Hakuna derby kati ya Azam na Simba au Azam na Yanga!

Ulichoandika hapa hakina tofauti na wanachokifanya Azam kujaribu kuipromote Azam FC kuwa na derby dhidi ya Yanga au Simba
Azam na hizo timu tajwa zinatokea mkoa gani?
Kama zote ni DSM = Mkoa mmoja basi ni Derby na kama ni mikoa tofauti basi haina sifa ya derby.
(Maelezo yangu ni kutokana na kamusi za kiingereza).

kama unatatizo na ubunifu au juhudi za wenzako basi ni tatizo jingine.
 
tunapenda ku complicate mambo ili tuonekane tu tunajua, huyo nae kaja na kitongoji kweli waelimishaji wanakazi.
shirikisha ubongo wako kwanza kuelewa maana ya neno kitongoji kabla vidole vyako havija andika mashudu kijana.
 
Kwa Mimi navyojua derby ni timu mbili zinazotoka mji/Jiji Moja, zenye historia Fulani, inaweza kuwa ya uhasama au jambo lolote lile,

Mechi ya yanga vs kmc huwezi sema ni derby kwakua hawana historia yoyote kati Yao hao wawili.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
mji mmoja sio kitongoji kimoja, sema Derby ni ya timu mbili, haiwezi kuwa timu 3 ndani ya mji mmoja
Screenshot_20240207_192548_Opera.jpeg
 
Wewe ndiyo hushirikishi ubongo sasa, bandiko lako mwenyew linasema mji na bado unapinga sio.
Kwa upande wangu niliandika shudu kwani nilishangaa eneo la kijiografia umeliweka kwa level ya kitongoji ambayo kwa nchi yetu ni eneo dogo sana.
hakuna sehemu nilipopinga mji ila naona nilivotaja kitongoji imewachanganya na kusema sio kitongoji bali ni mji.
 
Azam na hizo timu tajwa zinatokea mkoa gani?
Kama zote ni DSM = Mkoa mmoja basi ni Derby na kama ni mikoa tofauti basi haina sifa ya derby.
(Maelezo yangu ni kutokana na kamusi za kiingereza).

kama unatatizo na ubunifu au juhudi za wenzako basi ni tatizo jingine.
kule Spain kuna Real Madrid yuko jiji la Madrid na Barcelona yuko jiji la Barcelona baina yao hawa wanatofautina zaidi ya kilomita 500

Hata Germany pia Dortmund yupo jiji lake na Bayern yuko jiji la Munich hawa nao wanatofautiana zaidi ya kilomita 600.

Sasa hebu niambie hizi nazo sio derby kwa sababu zinatoka majiji tofauti?
 
London Derby Chelsea Vs Arsenal
North London Derby Totenham vs Arsenal
Mersey Side Derby Everton Vs Liverpool
Manchester Derby Man City vs Nyumbu Utd


West Ham, Fulham, Nottingham Forest, Crystal Palace, Brentford hizi zote ziko London lakini husikii zinaitwa Derby baina ya Chelsea, Arsenal au Totenham.
Screenshot_20240208_071822_Firefox.jpg

Tatizo mnakariri vibaya, ama mnalazimisha kuelewa vile akili yako inataka na si vile hali ilivyo. Derby ni nyingi kuliko unavodhania
 
London Derby Chelsea Vs Arsenal
North London Derby Totenham vs Arsenal
Mersey Side Derby Everton Vs Liverpool
Manchester Derby Man City vs Nyumbu Utd


West Ham, Fulham, Nottingham Forest, Crystal Palace, Brentford hizi zote ziko London lakini husikii zinaitwa Derby baina ya Chelsea, Arsenal au Totenham.
Siyo lazima timu
Derby ni match between local revels, kwa maana timu zinazotoka kwenye mji mmoja au kitongoji kimoja. mechi yao ina qualified kuitwa derby.
kwa mfano
Arsenal vs Fulham ni London Derby
Arsenal vs Chelsea pia ni London derby.
Arsernal vs Spurs
Arsenal vs West ham

Hizi zote zinaitwa London Derby.

Man UTD na Liverpool ni watani na mahasimu wa Jadi, ila mechi yao haiitwi Derby.
Inaitwa Northwestern derby. Mnavyoandika vitu jaribu kufanya research kwanza. Kuna intercity derbies. Liverpool mpaka Manchester ni over 50 km.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom