Godbless Lema akamatwa Kajiado akitorokea Kenya yeye na familia yake. Kurudishwa nchini kesho Novemba 9, 2020

Godbless Lema akamatwa Kenya akitafuta hifadhi Ubalozi wa Marekani

Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiando nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Standard Media ya Kenya Lema alikuwa na mkewe, Neema Godbless na watoto wao watatu.Lema ameliambia gazeti hilo kuwa maafisa wa uhamiaji walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wake, kwa madai hadi wamuone Lema. Amesema mke wake alipomuita alikwenda lakini akawaambia hana hati yake ya kusafıria kwa sababu alikuwa hasafıri, na kwamba mke na wanae walikuwa wanakwenda kutafuta shule ya kimataifa Kenya.

Maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka, na Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake ambaye alisema kwamba angeendelea na safari yeye na watoto. Lakini mara tu alipovuka mpaka, Lema na familia yake waliingia ndani ya gari la mwanasheria wake, George Luchiri ambaye alikuwa akifuatilia mchakato mzima wa Lema kuvuka mpaka kuingia Kenya. Maafisa hao wa uhamiaji walitoa taarifa polisi kwamba kuna mtu ameingia nchini humo pasi na kuwa na nyaraka husika. "Polisi walitufuatilia na wakatukamata tukiwa Ilbisil na kutupeleka kwenye kituo cha polisi.

Sikutaka wamuweke Lema hapo kutokana na ukaribu wake na mpaka wa Tanzania," mwanasheria huyo ameiambiba The Standard Media.

Mwanasheria huyo amesema alifahamu kwamba Lema anakwenda Kenya na kwamba alitaka ampeleke Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHCR) mara tu atakapavuka mpaka.

Luchiri amesema kwa mujibu wa UNHCR mtu anayetafuta hifadhi hahitaji kuwa na nyaraka za kumuwezesha kuingia nchi nyingine. Akieleza sababu za kutokutoa hati yake ya kusafıria, Lema amesema alijua kwa kufanya hivyo, maafisa hao wangemshikilia na kumzuia kuvuka.

"Nimeacha kila kitu nyumbani. Hivyo havina umuhimu kwa sasa. Muhimu ni usalama wangu na usalama wa familia yangu. Nipo na wanangu Allbless, Brilliance na Terrence. Sijui kesho itakuja na nini. Kwa sasa natafuta hifadhi," Lema ameiambia The Standard. Mwanasheria huyo amesema atawasilisha taarifa za Lema katika Ubalozi wa Marekani kwani amekuwa akifanya mawasiliano na maafisa wa ubalozi huo.

Wakati hilo likitokea, aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu yupo Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam alipokwenda kuomba hifadhi akidai ametishiwa kuuawa.

Chanzo: swahilitimes
 
Binafsi nisichangie chochote kumhusu.

Ila tu. kama nchi yangu Tanzania ip katika hii hali wanasiasa wanayotaka kutuaminisha, tusingeshindwa kuingia mtaani na kuwaunga mkono.

Mbona hapa kitaa barida tu.
 
Lema ana madhara gani wajameni.?
~hana bunduki
~hana jeshi
~hata jiwe hana

au mdomo wake umekuwa kifaru?
 
Godbless Lema akamatwa Kenya akitafuta
hifadhi Ubalozi wa Marekani
Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema amekamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiando nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga. Kwa mujibu wa tovuti ya The Standard Media ya Kenya Lema alikuwa na mkewe, Neema Godbless na watoto wao watatu.Lema ameliambia gazeti hilo kuwa maafisa wa uhamiaji
walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wake, kwa madai hadi wamuone Lema. Amesema mke wake
alipomuita alikwenda lakini akawaambia hana hati yake ya kusafıria kwa sababu alikuwa hasafıri, na kwamba mke na wanae walikuwa wanakwenda kutafuta shule ya kimataifa
Kenya. Maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka, na Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake
ambaye alisema kwamba angeendelea na safari yeye na watoto. Lakini mara tu alipovuka mpaka, Lema na familia yake waliingia ndani ya gari la mwanasheria wake, George Luchiri ambaye alikuwa akifuatilia mchakato mzima wa Lema kuvuka mpaka kuingia Kenya. Maafisa hao wa uhamiaji walitoa taarifa polisi kwamba kuna
mtu ameingia nchini humo pasi na kuwa na nyaraka husika. "Polisi walitufuatilia na wakatukamata tukiwa Ilbisil na kutupeleka kwenye kituo cha polisi.Sikutaka wamuweke
Lema hapo kutokana na ukaribu wake na mpaka wa Tanzania," mwanasheria huyo ameiambiba The Standard Media.Mwanasheria huyo amesema alifahamu kwamba Lema anakwenda Kenya na kwamba alitaka ampeleke Tume ya Haki
za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHCR) mara tu atakapavuka mpaka.Luchiri amesema kwa mujibu wa UNHCR mtu anayetafuta hifadhi hahitaji kuwa na nyaraka za kumuwezesha kuingia nchi nyingine. Akieleza sababu za kutokutoa hati yake ya kusafıria, Lema amesema alijua kwa kufanya hivyo, maafisa hao wangemshikilia na kumzuia kuvuka.
"Nimeacha kila kitu nyumbani. Hivyo havina umuhimu kwa sasa. Muhimu ni usalama wangu na usalama wa familia yangu. Nipo na wanangu Allbless, Brilliance na Terrence. Sijui kesho itakuja na nini. Kwa sasa natafuta hifadhi," Lema
ameiambia The Standard. Mwanasheria huyo amesema atawasilisha taarifa za Lema
katika Ubalozi wa Marekani kwani amekuwa akifanya mawasiliano na maafisa wa ubalozi huo.
Wakati hilo likitokea, aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu yupo Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam alipokwenda kuomba hifadhi akidai ametishiwa kuuawa.

Chanzo: swahilitimes
Hivi tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa inaitwa UNHCR?
U= United
N= Nations
H= High
C= Commissioner for
R= Refugees
 
Kwani ni tabu sana kusema naipongeza ccm kwa ushindi halafu ukatulia zako ukalea familia?
Ataleaje familia sasa wakati kazi yake ni siasa? Akiipongeza CCM ndio anakuwa hana kazi tena sasa familia utailea mikono mitupu mkuu?

Lakini pia kwani tabu sana ilikuwa kwa wahusika kuondoa viashiria vya kuonesha uchaguzi umeporwa na kuionesha jamii kuwa uchaguzi uko huru?
 
Kweli?
Binafsi nisichangie chochote kumhusu.

Ila tu kama nchi yangu Tanzania ip katika hii hali wanasiasa wanayotaka kutuaminisha...tusingeshindwa kuingia mtaani na kuwaunga mkono.

Mbona hapa kitaa barida tu.
Hujaona ona hata mifano?
 
Kataka kutoka bila hati ya kusafiria.

Kawadanganya maafisa uhamiaji hana hati ilihali anayo. Inawezekana dhamira yake ilikuwa nzuri.

Lakini...mimi kama afisa uhamiaji nitakuruhusu vipi upite bila hati ilihali hakuna anayeruhusiwa kupita bila hati.

Na umeshanieleza wewe hauendi kabisa...unamtafutia mkeo na familia pesa za Kenya kisha urudi nyumbani????

Pole kwake.
 
Back
Top Bottom