Hakuna mwenye kumiliki UFAHAMU

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,323
Nimewajibika kuwaandikia enyi mjuao kiswahili, ya kwamba si mtu, kundi la watu, taasisi binafsi au za serikali, nchi, wala bara lolote linalomiliki "UFAHAMU" niwakumbushe, wanasayansi wa awali, kwa UFAHAMU wao walikubaliana kusema umbo la dunia ni kama meza kubwa, wakatengeneza na sheri kuwa ni marufuku kusema au hufundisha vinginevyo, kanuni za adhabu kwa kosa hilo ikawa ni kunyongwa ikithibitishwa umehubiri kinyume na "UFAHAMU" ule. Kwa wajuao, akatokea miongoni mwao kupata UFAHAMU tofauti ya kuwa dunia haiko kama meza, bali dunia ni duara, jopo la wanasayansi walipothibitisha mwenzao amepingana na UFAHAMU wao walimnyonga, hatimaye walikuja kubaliana na ufahamu wa marehemu kuwa dunia ina umbo la duara, yapimeni maelezo haya myaweke kwenye mizania ya mchungaji msataafu wa Loliondo. Mwenye hoja aweke jamvini.
 
Umenena ndg.nami nimekuwa na wasiwasi kuhusu dira ya hii sayari yetu. Kile tulichozoea kikiita magharibi mimi naita mashariki na mashariki naiita magharibi na hata hivyo dunia yote kwangu ni magharibi na au mashariki.
Sitaki swali ukizingatia hoja hii kwamba hakuna binadamu mwenje kuumiliki ufahamu.
.
 
Unataka kusema kuwa babu wa Loliondo ame kwenda kinyume na ufahamu wa wana sayansi?
 
Unataka kusema kuwa babu wa Loliondo ame kwenda kinyume na ufahamu wa wana sayansi?
Babu kawaambia dawa yake hajaigundulia maabara, wanasayansi/serikali wanaitafutia vigezo vya maabara, wangeangalia matokeo ya tiba. Siyo inatibu kwa mchanganyiko wa chemical compound, yale yale ya dunia kama mezaa!!!!
 
Back
Top Bottom