Hakuna hukumu baada ya maisha ya hapa duniani kwa sababu hizi

NAAMINI MUNGU YUPO KUFA KUPO KUFUFULIWA KUPO KIYAMA KIPO MOTO UPO NA PEPO IPO huyu mtoa mada anafikir kwa upeo wake tu Mungu anasema hivi nimewaumbeni hivi hivi tu nisiwape mtihan ss sijui hayo anayatoa wapi ni kama yy kawa msemaji wa Mungu mtu mwenye akili timamu hawez kukubaliana na ww ndio mana walikuwepo manabii na mitume kutupa habar za Mungu na ndio tunafuata hayo mafundisho ss ww mwenzetu hayo umeyatoa wapi
Nakuunga mkono mkuu.....kufa kupo..qiyyama kipo..hukumu IPO..moto au pepo vyote vipo na tutafufuliwa mbele ya mungu na kuulizwa tuliyokuwa tukifanya duniani.
 
Elimu zote huishia kukiri Mungu yupo!, tunachokijua ni kuwa huyu Mungu huwaza yaliyo mema kwa mwanadamu ndiyo maana atahukumu na kutoa adhabu ya dhambi na mdhambi kisha kumrehemu mwenye haki. Endelea kutenda mema Mungu atahukumu waovu wote.
 
Mkuu ZNM hivi uwepo wa Mungu umeutambua kupitia nini?? Kama ni vitabu vya dini, iweje utambue uwepo wake kupitia vitabu hivyo na uache kuamini siku ya mwisho na moto kama ilivyo kwenye vitabu hivyo??
 
Hayo ni mawazo na mafundisho ya Buddha, kila mtu yupo huru kutumia akili zake kufikiri sio kila unaloambiwa unaliamini chukua muda wako kutafakari kwa undani.. chanzo cha dini kuu 2 ni Mashariki ya kati na kutoka hapo na Africa ni karibu sana hasa nchi ya Misri ambapo hata yesu aliwahi kukimbiziwa huko na wazazi wake kwa hofu ya mfalume Herode..lakin dini imeletwa na wazungu na waarabu..
All Countries in Middle East
Bahrain
Cyprus
Egypt
Iran
Iraq
Israel
Jordan
Kuwait
Lebanon
Oman
Qatar
Saudi Arabia
Syria
Turkey
United Arab Emirates
Yemen
C vibaya ukazijua nchi hiz maana hujui km nchi za kiarabu zimo ktk middle East. Ila ujuulize kwanin Ukristo umeletwa na Wazung wakat nchi za kizung hazim ktk middle East countries
 
Mkuu Shemtibuko, Unajua chanzo cha kutofautiana imani baina ya wanadamu?
Maana yake mapokeo hayo si sahihi na hayana uthibitisho wa kutosha kwa pande zote na ili ubaki aidha kwa moja ya pokeo ni lazima utiwe hofu!
Haya yote nina elimu nayo na hii yote nilifanya udadisi kwa undani kwa kila pokeo!
Nimetumia jina Mungu as a popular name kila mmoja aelewe ila ukweli huyo nimkusudiaye hutajwa kwa majina mengi kutegemea jamii tofautitofauti! Elimu pekee itakufanya uwe mdadisi kwa mambo yenye utata duniani kama suala la dini!
 
uwezo wa mwanadamu kutenda mema ama mauvu uko nje ya uwezo wake binafsi bali unajengwa na mazingira ya wakati wake ktk kipindi anazaliwa, kukua na malezi!
 
Inaillayih-w-wainnalilah-r-rajiun sishangai kumbe matatizo yote tunayapata kwa kutoamini uwepo wa Muumba wetu na kutoamini kuwepo siku ya mwisho/siku ya malipo.

[HASHTAG]#sihitaji[/HASHTAG] swali wala mjadala katika hili.ila nimetoa kwa maoni yangu na mawazo yangu kwa imani niliyonayo
 
Kuna kiumbe aliyechagua kuzaliwa mahala fulani na nani? hapana, vp ukizaliwa na kulelewa katika mazingira ambayo ni hatarishi kwa mapokeo ya dini hizi lakini katika jamii uliyokulia mambo ni shwari? wewe nawe uhukumiwe? vipi iwapo matendo yako yanatokana na ulemavu wa ubongo na know la ukihubiriwa huelewi, nawe uhukumiwe?
acheni kutishana, pendaneni na muelekezane kwa upendo!
 
