Good news kwa mashabiki wa yanga

OkSIR

Senior Member
Jun 3, 2009
108
1
Boban kuikosa Yanga, atimkia Sweden
broken-heart.jpg
Clara Alphonce

KIUNGO wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' kwa mara ya kwanza anaikosa mechi ya Yanga baada ya kuondoka jana kwenda Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutokea Nairobi Boban alisema kuwa anaenda kwenye majaribio Sweden kwa mwezi mmoja katika klabu ya Dakurd.

"Niko Nairobi hapa napumzika safari inaendelea tena jioni kwenda Sweden ndio hivyo bwana naikosa mechi hiyo da sina jinsi," alisema Boban.

Alisema kuwa anasikitika sana kuikosa mechi hiyo kwani alikuwa na hamu nayo kwani safari hii tumepania kuwafunga baada ya kushindwa kuwafunga katika msimu uliyopita.

Pamoja na hayo Boban alisema kuwa bado anaimani kubwa na kikosi cha Simba msimu huu na anaamini kuwa watashinda katika mechi hiyo ambayo inasubiliwa na mashabiki wa pande zate mbili.

Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa ameamua kuelekeza akili yake katika majaribio hayo iliaweze kufanya vizuri na kupata timu huo ya kuchezea.
 
sasa ina maana gani? Boban ndio mchezaji pekee simba au. wengine hawajui kucheza, acha kudhalilisha wachezaji wengine
 
Timu yetu kandambili ubingwa uliobaki ni kumfunga Simba tu
 
Yanga Imara wewe hata kama angekuwepo Nyama lazima auwawe!
Mnyama anatisha kutokuwepo kwa Haruna Moshi, kutatoa nafasi kwa wengine kama Ulimboka, Mrwanda, Uhuru nk yaani mwaka huu simba tume kamilika kila idara, hayo maneno yako utayameza Jmosi, msimu uliopita mlibebwa mkasawazisha dakika ya 98, safari hii sahau yaani hamna uwezo huo na mapro wenu 11...Nasikia mshaanza kudraft rufaa ya Uhuru seleman tena
 
yanga 2 vs simba 1 keep my words til 31st oct. 2009
Jidai unajua kutabili safari hii mwenye timu bora ndiyo atashinda siyo yebo yebo na maadalizi yake yazima moto halafu eti ashinde 2-1.....angalie kisije kuwa geuka mkaacha kupeleka timu uwanjani, maana ndiyo tabia yenu mkichungulia mkaona Mnyama 4 Yebo Yebo 1.
 
Acheze asicheze jumamosi mnyama anakula kibano tu,tena cha nguvu 3 bila!
 
Ushindi wa watoto wa Jangwani upo pale pale hatuna presha asubuhi hii nimewaona shule ya Jangwani pale wanapita toka mazoezini alafu wabaya wetu wanasema eti tumeenda Pemba wkt tupo jijini tunapiga tizi kama kawa.
 
Mimi nafurahi Maftah na Ojwang sijui Odhiambo wamefunguliwa maana kichapo lazima wakichezee. Bila hao wangeanza kusingizia ooh wachezaji wetu walifungiwa mara sijui canavaro. Yebo yebo mmpewa wachezaji wenu anzeni kuandaa bakora maana jumamosi hambebeki.
 
Muda ndiyo hiyo imewadia..Angurumapo Simba mcheza nani???Yebo Yebo kaeni tayari kula kichapo ya mwaka...sijui huyo mkikuyo wenu Ambani anajigamba ataanza kufunga dhidi ya mnyama...subutu kama atafanikiwa kupita hiyo ukuta ya simba na wala hamtutishi na hizo hela sijui milioni 20 zilizotengwa na fisadi Manji kuwapa timu iwapo watashinda.....na hata mkitaka refa achezeshe dakika 120, kichapo mtakula tu...
 
Back
Top Bottom