yoyote katika utu wao. Udhibiti wa Msamiati KUDANGA ungedhibitiwa, na hao wapigania HAKI SAWA. Maneno ya namna hii sio tuu hayafurahishi bali pia yanawadhalilisha wanawake pasipo ya wao kujua wenyewe.

Ongezeko la Umalaya limefanya tendo la ndoa kupoteza uthamani, kupata tendo la ndoa kwa sasa sio HABARI kama ilivyokuwa zamani ambapo ilikuwa mshike mkamate kukubaliwa na mwanamke.

3. KUZAA SIKU HIZI SIO MPAKA NDOA
Siku hizi hakuna tofauti kubwa baina ya Mtu na Mnyama. Moja ya mambo yaliyomtofautisha binadamu na mnyama ni pamoja na ndoa, ili uweze kupata watoto basi ilikubidi Ufunge Ndoa, yaani Uoe au Uolewe. Bila kuoa au kuolewa ilikuwa ngumu kupata mtoto.

Thamani ya ndoa pia ilijengwa kwenye kupata watoto, Binadamu wengi asilimia 99% huwa na ndoto siku moja wawe na watoto na kwa zamani mahali pekee pakupata watoto ni ndani ya ndoa. Hii iliipa thamani taasisi ya ndoa.

Lakini zama hizi, kupata watoto sio sababu tena ya kuingia ndani ya ndoa. Mtu anaweza akawa na watoto bila hata ya ndoa. Tena anaweza akawa na watoto na wanawake hata kumi, au wanaume wengi pasipokuoa au kuolewa nao.

Zamani ukimpa mwanamke mimba hesabu umeshamuoa, lakini sio siku hizi.

Kama serikali na taasisi za dini zingekuwa zinataka ziondoe tatizo la watoto wasiolelewa na wazazi wawili lingeboresha sheria za ndoa na uzazi. Haya mambo ya Single mother yasingekuwepo. Ingekuwa sheria kuwa ni marufuku kuwa na mtoto pasipokuwa ndani ya ndoa ingawaje ingeleta athari kubwa kijamii lakini ingesaidia sana hapo baadaye.

Vijana wa sasa wengi wao huwapachika mimba wasichana kisha huwatelekeza na kuishi kibachela, wanajua wanawatoto tayari sasa ndoa ya nini ikiwa mahitaji yote ya ndoa wanayapata hata wakiwa hawajaoa.

Kwanza kuishi ndani ya ndoa katika zama hizi inachukuliwa kama mateso makubwa kuliko unafuu.

4. SHERIA YA PASU KWA PASU
Karne hii vijana wengi hawataki kusikia habari za ndoa kutokana na aidha uelewa mdogo kuhusu sheria za pasu kwa pasu, au kuzijua sheria hizo kupitiliza. Niliwahi kumsikia rafiki yangu ambaye kimsingi amefanikiwa kwa umri wake, ana nyumba mbili, gari moja pamoja na vimiradi midogo midogo akiwa na umri mdogo tuu wa miaka 33. Rafiki yangu huyu nilimuuliza kwa nini asioe kwani umri wa kuoa anao, na anauwezo wa kumudu mahitaji ya kifamilia alichonijibu kilinishangaza. Alinijibu hivi; Nina watoto wawili kwa nini nioe, unataka nioe alafu nigawane mali na mwanamke siku tutakapoachana?"

Nilimuuliza kwa nini anafikiri kuachana zaidi kuliko kuishi mpaka kifo, akaniambia nisijifanye sioni wanawake wa zama hizi.

Vijana wengi wanafikiri habari ya Pasu kwa Pasu, sheria hii inawaumiza kila wakiifikiria linapokuja suala la kuoa, hata hivyo hawaoni sababu ya kuoa ikiwa tayari wameshapata kila kitu kilichopo ndani ya ndoa.

Vitu vilivyopo ndani ya ndoa ambavyo kwa karne hii vinapatikana hata mitaani
i. Tendo la ndoa
ii. Watoto
iii. Kazi za nyumbani kama Kufua, kupika, vyombo, usafi n.k
iv. Ushauri na kusaidizana

Vitu ambavyo vipo nje ya ndoa lakini ndani ya ndoa havipo

i. Uhuru
Ndani ya ndoa hakuna uhuru kwani wewe ni mali ya mtu, nje ya ndoa wewe sio mali ya mtu unafanya utakavyo, urudi usirudi nyumbani yote sawa, ulale usilale na mwanamke yote sawa.

ii. Hakuna sheria inayokulazimisha kumhudumia yeyote yule kwani sio mke wako lakini ndani ya ndoa zipo sheria zinazokulazimisha kumhudumia mke wako

iii. Tahadhari
Nje ya ndoa kuna tahadhari kwa sababu unawachukulia wanawake wote utakaodate nao ni Malaya, hivyo utaogopa Maradhi, pia utakuwa makini na pesa unazotoa.

