Habari njema kwa nchi, gesi nyingine ya Helium yagunduliwa Bonde la Ziwa Nyasa. Tanzania kuwa muuzaji kinara Duniani

Hapa nitakufa na nitazaliwa tena na nitakufa bado gesi haijaanza kuchimbwa Liganga na Mchuchuma ilianza kuimbwa bado nipo kijijini nacheza mchezo wa kuigiza nachunga Ng'ombe na kukimbizana na kujificha kwenye vichaka mpaka leo hii nina akili zangu nimezunguka nchi nzima na mataifa mengine kadha wa kadha lakini bado madini hayo yanaimbwa tu.

Hii nchi na viongozi wetu sijui nani katuloga hata hatujui ni kipi kinatufanya kubaki tulivyo na hatusogei mbele
Liganga na mchuchuma wanaokwamisha Ni Serikali kwa kuweka vikwazo lukuki,inahitaji umeme mkubwa zaidi ya megawatt tulisonazo Sasa na haupo,Hakuna miundombinu wezeshi Kama Barabara na relo so Hakuna investor atakuja.

Juu ya hayo Kimbuka chuma kipo kila mahala Duniani ukizingua wanasepa tofauti na Gas hii ambayo inapatikana sehemu chache Sana hapa Duniani na hatuhitaji maumeme meengi.
 
Tutakuwa tunashangilia hivo hivo miaka yote kama ilivo Mwadui, Geita, North Mara, Mtwara, Bulyankulu, Chunya, Yaani unufaikaji wetu haupo kwa maslahi ya taifa, hata gesi ya Mtwara tulielezwa sio yetu na kwa aina ya viongozi waliopo ambao hawana uzalendo wanaojali matumbo yao ndio maana tunaibiwa rasilimali zetu mchana kweupe tunazidiwa hadi na Uganda na Botswana wanapata mgao wao wa kueleweka sisi ni mazezeta kabisa.
+ Buzwagi Gold Mine, Mgodi umemaliza muda wake, tumeachiwa mashimo tu
 
Unanufaika nini hata ikigundulika? Tutaendelea kushangilia hivyohivyo ila wanufaika ni vibaraka wachache tu
Usikariri maisha ukajua zama za zamani bado zipo..

Mradi ukianza commercial productions mgao utakuwa Kama huu wa gas ya Mtwara 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221201-100819.png
    Screenshot_20221201-100819.png
    86 KB · Views: 6
Helium ya mwekezaji huyo mtafiti. Kwa mujibu wa sheria zilizotungwa kwa mbwembwe na bunge la CCM ni kwamba mtafiti akipewa leseni ya kufanya utafiti atakacho kipata hapo chini ni mali yake serikali haina chake hapo itaambulia kodi kama illivyo kwenye migodi mingine. Ukumbuke mtafiti alitumia gharama zake kufanya huo utafiti
 
Helium ya mwekezaji huyo mtafiti. Kwa mujibu wa sheria zilizotungwa kwa mbwembwe na bunge la CCM ni kwamba mtafiti akipewa leseni ya kufanya utafiti atakacho kipata hapo chini ni mali yake serikali haina chake hapo itaambulia kodi kama illivyo kwenye migodi mingine
Hapa Nani anafanya Utafiti? 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221201-100819.png
    Screenshot_20221201-100819.png
    86 KB · Views: 6
Hawezi gundua mwingine afu mkagawana sawa ,tunachokipata ndio stahiki zetu'.

Ukitaka kikubwa weka teknolojia,staff na mtaji ugundue mwenyewe
Km ndo hivyo akagundue kwao yani wewe kwa akili ndogo tu kiwanja chako kina madini halaf mchimbaji akukadirie cha kukupa?? Pathetic bora yakae tu huko chini mpka wazalendo wa kweli watakapopatikana na kusaidia nchi. Mbona mwl aliacha? Huu ni upoyoyo na mindset zenu ndo zinarudisha nyuma taifa hili
 
Km ndo hivyo akagundue kwao yani wewe kwa akili ndogo tu kiwanja chako kina madini halaf mchimbaji akukadirie cha kukupa?? Pathetic bora yakae tu huko chini mpka wazalendo wa kweli watakapopatikana na kusaidia nchi. Mbona mwl aliacha? Huu ni upoyoyo na mindset zenu ndo zinarudisha nyuma taifa hili
Ndio unakadiriwa kadiri ya mlivyokubaliana kwa sababu hawakujileta Bali wewe ndio uliwaleta kwa vile huna uwezo..
 
Helium ilipogundulika mara ya kwanza yule Profesa mmoja katika University ya Uingereza alisema bei ya helium duniani inabadilikabadilika. President Magoofuli asubiri mpaka bei iwe nzuri. Yule Prof alikuwa anaitwa Andrew nani sijui.
 
Helium ilipogundulika mara ya kwanza yule Profesa mmoja katika University ya Uingereza alisema bei ya helium duniani inabadilikabadilika. President Magoofuli asubiri mpaka bei iwe nzuri. Yule Prof alikuwa anaitwa Andrew nani sijui.
Ni kawaida ya bidhaa yeyote,hata gold saizi imeshuka
 

Nchi yenye bahati ya rasilimali nyingi lakini ina uhaba wa viongozi sahihi, na haitakiwi iwe na kiongozi sahihi pale juu.

Rasilimali mtaendelea kuzishangilia tu kama mazuzu.
 
Back
Top Bottom