Hadithi Ya Wafungwa kwenye Pango (Fumbo la Maisha)

Hapa naona ni imani ndo imeguswa sana watu tukizaliwa kwenye imani ya ukristo au uislam tuna imani izi imani ni bora kwamba zingne ni ushetani tu

Watu atutaki kujifunza na imani nyingne tunajiona imani zetu zipo salama kabisa aziitaji ata kuchunguzwa.
 
Hii hadithi inatuangukia sisi waafrika. Shule na dini ndio hasa vifungo vyetu vinavyotutengenezea zuio la kufikiri nje ya tulivyofundishwa.
Hapo wametuweka kwenye mapango ya DINI SIASA na UCHUMI

Mf. shule tunasoma vitu kinyume hasa na uhalisia wa mazingira yetu, kutokana mitaala yao haiendani kabsa na mazingira yetu. Mahali tumewezwa hasa na kuwezekana ni kwenye dini.

Mungu wa vitabani ukimfikiri sana ambaye ndiye chanzo cha dini nyingi unaona kuna vitu havipo sawa kiasi tumempa MZUNGU Id ya ubinadamu.
Hua natafakari hivi "kwa nini wafu kwao wawe watakatifu na wa kwetu wawe mizimu?
Jambo la pili "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" tukiweza kupata codes na ku unlock this statement tutakua tumepona.

Ukiigeukia siasa ndipo pango kulichomoka ni ngumu. Kwa ufupi siasa dini na uchumi ndio mapango yetu tumo humu ila
pango hatari kabisa ni dini.
 
Mzee wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
 
Animation ya The croods nahisi wamechukua mawazo kutoka kwenye hii hadithi.
images%20(84).jpg
 
Hili si fumbo per say.

Ni analogy, ni falsafa.
Falsafa ya ufaham, falsafa ya mtazamo (relativistic perspective).
Kikubwa zaidi ana-demonstrate kwa jinsi gani pamoja na ujuzi wote tunaodhani tunao kuhusu 'reality' ni kwa namna gani tunaweza kuwa wrong kabisa au yaani tunajua kidogo mno.

Ni falsafa fikirishi ya kujiuliza "Tunajua Kweli Tunachojua?" Na " Tutajuaje zaidi kama hatujui zaidi?"

Point ya muhimu zaidi ni pale ambapo anakuja mtu aliyeona ambacho hujawahi ona wala kufikiria.
Hii ndo ilipelekea akina Gallileo kuuawa. Wao walikuwa ni mfano wa huyo mtu mmoja aliyekuwa pangoni akatolewa, akaona, halaf akarudi kuwaambia na wengine. Lakini wa pangoni walikuwa comfortable sana na vivuli vya pangoni kiasi kwamba walichukizwa na dhana ya tofauti kabisa ya ukweli.
Plato aliona mbali mno.
Na kitu kinachofurahisha sana ni kwamba hali hii ni sugu katika historia ya binadam mpaka sasa. Na mifano ni mingi mpaka leo.
 
Hii ni hadithi ambayo ilikuwa ni fumbo ambalo mpaka leo hii Plato hatasahauliwa kwa kuweza kutumia ufahamu wake kuelezea uhalisia wa maisha na ufahamu wa mwanadamu ulivyo kwa ujumla. Ni mfano ambao kila mtu ameachiwa tafsiri yake ni kila mtu atauelewa kutokana na mwanga alioweza kuuona maishani wake.

Miaka za zamani kulikwepo na mwanafalsafa mmoja aliyekuwa anaitwa Plato katika tamaduni za wagiriki. Naamini wengi wanamfahamu Plato kama mojawapo kati ya wanafalsafa wakubwa walioweza kufundisha mengi Ugiriki na maisha yake kuheshimiwa kutokana na utambuzi wake juu ya falsafa na maisha kwa ujumla.

Plato

Plato Aliwahi kuhadithia hadithi moja. Hadithi hiyo aliielezea kwa kufafanua maisha kwa ujumla yapoje na mwanadamu na ulimwengu.

"Fikiria pango ambalo ndani yake kuna watu wamefungwa tangu walipozaliwa na maisha yao wamefungwa ndani ya pango hilo.

Wafungwa walio ndani ya pango na hawawezi kutoka wala kugeuka nyuma

Na katika kufungwa kwao wamelazimishwa kutazama ukuta uliokuwa mbele yao. Watu hao wamefungwa shingoni na nyuma na wala hawawezi kugeuka nyuma kutazama kilichopo nyuma lakini maisha yao wamekuwa wakitazama mbele tu na wameshazoea na hawafahamu tena kama kuna kugeuka nyuma.