Ndani ya ndoa hakunaga tahadhari kubwa kwa maana unaamini huyo ni mkeo, na ni rahisi kupata UKIMWI ndani ya ndoa kuliko nje ya ndoa.

Ni ngumu kwa mtu ambaye hajaoa na hana mpango kujiua kisa mapenzi ila ni rahisi kwa mtu aliyeoa au mwenye matarajio ya kuoa kujiua kisa mapenzi

Wanawake ni lazima walazimishe ndoa kwa sababu thamani na utu wao unalindwa zaidi akiwa ndani ya ndoa kuliko akiwa nje.
Sasa Ongezeko la wanawake wasiotaka ndoa kutokana na sababu mbalimbali zinazidi kuondoa utu wa mwanamke.

Hata hivyo wapo wanawake ambao bado wanazijua thamani zao, ingawaje thamani zao zipo mashakani kutokana na kundi kubwa la wanawake kuamua kujipa uhuru unaowavua nguo wanawake wote duniani.

Wanawake wasafi na waaminifu wapo, namaanisha wasiopenda kutembea na wanaume hovyo kama wanyama, lakini wanajikuta katika wakati mgumu pale anapotaka kumnyima Mwenza wake mpaka ndoa ilhali anajua kabisa akimnyima basi wapo wenzake kama mia wanamsubiria huyo mchumba wake, hivyo wanaamua kutoa uroda na kujikuta wakiwa kundi moja la wale wasiosafi na wasiowaaminifu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Mbona leo andiko lako fupiiii sanaaaa jamani!? Anyways, umuhimu wa ndoa kamwe haujawahi kupungua, hauwezi kupungua na hautakuja upungue. Tunza uzi wako huu, sawa? :) Takwimu!? Takwimu zinaonesha kwamba kwa sasa asilimia 70 hadi 83 (70-83%) ya vijana na watu wazima wenye umri wa kuoa na kuolewa hadi umri wa kati na utu uzima wanathamini sana ndoa kuliko wakati mwingine wowote.
 
Mbona leo andiko lako fupiiii sanaaaa jamani!??? Anyways, umuhimu wa ndoa kamwe haujawahi kupungua, hauwezi kupungua na hautakuja upungue. Tunza uzi wako huu, sawa!??? :) Takwimu!??? Takwimu zinaonesha kwamba kwa sasa asilimia 70 hadi 83 (70-83%) ya vijana na watu wazima wenye umri wa kuoa na kuolewa hadi umri wa kati na utu uzima wanathamini sana ndoa kuliko wakati mwingine wowote.

Just watch, then you will see
 
Heriel umeongea mambo ya msingi sana.

Kwa bahati mbaya msingi wa familia ni ndoa na msingi wa jamii ni familia. Kwa hiyo ndoa zinapokuwa vurumai, familia zinakuwa vurumai na hatimaye jamii kuwa vurumai tu. Kwa bahati mbaya zaidi sioni ni kwa namna gani jamii inaweza kurudi kwenye mstari.
 
Hili jambo wazungu walishaliona mapema ndo maaana wakawa na ndoa za mikataba. Baada ya kuoana, kutifuana na kuchokana, kama mliweka mkataba wa miaka miwili ikiisha unachukua mtoto/mrembo mwengine laini kabisa

Na huku bongo kwa namna hali ilivyo ni heri tukawa na ndoa za mkataba.
 
hili jambo wazungu walishaliona mapema ndo maaana wakawa na ndoa za mikataba. Baada ya kuoana, kutifuana na kuchokana, kama mliweka mkataba wa miaka miwili ikiisha unachukua mtoto/mrembo mwengine laini kabisa

Na huku bongo kwa namna hali ilivyo ni heri tukawa na ndoa za mkataba.

Haswaaa!! Tunaelekea huku
 
Heriel umeongea mambo ya msingi sana.

Kwa bahati mbaya msingi wa familia ni ndoa na msingi wa jamii ni familia. Kwa hiyo ndoa zinapokuwa vurumai, familia zinakuwa vurumai na hatimaye jamii kuwa vurumai tu. Kwa bahati mbaya zaidi sioni ni kwa namna gani jamii inaweza kurudi kwenye mstari.

Tushaharibikiwa Kwa sehemu kubwa, namna Bora ni serikali kuweka mifumo imara na sheria Kali kurejesha maadili
 
Back
Top Bottom