Hakuna haja ya kusumbuka na Rais Magufuli, Hakuandaliwa huyo

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,225
3,290
Wengine tulipata tabu sana katika siku za mwanzo za utawala wa Mh rais wetu. Tulitumia muda mwingi kujaribu kumpa muda ili tujiridhishe mwelekeo wake lakini kadiri siku zilivyosonga alizidi kutupoteza.

Nilipata shida zaidi nilipomsikia akilalamikia kazi ngumu ya uraisi hata mwaka mmoja wa urais haujaisha na nilistuka zaidi na kile mwenyewe alichosema "kusukumiziwa urais" baada ya kujaribu.

MAAMUZI TATA
Mh rais alifanya maamuzi mengi tata yakiwemo kufuta baadhi ya vikorombezo vya sherehe za muungano mwaka 2016 kwa kile kilichoitwa kupunguza gharama na fedha kuelekezwa kwenye ujenzi wa barabara, kuondolewa Bunge kutangazwa live kwa sababu za kupunguza gharama n.k.


Kulifanywa tena maamuzi tata ya kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa hadi 2020. Baadhi ya haya yalifanywa katika mazingira yenye utata kwa sabababu wachambuzi walikosoa kupingana na Katiba na sheria lakini yalifanywa. Hakuishia hapo alianza kutumbuwa na kuagiza kushughulikiwa wenye vyeti feki lakini zoezi likapotea katika mazingira ya utatata hadi leo, sababu kuu ni upendeleo wa wahusika wa vyeti feki kwani kuna baadhi ya maeneo ingekuwa shida na hadi leo hatujasikia tena nini kinaendelea.

Kuna maamuzi tata ya kujengwa uwanja wa ndege wa chato unaolalamikiwa kutofuatwa taratibu za kibajeti.

KAMATAKAMATA YA WAKOSOAJI.

Kulizuka na bado kunaendelea kamatakamata ya kila anayempinga mh rais, na ubaya wake mh rais hajifichi kwa kauli zake husema hadharani na wasaidizi wake bila ajizi wanachukuwa hatua ingawa wakati mwingi hukosekana mashiko ya kisheria pale watuhumiwa wanapopelekwa mahakamani. Huu umekuwa ni mwendelezo kwa kila anayempinga Mh rais hasa wapinzani.

LUGHA ZA KUUDHI
Katika hali ambayo isingetarajiwa ni kiongozi mkuu wa nchi kutoa lugha ambazo hazifai nyingi zikidhalilisha watu na kuwagawa. Lugha za kulala nao mbele, wapumbavu, fyoko fyoko , kuwashwa washwa nk. ni mifano tu.

KUTUMIKA NGUVU NYINGI KUNYAMAZISHA.
Kumezuka tabia ya kutaka kunyamazisha sauti na maoni ya watu. Vyombo vya habari havukubaki salama pale vilipotoa taarifa zinazokinzana na watawala. Vimeonywa na kuchukuliwa hatua za kufungiwa badala ya kushtakiwa ili koneshwa makosa yao mahakamani. Tabia ya kufungia vyombo si sahihi ziko njia za haki za kunyamazisha pale ambapo mtuhumiwa angepatikana na kosa mahakamani. Hili halifanyiki.


NINI KINASABABISHA HAYA ?
Yako majibu mengi yakiwemo uoga wa baada ya kile kilichotokea 2015 kwenye uchaguzi, lakini yanachagizwa na KUTOANDALIWA au kutojiandaa rais Magufuli kwa nafasi hii na ndipo wengine huita mambo haya USHAMBA. Amekiri kuombewa duwa, amekiri kusukumizwa uraisi, amekiri kazi ngumu yote haya kwa maoni yangu ni ishara ya kutoandaliwa.

Katika hali hii, Mh Magufuli hakupaswa kujaribu uraisi, Kujaribu huku ni kuitia majaribuni Tanzania na demokrasia yetu , uchumi wetu, utu, na uzalendo. Tumeshuhudia malalamiko ya wadau katika maeneo mengi yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi, kiharakati n.k.

Hatukushangaa kauli za kuwaita wasaliti wale wabunge waliokwenda kumtembelea mbunge mwenzao kule gerezani na kuishia kuachia nafasi zao kwenye kamati za bunge ili kuonesha kukerwa kwao.

Hatutashangaa kuendelea kuwa kimya kwa wasomi wetu na wastaafu hata pale wanapoona misingi inavunjwa, kumejengeka hofu kubwa kwa sabababu ya mtu mmoja kutoandaliwa na kuikosesha jamii nzima furaha na mustawa.

MWELEKEO WETU
Mwelekeo sio nzuri katika maeneo mengi ingawa watawala hawataki kusikia hilo. Jamii inajengeka hofu na visasi, kubaguwana na kutishana, Hili naamini liko hadi CCM chama Tawala. Kuna watu wamenyamaza kimya kwa uoga tu lakini naamini hawafurahii yanayotendeka.

Uchumi wetu hauoneshi afya njema, uwekezaji uko majaribuni, siasa na demokrasia inayumba, n.k.

MWISHO.

