Haki ya mtuhumiwa ni pamoja na kabali ya polisi...........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
04_12_uhvwv5.jpg

Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Morogoro, wakimrejesha mahakamani mtuhumiwa aliyetambuliwa kwa jina moja la Linus, mkazi wa mjini hapa, baada ya kukamatwa na wananchi akitimua mbio kutoka kortini muda mfupi kabla ya kuanza kwa kesi yake na wenzake ya wizi wa pikipiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro. (Picha na John Nditi).
 
"......haki ya mtuhumiwa ni pamoja na kabali ya Polisi....."

Heading ina ujumbe mzito sana.

a. Polisi wamemwokoa katika mikono ya wananchi ambao bila shaka wangemtenda isivyo. Polisi wanajitahidi kuhakikisha mtuhumiwa anapata haki yake ya kusikilizwa kutokana na tuhuma za wizi zinazomkabili.

b. Katika mazingira hayo ya utoro hakuna namna nyingine ya kumshika? Je, angeshikwa nyuma ya mkanda asingefika?
 
Ruta picha ina maelezo mengi sana
Je hao polisi hata pingu hawakuwa nazo mpaka wamkabe kihivyo
japo ameokolewa kwenye mikono ya wananchi "wenye hasira kali" hiyo kabali imezidi kipimo
 
Picha kweli inamaelezo mengi, maana pia huyo mtuhumia naona ni mfugaji au jamaa alikuwa kasimama? mambo ya ma-mwinyi hayo.
 
Back
Top Bottom