Great thinkers.... hivi vifo vyote ni mapenzi ya Mungu??

collezione

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
352
178
Leo naomba tujadili usalama wa maisha yetu.

1)Tuseme Umepanda basi unaelekea mwanza. Huko Barabarani hakuna sheria za uendeshaji high_way (na kama zipo hazifuatwi). Uko kwenye basi na dereva anakimbiza vibaya mno... Wakati huo huo tunajua mabasi mengi yanatumia matairi ya kichina ambayo sio imara (tanzania hakuna chombo kinachokagua, wamiliki wa mabasi watumie matairi gani, kwa usalama wa raia)... Punde basi likipinduka, watu wakafa. Hayo ni mapenzi ya Mungu????

2)Unaumwa tumbo. unaenda pharmacy kununua pain killers. Huko dukani pamejaa madawa feki na mengine yame-expire. Baada ya miaka michache unagundulika na cancer... Hayo ni mapenzi ya Mungu???

3) Wana_reseach wameandika, magari mabaovu Ndio chanzo cha magonjwa mengi yatokanayo na mfumo wa hewa. Kutokana na uchakavu wa injini. Moshi wa magari chakavu ni hatari kwa maisha ya binadamu.... Haya Unaishi Tanzania nchi ambayo haina sheria ya magari chakavu. Foleni ziko kila kona ya jiji la dar-es-Salaam... Hivi baada ya miaka kadhaa ukakutwa na cancer ya mapafu. Hayo ni mapenzi ya Mungu??

Hivi ndugu hatujiulizi kwa nini wazungu average wanaishi miaka mingi kuliko wa-Afrika????
Ukijiuliza hilo, utajua kwamba vifo vingi sisi waafrica tunaweza kuviepuka. Ila tatizo hakuna sheria, na mikakati ya kupunguza hivi vifo.

Wahisani, wanaleta misaada ya Malaria na ukimwi. Wajanja wanakula. Leo hii kila baada ya dakika Africa mtoto anakufa kwa Malaria. Hii nayo ni mipango ya Mungu????
 
Hii mada ni ya great thinkers tu au hata sie wengine tunaruhusiwa kuchangia?
 
If you are in JF. You are supposed to be a great thinker. And hii mada inatuhusu wote kwenye maisha yetu ya kila siku.
 
Mambo mengine yanaepukika kabisa basi tu ni uzembe wetu wenyewe kama hizo ajali za kila siku...naona hata Mungu atakuwa kashachoka kusikia malalamiko na lawama zetu kila mara ajali au vifo vikitokea ambavyo tungeweza kuzuia.
 
Leo naomba tujadili usalama wa maisha yetu.

1)Tuseme Umepanda basi unaelekea mwanza. Huko Barabarani hakuna sheria za uendeshaji high_way (na kama zipo hazifuatwi). Uko kwenye basi na dereva anakimbiza vibaya mno... Wakati huo huo tunajua mabasi mengi yanatumia matairi ya kichina ambayo sio imara (tanzania hakuna chombo kinachokagua, wamiliki wa mabasi watumie matairi gani, kwa usalama wa raia)... Punde basi likipinduka, watu wakafa. Hayo ni mapenzi ya Mungu????

2)Unaumwa tumbo. unaenda pharmacy kununua pain killers. Huko dukani pamejaa madawa feki na mengine yame-expire. Baada ya miaka michache unagundulika na cancer... Hayo ni mapenzi ya Mungu???

3) Wana_reseach wameandika, magari mabaovu Ndio chanzo cha magonjwa mengi yatokanayo na mfumo wa hewa. Kutokana na uchakavu wa injini. Moshi wa magari chakavu ni hatari kwa maisha ya binadamu.... Haya Unaishi Tanzania nchi ambayo haina sheria ya magari chakavu. Foleni ziko kila kona ya jiji la dar-es-Salaam... Hivi baada ya miaka kadhaa ukakutwa na cancer ya mapafu. Hayo ni mapenzi ya Mungu??

Hivi ndugu hatujiulizi kwa nini wazungu average wanaishi miaka mingi kuliko wa-Afrika????
Ukijiuliza hilo, utajua kwamba vifo vingi sisi waafrica tunaweza kuviepuka. Ila tatizo hakuna sheria, na mikakati ya kupunguza hivi vifo.

Wahisani, wanaleta misaada ya Malaria na ukimwi. Wajanja wanakula. Leo hii kila baada ya dakika Africa mtoto anakufa kwa Malaria. Hii nayo ni mipango ya Mungu????

Wale 'wenzetu' wanaamini hivyo.
 
Kifo ni MATAKWA ya muuaji. Kama huamini jijaribu mwenyewe kujiua uone matokeo. Ila EMOTIONS zinapenda tupooze mambo kidogo na kumlaumu maulana. Tunakufa kwa kuuana, au kwa majanga ya kiasili, FULUSTOP.
 
Mungu alipokupa akili ina maana mambo mengine alijitoa,sasa mtu anauza madawa feki au dereva anakimbia mwendo kasi hata sehemu mbaya Mungu anaingiaje hapo?

Mungu hushirikishwa haswa ktk natural disasters kama kimbunga,mafuriko,matetemeko nk. sasa hata hizi stori za mtu kalewa hadi kufa hapo Mungu tena Jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:heh:
 
Wale 'wenzetu' wanaamini hivyo.

Sio kila kitu ni mapenzi ya Mungu. Tusilitaje bure jina la BWANA Mungu wetu.

Kazi ya Serikali ni kutunga sera na kuzisimamia kuepuka haya matatizo yote, badala ya kuja kutuambia ni mapenzi ya Mungu.
 
If you are in JF. You are supposed to be a great thinker. And hii mada inatuhusu wote kwenye maisha yetu ya kila siku.

The operative words is "supposed". And why would you suppose everyone with access to JF is a great thinker? We have seen more than our fair share of great tinkerers and great sinkers up in here.

Halafu mi nilifikiri "Great Thinkers" hawatakiwi ku-suppose suppose tu?

Great thinkers my foot.
 
Mapenzi ya kukujaali kuwa mtanzania ungekuwa mzungu usingekutana na matairi ya kichina na dawa fake
 
'' Yeye ndiye aliyekuumbeni kwa udongo, kisha akaweka muda. Na muda huo maalum uko kwake. Juu ya haya (Makafiri) mnafanya shaka. Qur'an; 6:2.
'' Na maisha ya dunia si kitu ila mchezo tu na upuuzi. Na bila shaka nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wale wamchao. Basi hamtii akilini !? Qur'an: 6:32.
 
shetani huwa anataka upate mateso hapa duniani lakini mungu huwa anakupenda na kukupumzisha milele
 
'' Yeye ndiye aliyekuumbeni kwa udongo, kisha akaweka muda. Na muda huo maalum uko kwake. Juu ya haya (Makafiri) mnafanya shaka. Qur'an; 6:2.

Haha, kaka ngoja nikuulize swali.
Serikali za ki_Africa zinapokea misaada mingi sana kwa ajili ya kutokomeza Malaria.... Hakuna asiyefahamu Viongozi wetu wanakula hizo hela.

Matokeo yake, Afrika kila baada ya dakika tunapoteza watoto wadogo kutokana na ugonjwa wa malaria. Kiasi kwamba madawa hayo yangekuwa yanasambazwa ipasavyo. Vifo vya watoto vingepungua.

Hili pia unamsingizia Mungu???
 
......................... Juu ya haya mnafanya shaka !! Qur'an 6:32.
 
Back
Top Bottom