Hakuna Mtanzania atakayedai risiti kwa bei hizi, hata wewe ungeweza?

INSIDER MAN

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
1,748
15,929
Serikali inabidi ikae chini na kulijadili suala la ulipaji kodi kwa kina zaidi maana kama TRA wamefeli kwa upande wao.

Unakwenda dukani Kariakoo wengi ndo tunanunua bidhaa zetu kule mfano unanunua fridge au Smart tv muuzaji atakwambia bei ni TZS 870,000 bila risiti ni 820,000 unafikiri mtanzania atachagua nini kati ya hizo bei 2??.

Mimi binafsi nitakimbilia 820,000 hapo nasave 50,000 napata na pesa ya uber. Hakuna mtanzania ambaye atakubali kulipa VAT kwa ugumu huu wa maisha unafikiri hiyo 50k ni kubwa sana kwa mtu kuifanyia matumizi. Hakuna atakayedai risiti na ukiona mtu kapewa risiti jua kalipia pesa yote katika watu 1000 utapata mmoja au watatu.

Kwanini wafanyabiashara wanafanya hivo??

Wengi wao wanalalamika na utitiri wa kodi hapa nchini bidhaa ikishafika bandarin inakatwa makodi kibao mpaka VAT, sasa bidhaa hiyohiyo tena ikiingia sokoni inakatwa kodi mpaka VAT japokua wanasema VAT analipa mnunuzi wa mwisho (final consumer) hii sikweli.

Unakuta maduka yameongozana na wote tunafanya biashara ya aina moja Electronics au Home appliances mimi nimesajiliwa na VAT wengine hawajasajiliwa wote tunauza fridge ya aina moja mimi mwenye VAT natakiwa kuongeza thamani (Add value) ya bei kwa ajili ya VAT kama bei elekez ya soko ni 800,000 itabidi niongeze let say 50,000 kwa ajili ya VAT. Kwa mwenzangu ambaye hana VAT atauza dridge hiyo kwa 800,000 hana hasara.

Wateja wanatabia ya kuzunguka maduka tofauti mwisho wa siku atanunua kwenye unafuu sasa akikuta mimi nauza 850k afu akaenda kwa jirani yangu anauza 800k unategemea mimi nitauza?? Ndomana unakuta hapo mteja anapewa bei 2 maana siwez kukataa mteja hapohapo natakiwa nilipe kodi ya mapato bado VAT bado Pesa za wahasibu( consultation fees za kila mwezi na mwaka) bado nilipe kodi ya pango.

Kodi haziwezi kulipwa kama hakuna “fairness” kama VAT tusajiliwe wote maana ukifuatilia kwa ambao hawasajiliwa utagundua wamehonga, au wanawatu wao serikalini au ni biashara za wakubwa hawaguswi.

Narudia hakuna mtanzania ambaye tuko tayari kulipa VAT na kudai risiti, je hata wewe mwana JF kati ya 800k na 850k utachagua ipi??

31.12.2022
 
Kwa hali ilivyo ni kama TRA nao wanachangia sana hii Nchi kuwa maskini wakati huo huo kukwamisha mwananchi wa kawaida kukuza biashara yake, hakuna namna ikaundwa tume fulani huru ya Wachumi wakasaidia kusuka hichi chombo (TRA)? Inaonekana wao wameshindwa kabisa, maana malalamiko kila kona.
 
Upo sahihi ndugu yangu wengi wanapeleka bahasha hawasajiliwi na VAT serikali ikae chini na wataalamu maana hali itakua mbaya zaidi kariakoo ishakua black market
 
Serikali inabidi ikae chini na kulijadili suala la ulipaji kodi kwa kina zaidi maana kama TRA wamefeli kwa upande wao.

Unakwenda dukani Kariakoo wengi ndo tunanunua bidhaa zetu kule mfano unanunua fridge au Smart tv muuzaji atakwambia bei ni TZS 870,000 bila risiti ni 820,000 unafikiri mtanzania atachagua nini kati ya hizo bei 2??.