Rais na washauri wake waisome hali na kuja na majibu muafaka, hili la kutoandaliwa au kujiandaa isiwe sababu ya kutaka kupoteza Tanzania yetu. Binadamu ana uwezo wa kujifunza pale anapokosea. Rais afanye self evaluation ya uongozi wake kwa nini watu wanalalamika na wasaidizi wasimuendekeze mkuu wetu huu ndio uzalendo. Uzalendo ni pamoja na kusimamia misingi yote ikiwemo ya UTAMADUNI, KISIASA, KIUCHUMI n.k ambayo inaongozwa na katiba NA SHERIA ZAKE.

Kwa wale wanaokwazika na Rais Magufuli, tumchukulie huyu hakuandaliwa hebu tujaribu kumshauri abadilike. Miaka miwili inatosha kujitathminini cha msingi abadilike.

Huwezi kuvunja KATIBA kwa kisingizio cha uzalendo halafu ukaachwa BILA KUAMBIWA.

Tubadilike wakati ni sasa kwa ajili ya Tanzania yetu.


Kishada.
 
Licha ya kuandaliwa pia HANA KIBALI kutoka kwa Mungu na hata afanye jambo lolote zuri kwa watanzania machoni pa Mungu ni bure tu!!

Mungu hawezi kwenda pamoja na huyo mtu na tusitegemee uchumi wa viwanda chini ya utawala wa huyu nebukadreza
 
Nadhani hlilo ndio la msing
Licha ya kuandaliwa pia HANA KIBALI kutoka kwa mungu na hata afanye jambo lolote zuri kwa watanzania machoni pa mungu ni bure tu!!

Mungu hawezi kwenda pamoja na huyo mtu na tusitegemee uchumi wa viwanda chini ya utawala wa huyu nebukadreza


Hayo ndio na Mungu atakuja kutuonyesha soon........................... Maana sio kwa shdia hizi kwa kweli khaaa Bora tuu utabirii wa Lema ufikie
 
Walau tungeoneshwa njia na kule tunakotaka kupelekwa baSI INGEFURAHISHA SANA.
 
Kuna makondokando mengi ambayo utatuzi wake ulihitaji muda na mikakati. Usishangae mkuu alitaka kuvuta mass ya wapiga kura kipindi kile kwa kuanzisha hii mahakama na kusahau meno ya sheria kupitia KATIBA MPYA.

Hapa hakujuwa kipaumbele tu.
 
areafiftyone
Yaani hujaelewa kweli ? Basi rejea kusoma tena. Katika bandiko kuna viashiria vingi vya kukosa kuandaliwa kwa JPM ikiwemo kauli zake mwenyewe. Hapa tunamchambuwa mwenyewe kwa kauli zake sio kumlinganisha na yoyote. Wewe tusaidie kwa kumlinganisha utafanya la maana sana.
 
Ni kweli hakuandaliwa kuwatetea majizi na kuwalinda wazungu ili waendelea kutwibia madini yetu,ulitaka tuwape majizi urais waendelea kututesa walala hoi na wewe na maswaiba wako muendelea kupiga dili na kusafiri nje?au ulitaka serikali ya kupiga dili ili wapinzani wapate mtaji kwa udhaifu wa serikali waimarike kisiasa kwamba wanawatetea wananchi?.

Kwani kuna wakosoaji wa mana siku izi?wakosoaji wanakosoa wezi wa madini yetu wanavyoshughulikiwa eti jpm dikteta anavunja katiba.daaa jpm ana kazi hii ndo ghalama ya kurudisha equality utaona watu waliokua wanaishi kwa mazoea wanavopiga kelele.jpm kaza buti
 
Kwa kutumia akili njema, alipaswa kuwa msikivu na mnyenyekevu kwa vile (kama alivyokiri) hakuwa amajiandaaa (ameandaliwa).

Sasa anapofanya na kusema (huku akijua hakuwa fit kwa nafasi ile) kana kwamba anajua hapo ndipo anapoharibu na alipokwama kabisa.

Sijui ni kwa namna gani atasaidika maana inasemekana hata wasaidizi wake wanaogopa kumshauri hasa kwa mambo asiyopenda kusikia. Hivyo wanaishi naye kinafiki nafiki tu.
 
Ukishashiba wakati mwingine unaweza kwenda kupumzika tu ili shibe yako itulie vozuri tumboni
 
Tatizo ni kwamba mmekariri marais,

Magufuli ni mwanaume, mwanaume anatakiwa kujiamini na kukisimamia madhubuti kile anachokiamini bila kuyumbishwa na hapo ndipo Tanzania ilipokua imefikia tulikua hatuhitaji tena Rais wa kuchekesha na kufurahisha watu.
 
Huuu sio muda wa kuwaandaa watu na kuja kufanya utumbo, huu ni muda wa kkkkaazzziiii
 
Thread ya siku hii nimeipenda, je MTU mwenyewe atabadilika kwanza alishasema yeye hapangiwi na mtu ukimpangia ndiyo kabisa umechokoza.

Mawazo yako mazuri kwa kiongozi anayependa kujifunza lakini huyu wa kwetu hamna kitu nakuambia kaka.

Miezi sita ijayo khali ya uchumi itakuwa mbaya zaidi hapo ndipo Furaha ya maisha itazidi kupotea Mara dufu.
 
Back
Top Bottom