Godbless Lema: Makamu wa Rais si Mungu, ukiumwa sema, ukisafiri kikazi sema

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,313
Makamu wa Rais nakusalimu. Wewe sio makamu wa Rais wa familia yako.Wewe ni Makamu wa Rais wa Nchi.Watu wanapofuatilia taarifa zako wako sawa asilimia 100. Ukuonekana kwa muda mrefu na serikali na ofisi yako wakawa kimya,watu wakaanza huko wapi? Tena ni jambo jema kwako,nilifikiri ungefurahi badala yake nimekuona tofauti.

Wewe sio Mungu ukiumwa sema, ukisafiri kikazi sema.Cheo chako sio utakatifu. Wewe ni mfanyakazi wetu,uwe unatoa taarifa ya mienendo ya kazi zetu. Sasa umewashukuru waliokuwa wanakuombea, je,walikuwa wanakuombea kitu gani ?uwe na amani na afya njema.
Screenshot_2023-12-12-20-49-27-480_com.twitter.android-edit.jpg
 
Tatizo huyu Lema na wenzake wenye pigo kama zake wote ni wapuuzi, sababu Kairuki kwenye mkutano aliomwakilisha alisema Makamu yupo nje kikazi, sasa ni taarifa gani mnayotaka zaidi??

Lakini kwa jinsi walivyo mapunguani, wakadai hiyo ni danganya toto jamaa kashakata moto tuambiwe mapema, na yule kigogo akaropoka amemalizwa kwa sumu sijui na hila nyinginezo

Haya karudi mzima wote wamepoteana, punguzeni unaa
 
Mh Makamu wa Rais nakusalimu. Wewe sio makamu wa Rais wa familia yako.Wewe ni Makamu wa Rais wa Nchi.Watu wanapofuatilia taarifa zako wako sawa asilimia 100. Ukuonekana kwa muda mrefu na serikali na ofisi yako wakawa kimya,watu wakaanza huko wapi? Tena ni jambo jema kwako,nilifikiri ungefurahi badala yake nimekuona tofauti.

Wewe sio Mungu ukiumwa sema,ukisafiri kikazi sema.Cheo chako sio utakatifu. Wewe ni mfanyakazi wetu,uwe unatoa taarifa ya mienendo ya kazi zetu.Sasa umewashukuru waliokuwa wanakuombea, je,walikuwa wanakuombea kitu gani ?uwe na amani na afya njema.
Lema yuko sahihi
 
H

Safi kabisa NABII.
 
Tatizo huyu Lema na wenzake wenye pigo kama zake wote ni wapuuzi, sababu Kairuki kwenye mkutano aliomwakilisha alisema Makamu yupo nje kikazi, sasa ni taarifa gani mnayotaka zaidi??

Lakini kwa jinsi walivyo mapunguani, wakadai hiyo ni danganya toto jamaa kashakata moto tuambiwe mapema, na yule kigogo akaropoka amemalizwa kwa sumu sijui na hila nyinginezo

Haya karudi mzima wote wamepoteana, punguzeni unaa
Nakuunga mkono mkuu maana siyo kwa upuuzi wa Lema km alivyowahi kusema eti aliota kuwa mh flani kafia madarakani,watu hawakumchekea wakampeleka gerezani na kamwe ndoto yake haijawahi timia,mpuuzi kweli huyu jamaa.
 
Tatizo huyu Lema na wenzake wenye pigo kama zake wote ni wapuuzi, sababu Kairuki kwenye mkutano aliomwakilisha alisema Makamu yupo nje kikazi, sasa ni taarifa gani mnayotaka zaidi??

Lakini kwa jinsi walivyo mapunguani, wakadai hiyo ni danganya toto jamaa kashakata moto tuambiwe mapema, na yule kigogo akaropoka amemalizwa kwa sumu sijui na hila nyinginezo

Haya karudi mzima wote wamepoteana, punguzeni unaa
Kazi gani hiyo ya kumweka nje ya nchi mwezi mzima? Hata na wewe hauna jibu, labda useme alienda kusoma kama sio matibabu.
 
Nawashangaa sana watu wenye hasira wananchi wanapouliza kiongozi wao yupo wapii??

Kama uyu anayesema lema ni mpumbavu..... utafikiri yeye ni mtoto wa V.P....ana Stress tupu......hawa ndio wale chawa tena wasiolipwa...
 
Lema yupo sahihi, viongozi wetu wote Mara zote wanaposafiri kikazi nje ya nchi wananchi wanataarifiwa na hata ziara zao huko nje ya nchi tunaonyeshwa wanafanya nini huko nje.
Sasa huyu VP inakuwaje haonekani mwezi mzima bila taarifa yeyote Kwa wananchi.
Hata Baba wa Taifa Hayati Nyerere alopokuwa anakwenda UK Kwa matibabu/ckeck up wananchi tulotaarifiwa yeye amekuwa Nani tusitaarifiwe wakati anatumia fedha za wananchi
 
Acha awe anajifichaficha. Siku atakutana na wasio mtakia mema hukohuko mafichoni
 
Kazi gani hiyo ya kumweka nje ya nchi mwezi mzima? Hata na wewe hauna jibu, labda useme alienda kusoma kama sio matibabu.
Mbona tunakuwa wepesi kusahau hivi?? Kikwete alienda Marekani kikazi lakini baada ya kufanya check up ndio akafanyiwa ile operesheni??

Huo mwezi wenyewe sasa wanahesabu siku ya mwisho kuonekana hadharani, sasa ni mara ngapi Makamu au hata Rais mwenyewe huchukua mpaka siku kadhaa akiwa anaendelea na majukumu yake ya kiofisi mpaka hafla au shughuli ya kitaifa itokee
.
After all, ishu sio kutoonekana bali ni kuambiwa kuwa yupo nje kwa kazi maalum afu mnang'ang'ana kafa utafikiri mlishiriki kuntoa roho
 
Kwani Lema kaishia darasa la ngapi?
Kuna makosa ya kiuandishi mengi kwenye bandiko lake, makosa ambayo Mimi nisingeyafanya kipindi nilipokuwa kidato cha kwanza au darasa la saba.
Ukuonekana ❌
Hukuonekana ✔️.
Huko wapi ❌
Uko wapi ✔️.
 
Back
Top Bottom