Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Amani iwe nanyi wanajamvi!

Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.

Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.

Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!

Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!

Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.

Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.

Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.

Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.

Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.

Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.

Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.

Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show
Mlivyokula kwa mlango wa nyuma vinatosha sasa......embu tuooneni huruma na sisi watu wa chini.........na mumuogope Mungu.
 
magu ni dikteta kwa lipi? Haya?

1. kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

2.kusimamia watumishi wa uma kutimiza wajibu wao ipasavyo.

3. kukusanya mapato ipasavyo.

4. kuondoa urasimu na kuongeza uwajibikaji.

kama hayo yanamfanya mtu kua dikteta: basi ni vyema kua na madikteta wa aina hiyo.
 
Mimi sijaelewa mpaka sasa hv watanzania wanataka rais wa aina gani!!!??? Unajua ni ngumu hata kuwaelezea!!!! Hivi rais asipofanya haya anayoyafanya nchi ingekuwajeeee! Watz wanachokitaka hawakitaki! Wasichokitaka wanakitaka! Wanachikitaka wanakikataaa! Shaaaame! Mnatakaka mini nyieeeeeee!

Tatizo watanzania tumejaa unafiki sana......Mungu msaidie Magufuli azidi kutumbua haya Majipu yaliyokomaa.
 
Eti wameporwa uhuru wao....hivi walipokuwa na huo unaouita uhuru walilifanyia nini taifa?Umesahau mapema kuhusu hawa wezi..
Magufuli go go go
 
siku moja uwe kiongozi halafu uige staili hii uone utakavyo baki peke yako. kimsingi wote hatupendi uzembe kazi, lakini je, inawezekana mkuu wa mkoa kupita kuhakiki taarifa alizo pewa na wasaidizi wake? mimi ninge muelewa kama angewaadhibu wakurugenzi na wakuu wa idara walio mpa Mkuu wa mkoa taarifa za uongo.

Mkuu hiyo ilikua iwe kazi ya Mkuu wa mkoa kuhaikiki taarifa anazopewa na watendaji na kuwachukulia hatua endapo atabaini zipo kinyume kiutekelezwaji Nadhani upate wasaha wa kusikiliza alicho kisema Anna Kilango siku anakanusha kuhusu kutokua na watendaji hewa ........
 
Hapo ndio tunatofautiana kuelewa mambo. kazi ya kuhakiki watumishi hewa kwa vyovyote vile ilifanywa na kamati maalumu ambao ni wasaidizi wa mkuu wa mkoa. sasa kama kamati uliyo iteua hujawaamin ukaenda kuhakiki mwenyewe sasa kuna sababu gani ya kuwa na RAS, Wakurugenzi wa Halmashauri na wengineo? Ni sawa na kusema Rais akipewa taarifa say na TAKUKURU AU CAG aende tena kuhakiki taarifa zile. mimi ninge muelewa kama angewafukuza wasaidizi wa mkuu wa mkoa wote kwa kumpelekea taarifa za uongo.

kazi ya kuwafukuza wasaidizi wa Mkuu wa Mkoa ilipaswa ifanywe na mkuu wa Mkoa mwenyewe baada ya kugundua alichopewa sio sahihi badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kutangaza kwa unabe, Ukaguzi wa watumishi hewa ni kazi kubwa waliyokabidhiwa wakuu wa mikoa na Raisi mwenyewe kama kipaumbele chao cha kwanza so hakupaswa kukurupuka kwa kusema anawaamini watangulizi wake ati wako sahihi...... Tufike mahali tukubali kuwa kuna uzembe japo hakuna mtu anapenda kufukuzwa kazi,.......
 
Kukosoa ni jambo la kawaida kwani katu watu hatufanani mitazamo ndio kunakuwa na mijadala.....lakini kukosoa huko kuwe na mantiki.....
Kumbukumbu yangu inaniambia kuwa wengi wetu humu tulikuwa tukilalamikia jinsi serikali isivyowachukulia hatua watendaji wake wabovu.....lakini leo hii sisi tena ndio tunalalamika kuwa kwanini anachukua hatua....hivi sisi tutakuwa na akili za aina gani....tulitaka aharibu kiasi gani ndio tuone kuwa anastahili kuwawajibishwa...??
Tulitaka akosee kosa gani hadi tuone kuwa anastahil kuwajibika.....au kuwajibishwa....ifikie kipindi mahaba tuyaweke kando na tuache uzalendo utamalaki kwenye nyoyo zetu.....