Laaana zitolewazo na watu wanyonge mfano mabibi na mababu wanapotendewa uonevu huzitoa kwa mustakabari wa dini gani?
 
Ndefu mpaka inaboa ila nimesoma paragraph 3 nanimeshaelewa anazungumzia nini ila minapita tuu
 
Unaonekana kumaanisha kuwa mambo yanayotokea hapa duniani ni maumbile tu hakuna kuhusika kwa Mungu. Elewa pia kuwa shetani yupo na unaweza ukajikuta mikononi mwake hata kama ni kwa bahati mbaya kama vile swala anavyoliwa na simba.
jambo lolote unapolihofia unalijenga /kuliumba na kulitukuza! watu wengi kwa kutokujua mmemuumba kiumbe shetani na kuanza kumtukuza! kwangu kiumbe shetani hakuna!
 
Ndugu wana JF,

Leo naomba kuwasilisha sababu ambazo kimsingi zinazihirisha kuwa hakuna hukumu baada ya Maisha ya hapa Duniani inayomhusisha Mwenyezi Mungu!

Kwanza, kila unaloliona kwa macho ama lile usiloliona kwa macho ila lina matokeo flani katika maisha ya viumbe vyote duniani halikutokea kwa bahati mbaya ama kuna kiumbe kinahusika kuliunda. Muundaji wa vyote hivyo ni Mungu (Super Natural Power) na hakuna jambo anajutia katika yote aliyoyafanya.

Mungu aliumba majabali mengi sana tena yenye kustaajabisha ila akaona moja ya majabali hayo aweke mazingira ya viumbe hai kuweza kuishi, yaani inasadikika kuwa Dunia ndilo jabali lililowekewa mazingira ili viumbe wengi waweze kuishi na hii ni sehemu tu ya Mungu kuendeleza uwezo wake ulivyo mkuu!

Hakuna kiumbe ambacho yeye Mungu anakihofia na hata kufikia hatua ya kuvihukumu baada ya maisha ya hapa Duniani. Mungu huyu hakuweka viumbe katika matabaka kama tunavyojionea leo, matabaka haya hayahusiani kabisa na Mungu na wala kwake si tatizo, yote ni katika kuendeleza ukuu wake wa ajabu.

Mungu alijua kabla na si kwa bahati mbaya kuwa, umbo la Dunia haliongezeki kadri viumbe hai vinapoongezeka, na ili ukuu wake uendelee sawasawa na matakwa yake, aliweka ukomo wa uhai kwa viumbe vyote. Yaani hauna kiumbe ambacho kina uwezo wa kuishi milele katika Dunia hii, ni lazima viumbe hawa wawe na ukomo wa uhai wao ili kupisha viumbe wengine kuendelea kuzaliwa na kuishi.

Ili kutimiza adhima hiyo, Mungu aliweka mazingira ambayo ni lazima yatokee pindi hitaji hilo linapohitajika. Mfano, iwapo viumbe wakazaliana na kuwa wengi sana katika eneo moja na kufanya eneo hilo kuwa na upungufu wa chakula, basi aliamua yajitokeze mazingira ya viumbe kuwa na tamaa na kujipenda wenyewe kuliko wengine ili wapiganie chakula kwa ajili ya uhai wao. mapigano hayo huitwa vita! hivyo, vita si jambo la kumhudhunisha Mungu bali ni moja na mambo aliyoyaweka ili kuilinganisha Dunia na Viumbe vyake.

Kwamba, iwapo viumbe hai wataongezeka kuzidi rasilimali walizitumiazo katika kulinda uhai wao, basi Mungu ameweka mazingira ambayo adhima yake ni lazima itimie mfano, uharibifu wa mazingira na misitu inaweza kuwa na matokeo ya baa la njaa, mafuriko, Tsunami, Matetemeko ya ardhi na kadhalika!