Mimi binafsi nitakimbilia 820,000 hapo nasave 50,000 napata na pesa ya uber. Hakuna mtanzania ambaye atakubali kulipa VAT kwa ugumu huu wa maisha unafikiri hiyo 50k ni kubwa sana kwa mtu kuifanyia matumizi. Hakuna atakayedai risiti na ukiona mtu kapewa risiti jua kalipia pesa yote katika watu 1000 utapata mmoja au watatu.

Kwanini wafanyabiashara wanafanya hivo??

Wengi wao wanalalamika na utitiri wa kodi hapa nchini bidhaa ikishafika bandarin inakatwa makodi kibao mpaka VAT, sasa bidhaa hiyohiyo tena ikiingia sokoni inakatwa kodi mpaka VAT japokua wanasema VAT analipa mnunuzi wa mwisho (final consumer) hii sikweli.

Unakuta maduka yameongozana na wote tunafanya biashara ya aina moja Electronics au Home appliances mimi nimesajiliwa na VAT wengine hawajasajiliwa wote tunauza fridge ya aina moja mimi mwenye VAT natakiwa kuongeza thamani (Add value) ya bei kwa ajili ya VAT kama bei elekez ya soko ni 800,000 itabidi niongeze let say 50,000 kwa ajili ya VAT. Kwa mwenzangu ambaye hana VAT atauza dridge hiyo kwa 800,000 hana hasara.

Wateja wanatabia ya kuzunguka maduka tofauti mwisho wa siku atanunua kwenye unafuu sasa akikuta mimi nauza 850k afu akaenda kwa jirani yangu anauza 800k unategemea mimi nitauza?? Ndomana unakuta hapo mteja anapewa bei 2 maana siwez kukataa mteja hapohapo natakiwa nilipe kodi ya mapato bado VAT bado Pesa za wahasibu( consultation fees za kila mwezi na mwaka) bado nilipe kodi ya pango.

Kodi haziwezi kulipwa kama hakuna “fairness” kama VAT tusajiliwe wote maana ukifuatilia kwa ambao hawasajiliwa utagundua wamehonga, au wanawatu wao serikalini au ni biashara za wakubwa hawaguswi.

Narudia hakuna mtanzania ambaye tuko tayari kulipa VAT na kudai risiti, je hata wewe mwana JF kati ya 800k na 850k utachagua ipi??

31.12.2022
Nani mwingine anaesemaga nipe risiti ya kutembelea 😀
 
Sio kila Mtanzania ni kama wewe. Na si kila mfanyabiashara ni kama hao uliozoea kudeal nao.
Kuna member humu alinunua gari showroom akaonesha hadi efd receipt ya 16m+
Kwa taarifa yako hata uchukue usichukue risiti faida ya mfanyabiashara iko pale pale unaiibia serikali tu
 
Mkuu,Issue sio faida ya Mfanyabiashara,Issue ni mteja kukwepa kulipa 18% ya VAT ambayo ukija ukijumlisha na 30% income TAX na 10% tozo za miamala halafu ukaongeza sijui na import duty,petroleum levy na vikodi vingine unakuta mfanyakazi analipa kodi 85% ya mapato ghafi yake.Tukubali au tukatae kuna tatizo katika mfumo wa kikodi wa nchi yetu na ndio maana ulipaji wa kodi uko chini na walipaji ni wachache na hao wachache wanaolipa kila siku wanatafuta namna bora ya kukwepa kodi.

Bado kwa wale ambao wanataka kulipa kodi process ya kulipa kodi ni very cumbersom iliyogubikwa na ukiritimba,rushwa na kero ndogondogo na kupotezeana muda
 
Mkuu tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa. Unaponunua TV 1.5m dukani hapo mfanyabiashara kashaweka vyote hivyo ulivyoorodhesha na faida yake. Wewe kupunguziwa 50,000 ili usichukue risiti unaiibia serikali tu.
NB; Nakubali kuna changamoto kwenye mfumo wa kodi zetu.
 
Back
Top Bottom