Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Hatimaye nimepata Takwimu mpya za Elimu kwa mwaka 2009. Haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania wanafunzi kuingia Sekondari kwa wingi kama wakati wa kipindi cha Edward Lowassa. Historia itamsuta kwa mengi lakini kwa hilo jamani tumpe hongera yake. Hongera Edward Lowassa!
Ni kweli kwa ujumla shule za Kata ni za kiwango cha chini hasa ukizingatia kuwa kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa na Walimu wa Vodafasta. Ndio, wanafunzi wa shule hizo wanakaa kwenye ndoo kama walivyopigwa picha kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi la leo. Naam ni kweli kabisa kuwa wananchi waliburuzwa sana tu ili wajenga shule za Sekondari.
Pamoja na hayo yote ni heri mwanafunzi akae chini shuleni kuliko kukaa tu nyumbani. Pia ni heri tushughulikie suala la ubora wa elimu wakati wanafunzi wako tayari mashuleni kulikuwa kulishughulikia wakati wanazagaa mitaani. Pasipo na mori wa Kilowassa na Kisokoine hatutaweza kuendeleza sekta hii ambayo ndio msingi mkuu wa kuwatokomeza wale maadui wanne wa maendeleo: Umaskini, Ujinga, Maradhi na Ufisadi (Hilo la nne sijaliongeza mimi, aliliongeza Mwalimu Nyerere mwenyewe kwenye Hotuba zake za miaka hiyo - kama mnataka rejea nitawatumia hivi punde!)