Kwamba, ongezeko kubwa la viumbe hai hawa, litawafanya waweze kuhama hama kutoka eneo moja kuelekea eneo jingine kutafuta maisha ili kulinda uhai wao, katika safari hizi za kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kunaweza kutokea ajali, mapigano ambayo yote haya yapo ili kutimiza adhima kuu ya Mungu kuwa ni lazima viumbe hivi vikome uhai wake pindi mazingira yanapohitajika kukamilisha adhima hiyo!

Jambo lolote linapotokea, Kwa Mungu halitokei kwa Bahati mbaya, huyo ndio ukuu wake na hakuna wa kuuzuia! Mipango ya Mungu ilivyotimilifu haiwezi kuepushwa na viumbe hawa hata kama wakatambua na kuanza kujipa tahadhali ili kuepuka mambo haya! Kujipa tahadhali ni sawa na kusogeza mbele deni unalodaiwa ila dawa ya deni ni kulipa!

Tunaweza kuelimishana sana ili tuweze kuzingatia taratibu za kuhifadhi mazingira ila iwapo ongezeko la viumbe hawa likizidi idadi ya rasilimali za dunia hii, ni lazima kutokea mazingira ya viumbe kutoelewa elimu itolewayo ili kutokee sintofahamu baina yao na hatimaye uharibifu utokee ili kumfanya wakala wa ukomo wa uhai kufanya kazi!

Nasema tena hivi, haya yote hakuna jambo ambalo linatokea kwa bahati mbaya mbele ya Mungu na hakuna jambo lolote linalomfedhehesha Mungu, yote haya yapo kutimiza adhima yake kuwa Duniani si mahali pa viumbe hai kuwepo milele!

Hivi, mnajua kuwa, baadhi ya matatizo tuliyonayo viumbe hai yanatokana na mazingira tuliyozaliwa na kulelewa wakati wa kukua kwetu? Mfano, ukizaliwa eneo lenye ukosefu madini ya chuma katika ardhi yake japo kidogo, utazaliwa ukiwa na matatizo ya mifupa katika umbile lako, aidha pia unaweza kabisha kuwa mlemavu wa viungo vyako vya mwili kwa urahisi!

Ukizaliwa katika eneo ambalo lina hali ya hewa yenye gesi hatarishi kwa afya yako, yapo matatizo mengi yasababishwayo na mazingira hayo, mfano, ulemavu wa viungo moja kwa moja ama ulemavu katika ubongo! Viumbe vyenye ulemavu katika ubongo, havikuamua viwe hivyo bali mazingira ndiyo yaliyopelekea viumbe hivyo kuwa hivyo vilivyo.

Mungu, hatohukumu kwa kuwa anajua, wewe na viumbe vyote ni mali yake, Dunia na rasilimali zake zote ni mali yake, kwa vyovyote hakuna kiumbe Mungu anakihofia kuwa kina mamlaka ya kupokonya idadi flani ya viumbe vyake! Mungu hahitaji viumbe hawa wahubiriwe, ama wapewe elimu juu ya ukuu wake maana hakuna jambo lolote linaweza kuepukika katika dhana ya kuhakikisha Duniani si mahali pa viumbe hai kuishi milele!

Inatajwa kuwa, moja ya amri zilizowekwa na Mungu ni Kutosema uongo na mambo kadha wa kadha kulingana na imani tuzipokeazo, jiulize kuwa, kuna jamii zinasadikika kuwa uongo ni sehemu ya maisha yao na hakuna kiumbe kilichagua kuzaliwa katika jamii hizo, inawezekanaje kwa jamii hiyo kujiepusha na uongo ilihali tatizo lao ni mazingira yaliyowafanya kuona uongo ni sehemu ya maisha yao?

Naweza kueleza mengi lakini kwa leo, niishie hapo na niseme tu kuwa, viumbe hai tunayo mazingira yaliyotengenezwa na Mungu ili tuhukumiane sisi kwa sisi mahali tunapoona kuna viumbe wenzetu wanakwenda kinyume na namna tunahitaji tulio wengi katika kuishi kwa amani na furaha! Hukumu tunayo wenyewe na na ipo hapahapa Duniani tukingali na uhai wetu!

Tafakari kabla ya ku-comment uzi huu!
Tunajua kuna biblia na korani hiki kitabu chako kinaitwaje? Naona nikusaidie "IBILISIA" litakuwa jina zuri na utauza sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom