2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,358
- 6,060
mkuu naona umeorodhesha magonjwa mengi kwelikweli hadi umenipeleka kwenye somo la medincine na macrobiology, kitu nachoweza kusema ni kuwa nguruwe ana nyama tamu sana, hili si jambo la siri. pia ina ubora kiafya kwa kuwa ni aina ya whitemeat kama unavyojua white meat iko safe na mambo ya cholesterol na mengineyo, na zaidi ya yote hata kwa tathmini yako binafsi maeneo yanayofuga nguruwe hayo magonjwa uliyoorodhesha hayajaonyesha athari za kufikia hatua ya kuacha ulaji ama kuweka quarantine, kiasi kwamba kuna watakaosoma hapa hasa malaymen na kuona kilichoandikwa ni hadithi na si kweli japo kuna ukweli wake. umeandika magonjwa mengi ya nguruwe lakini jua kuna magonjwa mengi ya wanyama wengine pia. kitu nachotaka kusisitiza hapa ni kuwa ulaji wa nyamakwa ujumla una madhara kuliko ulaji wa mimea/majani. mfano nyama maarufu ya kondoo inatatizo la kupelekea matatizo kwenye magoti (gauti) tena kuliko mbuzi!! kwanini basi hawakuiona ni nyama haramu? i dont know?Nguruwe ambapo katika mwili wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa
Mdomo ni maficho ya vijidudu, bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na wanyama.
Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo
Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis).
Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na wanyama.
Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis Buski) hupatikana kwa wingi nchini China.
Maradhi ya Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na wenye kuchanganyika nao, na
yanaweza kuenea kwa sura ya mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya bahari ya Pacific
baada ya kimbunga. Maradhi yanakuwepo panapokuwepo nguruwe katika nchi zilizoendelea
kiviwanda kinyume na madai ya uwezekano wa kuushinda uchafu wake kwa kutumia teknolojia
mpya zinazoharamisha kula nyama bila ya kibali, hasa nchini Ujerumani, Ufaransa, Philippines na Venezuela.
Kwa kula minofu ya nyama ya nguruwe, (Trichinellosis) hupatwa na ugonjwa wa Balantidium
Dysentery. Kwani mke hubungua kuta za matumbo kwa ajili ya kuweka mayai ambayo yanafikia
kiasi cha 10,000. Mayai hayo huingia kwenye misuli kupitia damu na kugeuka kuwa ni vijiyai vyenye kuambukiza.
Ama kupata maradhi kupitia mchango wa nguruwe, ni kuwa hiyo hupatikana baada ya kula minofu ya nguruwe mwenye ugonjwa.
Minyoo hukua kwenye mchango wa binadamu na urefu wake unaweza kufikia meta saba, na
unakuwa na kichwa chenye miba inayosababisha kukwaruzika kwa kuta za michango na mchupo
mkubwa wa damu, na ana mirija minne na shingo. Aina za mke huzaliwa kama kwamba ni
wanyama pekee na hufikia maelfu. Na katika kila mmoja kati ya mnyama, huzaliwa zaidi ya mayai
elfu moja iwapo utakula Cysticercosis.
Kupatwa na ugonjwa wa minyoo ya tumbo la binadamu, hutokana na kula chakula kilichoingia
mayai na kutoa lava, na huingia katika damu kupitia kiungo chochote. Na hatari yake hukisiwa kwa
mujibu wa umuhimu wake.
Maradhi haya hayatokei kabisa kutokana na kupatwa na mchango usio na miba katika kichwa na
wenye madhara madogo
kabisa Taenia Saginata ya ng'ombe. Chanzo.MziziMkavu
KIIMANI
kwa upande wa Quran
"Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).
KWA UPANDE WA BIBILIA"Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao" wala msiguse mizoga yao (Walawi 11: 7 – 8).
tukija kwenye upande wa bibilia ni vizuri tukifahamu kuwa namna ya kusomaji na kuielewa bibilia si kama inavyosomwa quran na kuitafsiri. kuna madai nisiyoweza kuthibitisha kuwa kuran inatasfsiriwa kama ilivyoandikwa, kama ni hivyo pengine neno la petro kuotesha kushushuiwa nguruwe kwenye ndoto na akaambiwa ale lakina akakataa akasema hawezi kula najisi na sauti ya mungu ikamjibu kuwa alichokiumba mungu usikitie unajisi lingetosha kabisa kuwafanya wakristo walitumie kutetea ulaji wa nyama ya nguruwe.
kuna neno kwenye baibo linasema kuhusu: ki=umuua mzinzi, kutokufanya kazi siku ya sabato, ulaji najisi.
tukianza na;
mafarisayo walimpelekea yesu mwanamke wakimwambia sheria ya musa inatutaka tumpige mawe tumwuue, lakini mpaka mwisho wa siku yesu hakumuua na waliomuhukumu waliondoka zao bila kumgusa, kama ni kulinganisha tungeanza na kujiuliza je waislamu mwanamke mzinzi anahukumiwaje?
pia kuna matendo yaliyofanyika yalioonekana yakivunja sabato lakini yesu akasema yeye ni bwana wa sabato(kama kula mashuke, kubeba kitanda).
pia kuna swala la kutoa talaka kwa mke yesu alionyesha kulipinga.je waislamu wanamtazamo sawa kuhusu talaka?,
vilevile swala la kuoa wake wengi(ndoa za mitaala, je yesu alisemaje kuhusu idadi ya wanawake wa kuoa na je waislamu wnachukuliaje idadi ya wanawake wa kuoa?
na ukiongezea na hili la ulaji wa nguruwe ukiweka neno la yesu aliposema si kimwingiacho mtu kinamtia unajisi bali kimtokacho kwani kile kimtokacho hupita na kwenda chooni...najua umeshasema kuwa unampenda yesu kwakuwa wewe ni mwislamu,na wakristo wanafuata alichofanya yesu na si kile tu wayahudi walikichukua katika mapokeo yao paradoxically yesu alisoma elimu ya kiyahudi pia. napata picha kuwa namna bibilia inavyotafsiriwa si vile kuran inatafsiriwa na ndio maana wakristo wengi wanakula nguruwe bila kujali andiko hilo linalodaiwa kukataza ulaji huu wa nyama ya nguruwe. naheshimu imani yako lakini najaribu kueleza kwanini wakristo hawajali hilo andiko na wanaendelea kula nguruwe kila kikicha.
wakristo wanamtumia yesu kama role model wao, ambapo yalioandikwa kwenye torati na sheria za musa alionesha kutofautiana nazo, na bibilia imezionyesha sheria zote na ajabu ni pale yesu aliposema hakuja kutangua torati bali kuitimiliza. na hapa ndipo tafsir inapoanzia kwani
mkuu lengo langu hapa ni kuonyesha kuwa namna ya kuitafsiri kuran ni tofauti na ile inayotumika kwenye bibilia. thats it.
yohana 10:34
34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); 36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu? 37 Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; 38 lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.