TANZANIA KWANZA....

umenena Vyema kiongozi kuna watu hawaoni kwamba zaidi ya Milioni 300 zilikua zinateketea kwa watendaji hewa na mpaka jana kulikua na ongezeko na kufikia watumishi hewa 102 kwa wilaya zote za shinyanga. Sasa sijajua kutoa kuambiwa hakuna mpaka 100+ still tunaambiwa tunyamaze ili kesho waseme ...'' walipolisababishia taifa hasara waliwahamisha ama kuwa samehe''......
 
Utawala wa aina hii tumeusubiri kwa muda mrefu sana, mlizoea kuwa mtu akiharibu anahamishwa, ukiharibu unapumzishwa tu, Ulitaka mama kilango asifiwe kwa kudanganya umma? Sio kiongozi makini na mfuatiliaji, alitakiwa ajiridhishe, Hapa kazi tu na Magufuli ndo tuliyemtaka.
 
kazi ya kuwafukuza wasaidizi wa Mkuu wa Mkoa ilipaswa ifanywe na mkuu wa Mkoa mwenyewe baada ya kugundua alichopewa sio sahihi badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kutangaza kwa unabe, Ukaguzi wa watumishi hewa ni kazi kubwa waliyokabidhiwa wakuu wa mikoa na Raisi mwenyewe kama kipaumbele chao cha kwanza so hakupaswa kukurupuka kwa kusema anawaamini watangulizi wake ati wako sahihi...... Tufike mahali tukubali kuwa kuna uzembe japo hakuna mtu anapenda kufukuzwa kazi,.......
Kwa mtu mgeni kudanganywa hakukwepeki, hata yeye Rais siku za mwanzo
Utawala wa aina hii tumeusubiri kwa muda mrefu sana, mlizoea kuwa mtu akiharibu anahamishwa, ukiharibu unapumzishwa tu, Ulitaka mama kilango asifiwe kwa kudanganya umma? Sio kiongozi makini na mfuatiliaji, alitakiwa ajiridhishe, Hapa kazi tu na Magufuli ndo tuliyemtaka.
Alichofanya Rais ni kama kuchana picha wakati Negative ameiacha!! kwa maana waliosababisa uongo kwenye taarifa ile bado wapo na wanaendelea na kazi zao.Ukitaka kumaliza kabisa Malaria inakubidi uangamize mazalia ya mbu.
 
Kwa mtu mgeni kudanganywa hakukwepeki, hata yeye Rais siku za mwanzo

Alichofanya Rais ni kama kuchana picha wakati Negative ameiacha!! kwa maana waliosababisa uongo kwenye taarifa ile bado wapo na wanaendelea na kazi zao.Ukitaka kumaliza kabisa Malaria inakubidi uangamize mazalia ya mbu.

Mkuu kumbuka na katibu nae hayupo ambaye ni mfano tosha kwa waliobaki.....
 
Amani iwe nanyi wanajamvi!

Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.

Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.

Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!

Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!

Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.

Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.

Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.

Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.

Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.

Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.

Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.

Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show
ni ujinga kumtetea mkuu wa mkoa ambaye analetewa taarifa na kuimeza kama ilivyo bila kujiridhisha,

huku akijua nyuma yake kuna agizo la raisi kuhusu kushughulikia watumishi hewa.
alichokipata kinamstahili mwacheni jpm afanye kazi yake,

waliozoea utawala uliopita watapata shida utawala huu naamini watajiondoa mmoja mmoja.
 
Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi

Kosa la kilango sio dogo,hiyo mishahara hewa watu wamelokea kwa muda gani?kiasi gani? Ni upumbavu kupinga utawala huu.ninyi ni wale walionufaika na ule utawala wa kipumbavu zaidi
 
Lugha yake mtu humtambulisha yeye ni nani na amekulia mazingira gani. siyo lazima utumie Lugha isiyo na staha ndio ufikishe ujumbe wako.
 
Back
Top Bottom