Wafungwa waliofungwa na kuutazama ukuta maisha yao yote wakiishi kuutazama ukuta, mwanga hafifu wa moto uliopo nyuma yao, na wakisikia sauti za wapita njia bila wao kuwatambua wala kutambuliwa.

Nyuma yao kuna moto unawaka. Na katikati ya moto ule unaowaka muda wote na pango wafungwa walipo kuna barabara inayopita kwa juu. Na fikiria kila siku kuna watu mbalimbali wanaopita kwani barabara ile ilikuwa inakwenda sokoni. Wanapita watu wa aina mbalimbali, mizigo na wanyama au mifugo. Vivuli vyao vinaonekana kwenye ukuta ambao wale wafungwa wanautazama muda wote na kutengeneza aina mbalimbali za vivuli vinavyopita na vinaonekana ni vikubwa na wao hawafahamu chochote kuhusu kilichopo nyuma yao na moto ule una mwanga hafifu unaotengeneza vivuli vya vitu na watu wanaopita kwenye barabara iliyopo katikati ya mwanga wa moto na kuelekea kwenye pango la wafungwa.

Barabara ya kwenda sokoni iliyopo nyuma yao ambayo wapita njia wanapita bila kujua kuwa kuna wafungwa chini. Wapita njia hao vivuli vyao na vya wanyama na mizigo yao huonekana kwenye ukuta mbele ya wafungwa na sauti zao na zikisisika na wafungwa bila kufahamu zimetoka wapi.

Fikiria maisha yao yote wao wanaona hicho ni kitu cha kawaida na hiyo ndio dunia yao. Maisha yao yote wanazaliwa wapo kwenye pango na mpaka wanakufa wao wanatazama projection ile tu na hawajui lolote mpaka wanamaliza maisha yao Vizazi na vizazi zinapita na kuona hiyo ni kawaida. Vivuli, sauti za wapita njia, sauti ya moto unawaka lakini hawajui vinapotoka bali hujua vile vivuli ndio chanzo.

Sasa fikiria endapo mfungwa mmoja akatolewa kwenye pango, anapowekwa nje ambapo kuna mwanga wa jua na yeye hajazoea ni lazima ataumia sana na itamchukua muda kuuzoea kwani maisha yake yote na vizazi vyake hakuwahi kuhimili mwanga kama huo. Na akiweza kuona atashangaa sana. Atagundua kuwa alikuwa hafahamu chochote na hakutegemea kufahamu hayo.

Mfungwa aliyeishi maisha yake yote kufungwa kwenye pango na kutazama ukuta tu akifanikiwa kuuona ulimwengu na maisha mengine ambayo hakuwahi kuyaona maishani mwake.

Fikiria mfungwa yule aliyefunguliwa akaamua kurudi kuwajulisha wenzie kuwa kuna dunia tofauti na hiyo, endapo akirudi kwa pale barabarani kwa juu na kuwaambia kuwa "Jamani geukeni" wenziye hawatamuelewa. Watabaki kushangaa kuwa wanasikia sauti lakini hawajui imetoka wapi kwani wanatazama mbele na pia watabakia kuona kivuli cha lijitu au kitu kikubwa kipo kwenye ukuta wanaoutazama na hawatafahamu wanaambiwa nini na nani.

Sauti yake itakuwa kama makelele, kivuli chake kitakuwa kama kinawakera muonekano wake au kitakuwa kinawachanganya kufahamu ni jitu gani hilo limetengeneza kivuli kwani hawawezi kugeuka nyuma wala hawafahamu kuna kugeuka nyuma.

Kivuli cha yule mfungwa aliyeweza kuona maisha mengine na sasa amekuja kuwaita wenziye lakini hawezi kuingia ndani bali amekaa naye kwenye barabara ya nyuma ya wafungwa na kivuli chake kuonekana mbele ya wafungwa wanaoishi kwenye pango na sauti yake kuwashangaza wenziye. Wenziye wanashindwa kufahamu mwenzao anasema nini na wanamtafsiri katika uelewa wao wa maisha yao na picha waonazo kwenye ukuta ndani ya pango

Na pia endapo akipewa nafasi hata kushuka kwenye pango chini na kuongea na watamuona kama amechanganyikiwa kwa ambayo atakuwa anawaeleza kwani wao hawakutegemea kabisa. Pia itawachukua muda na wao kuzoea mwanga wa nje kwani walizoea giza. Na inaweza kupelekea hata wakamuona yeye ni tofauti na wao na kumshangaa au kumtukuza.

