Elections 2010 Haki Kupokwa, Dawa ni Nini sasa?

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
Nimekaa nikatafakari bila kupata jibu hatua ya kuchukua kwa hili la Kupokwa haki yetu ya msingi, haki ya kupiga kura kuchagua kiongozi tunayemtaka na kisha kupatiwa kile tusichokitaka.

Naomba kujuzwa, ilichukua siku ngapi TUME ya UCHAGUZI (NEC) kusambaza vifaa vya kupigia kura? Je muda huo unalingana na huu wa kurudisha vifaa hivyo kutoka kule walikovipeleka?

Matokeo baada ya kuhesabiwa, ilichukua siku ngapi kujumlisha katika kila jimbo? Je jumla ya kituo kwa kituo ilihitaji SCIENTIFIC CALCULATOR kupata jawabu?

Tunajua NINI KIMETOKEA!! Sisi si WAJINGA kiasi hiki.

Sasa tufanye nini? Twende mahakamani kupeleka kesi ya Ngedere kwa Nyani? Tumshitaki Rais ilhali hashitakiwi kwa mujibu wa Katiba ya JMT? Tukae tu na kupiga kelele kama WEHU? Tufanyeje sasa?

Watanzania wana desturi ya kuchukua maamuzi! Tunajua kama kibaka ama jambazi akiwa anawasumbua na kila wakati haki ikiwa haitendeki ipasavyo huchukua hatua kukomesha hali hiyo ili sauti yao isikike.

Kwa nini tusichukue hatua? Hatua ya kumuonesha kila aliye dhalimu kuwa HATUKUKUCHAGUA!! Bali ULIJICHAGUA nasi hatuko tayari UTUTAWALE kwa namna Uliyoichagua wewe! CCM wajue na kwa hakika watambue kuwa haki ya wengi haichezewi kwa namna hii na wao si Miungu kwa Watanzania.

Tunahitaji uchaguzi Huru na wa Haki, tunahitaji TUME HURU, majimbo yenye utata uchaguzi urudiwe. Naam tuwafanye warudie uchaguzi na tukomeshe wizi wa kura kuanzia chini kabisa. Kwa kuwa tunawajua hawa waliopora Haki yetu, kwa tamaa zao za kuwa Wafalme miongoni mwa Watanzania masikini wa kutupwa wenye rasilimali zinazonufaisha wawekezaji, tuwaambie wewe si kiongozi wetu hatukuhitaji, ACHIA ama TUTAKUACHISHA. Kwa kuwa kuachia si rahisi kwao basi Tuwaachishe!!
 
Tukifanya migomo na maandamano mimi binafsi naona ndiyo njia muafaka ya kuelezea kutoridhika kwetu. Viongozi wa Siasa itisheni maandamano nchi nzima. Ili linawezekana kufanyika. Watanganyika wa leo siyo wa kubezwa wanaweza, wameamaka toka usingizini wanahitaji mtu wa kuwaongoza kjitwalia haki zao mikononi mwao. Maandamano yafanyikie Dar es Salaam, maana Dar es Salaam ndiyo kichwa cha nchi. Wabunge wote waliopata viti waje Dar es Salaam kushiriki kupanga maandamano. Maandamano ndiyo siraha pekee yenye uwezo wa kuwakomesha watu wenye vichwa vigumu kama hawa.
 
Back
Top Bottom