Haki za Abiria ni Zipi?

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Ukikata tiketi ya basi au ndege utakuta kwenye tiketi hiyo kuna masharti kadha wa kadha ambayo yanamuweka abiria kuwajibia. Lakini haki za abiria huwa haziwekwi wazi kwenye tiketi hizo. Je haki za abiria zikoje katika nyanja zifuatazo:

1) Uzani wa na aina ya Mizigo anayoruhusiwa kusafiri nayo bila kutakiwa kulipia gharama za ziada. Kwa wasafiri wa ndege huwa ni kilo 20 bila kujali aina ya mzigo. Kuna baadhi ya mabasi nayo yanaruhusu kilo 20 lakini kuna baadhi ya mizigo hata kama uzani wake haufikii kilo 20 lazima uulipie. Lakini ukipanda magari ya mikoa ya kusini, hata begi la nguo utalazimika kulilipia. Je hakuna sheria inayomlinda abiria kuhusiana na suala hili?

2) Kwa upande wa abiria mabasi nyuma ya tiketi watakueleza sharti kuwa Abiria anatakiwa kuwahi kituoni kwa ajili ya safari kama ilivyoandikwa kwenye tiketi, na ikitokea ukachelewa utarudishiwa nauli pungufu ya kiasi ulicholipia. Lakini unaweza kukuta abiria wanazo tiketi zimeandikwa muda fulani basi litaanza safari, muda huo unafika na kuzidi kwa zaidi ya nusu saa (kwa abiria wa treni unakutana na tangazo kuwa safari imeahirishwa hadi siku nyingine). Je kwa nini kusiwe na sheria ya kuwawajibisha wamiliki wa mabasi kwa kuwachelewesha abiria?

Leteni maoni yenu wana JF
 
Back
Top Bottom