Joyce joyce
JF-Expert Member
- May 23, 2020
- 457
- 1,973
Baada ya juzi Tundu Lissu kuibua sakata la wamachinga kuuziwa vitambulisho na kulaani kitendo hicho, Jana Rais Magufuli amelitolea ufafanuzi na kusema kuwa sio kweli na kutoa maagizo kwa wakuu wa wilaya nchi nzima kuwa ni marufuku wamachinga kuuziwa vitambulisho hivyo, Magufuli amesema kuwa hilo suala ni hiari na sio lazima.
Wakuu, hiii ndio maaana watanzania wanampenda Lissu, hakuna mtu anaeweza kumpinga Lissu kwani anachozungumza hata Magufuli mwenyewe anakikubali muda huo huo.
Hivi Kama watu wameteswa na kuumizwa Juu ya hili kwa kipindi chote cha miaka minne iweje Leo aje Lissu ndio itolewe amri? Ina maana Lissu angekuwepo Tanzania suala hili kumbe halingesumbua wamachinga, sasa wale wanaompinga Lissu wanatoa wapi nguvu ya kumpinga Lissu?