MAANA.
Mpaka leo limebaki kuwa ni fumbo japokuwa wengi wamekuwa wakijaribu kutafsiri Plato alikuwa anamaanisha nini alipokuwa akielezea uhalisia wa mwanadamu. Fumbo hilo kila mmoja anaweza kulifikiria kivyake na kujitahidi kujitoa katika pango na kuweza kujitambua zaidi. Nimependa kushare hadithi hii kwani mara ya kwanza mimi kusoma hadithi hii ilinigusa sana na nikahisi inaweza ikawagusa wengine kivingine au kama nilivyoguswa nayo.

ASANTENI

VIDEO YAKE KWA WATAKAOPENDA KUONA PICHA HALISI YA HADITHI TAZAMA VIDEO HII.

Ni fumbo la Roho na Mwili. Fumbo linahusu kujitambua au True Self realization. Roho inakuwa mtumwa wa Mwili na Mambo yake ambayo ni ya ki Dunia(Jela). Licha ya kwamba Roho ni ya milele ikiwa Mwilini inapoteza Ukweli kwamba, haifi, haina njaa, haina kiu, haina nyege, ina own kila kitu hivyo sio masikini, sio binafsi hivyo inaupendo wa kweli na ni kamili na timilifu.

Tafsiri ya ukuta ni limitation of our prosperity, achievemts, happness and fulfillment which end when we part with our bodies during death.

Tafsiri ya mfungwa aliona maisha mengine na anashindwa kuwambia wafungwa waliobaki Jela ni ugumu wa mawasiliano kati waliohai na wafu. Roho ilikufa haiwezi rudi kuwaambia walio hai what is life after death. If we new kwamba mafanikio yoote ya maisha ni kazi bure kwani ni ya mwili ambao hufa. Tusingelihangaika na maisha kaisi hicho tungeamua kufa kwa namna yeyote hii ndio tafsri ugumu wa kugeuka nyuma licha ya kwamba tunaitwa tufe.

In short the big lesson here is although we may think and approve the way we live and the way we term our successes, happyness and fulfillment but we should realize "There is nothing to achieve except realize that. "

Tafsiri ya aliyegundua maisha mazuri na bado hawezi kuchangana na wale waopita kwenda sokoni au kushindwa kuyaishi maisha mapya bado anarudi kuwajuza wafungwa wanzake ni kwamba inabidi kuijua KWELI tukiwa hai mwilini.

KWELI inatambuliwa rohoni na unaishi nayo maishani, sio simulizi. KWELI inakuweka huru milele.
 
Hili si fumbo per se.

Ni analogy, ni falsafa.
Falsafa ya ufaham, falsafa ya mtazamo (relativistic perspective).
Kikubwa zaidi ana-demonstrate kwa jinsi gani pamoja na ujuzi wote tunaodhani tunao kuhusu 'reality' ni kwa namna gani tunaweza kuwa wrong kabisa au yaani tunajua kidogo mno.

Ni falsafa fikirishi ya kujiuliza "Tunajua Kweli Tunachojua?" Na " Tutajuaje zaidi kama hatujui zaidi?"

Point ya muhimu zaidi ni pale ambapo anakuja mtu aliyeona ambacho hujawahi ona wala kufikiria.
Hii ndo ilipelekea akina Gallileo kuuawa. Wao walikuwa ni mfano wa huyo mtu mmoja aliyekuwa pangoni akatolewa, akaona, halaf akarudi kuwaambia na wengine. Lakini wa pangoni walikuwa comfortable sana na vivuli vya pangoni kiasi kwamba walichukizwa na dhana ya tofauti kabisa ya ukweli.
Plato aliona mbali mno.
Na kitu kinachofurahisha sana ni kwamba hali hii ni sugu katika historia ya binadam mpaka sasa. Na mifano ni mingi mpaka leo.
I have never seen an incredible reply here in JamiiForums than this

You had a perfect narration
 
Bonge la myth la kufikirisha.

Kweli katika dunia yetu tunafungwa na mengi and sometimes we think that we know almost everything kumbe bado tuko pangoni na hatujui lolote. Wanapokuja waliojua kutuzidi tunawaona wamepotoka na kuchukulia mitazamo yao ni uongo ila tunachkijua sisi ndio ukweli.

Mfano katika dini watu wamefungwa kiasi kwamba hawaoni hata makosa yaliyopo kwenye bible. Na ukimueleza mtu some errors zilizopo ana weza kugombana na wewe without finding the fact. Pia kwanini vitabu kama gospal of thomas vimeondolewa kwenye bible no one wanna know that. Tuko kwenye pango and we think what we see is reality while not.

Big up Apollo.
 
Back
Top Bottom