babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 13,112
- 16,012
Gazeti pendwa la Amani linakwenda mbele zaidi kwa kueleza mkakati mzima, jinsi kituo hicho cha ngono cha vigogo, kilichopo ndani ya ofisi ya Massage Centre, iliyopo Kijitonyama, Dar es Salaam ilivyofanyiwa upepelelezi kwa miezi sita kabla ya kufumuliwa rasmi Jumamosi iliyopita (Septemba 26, 2009).
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi, Machi mwaka huu, kituo hicho cha uchuaji kilibainika kujihusisha na utoaji wa huduma ya ngono kwa siri na katika hilo, tahadhari ya hali ya juu ilichukuliwa.
Vyanzo vya awali vilipasha kwamba huduma ya ngono haikuwa na maelezo mapokezi, badala yake mteja akiwa chumbani anafanyiwa massage anaruhusiwa kunongona na mhudumu kisha kuongeza hela ili apate huduma ya jumla.
Ilielezwa pia kwamba kwa wateja wazoefu ambao walikwishawahi kuhudumiwa ngono kituoni hapo, walikuwa na uhuru wa kuulizia kamchezo hako hata mapokezi au kwa njia ya simu kwa sababu hawakuwa wakitiliwa shaka yoyote.
Kufuatia hali hiyo, chanzo chetu kilibainisha kwamba kwa mteja mzoefu alipotaka kuhudumiwa ngono, alipofika mapokezi aliulizia full massage, kauli ambayo ilieleweka vizuri kwa mhudumu.
Aidha, uchunguzi ulibaini kwamba kwa mteja wa full massage, alikuwa akipewa upendeleo zaidi kwa kuwa fedha anazolipa ni nyingi ambazo zinakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ya mhudumu wakati kwa huduma ya massage, kiasi kikubwa ni cha mmiliki.
Kutokana na data hizo, Machi mwaka huu, kitengo cha waandishi wa habari za uchunguzi kwenye Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, kilituma mtu ndani ya kituo hicho na kuambulia majibu hasi.
Mchunguzi huyo wa Global ambayo inachapisha magazeti ya Amani, Uwazi, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda na Championi, alipofika kituoni hapo aliulizia huduma ya full massage lakini wahudumu walimtolea nje kwamba hakuna biashara ya ngono wanayoifanya.
Kutokana na majibu hayo, kitengo hicho cha habari za uchunguzi kilituma watu wengine watatu kwa nyakati tofauti ambao waliingia kwenye kituo hicho na kugundua kuwa, biashara hiyo ilikuwa inafanyika ndani kwa ndani, pengine bila hata mmiliki kujua.
Katika ripoti ya wachunguzi hao ndani ya kituo hicho, ilibainika kuwa watu ambao huingia kwenye jengo hilo la massage na kupata huduma ya ngono wengi wao ni vigogo kwa sababu ndiyo wanaoweza kumudu gharama.
Ilibainika pia kwamba watumishi wenye hadhi kubwa serikalini, wafanyakazi kwenye taasisi zinazolipa mishahara mikubwa na wafanyabiashara wakubwa au mapedeshee ndiyo ambao huingia kwa kificho kwenye kituo hicho na kupata huduma ya full massage.
Kutokana na kukusanya vielelezo hivyo, kitengo hicho cha habari za uchunguzi kiliwasiliana na Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam na kuandaa mikakati ya kukifumua kituo hicho cha ngono cha vigogo.
Katika mkakati wa pamoja kati ya Polisi Oysterbay na kitengo cha habari za uchunguzi cha Kampuni ya Global, alipangwa mtu kuingia ndani ya kituo hicho kama mhudumiwa wa full massage ambaye alitakiwa kubip simu ya kiongozi wa msafara pale mambo yatakapoiva.
Sanjari na infoma huyo, kitengo hicho cha habari za uchunguzi kilipandikiza mtu ndani ya kituo hicho ambaye alikuwa akivijisha taarifa za hali ya mambo yanayoendelea hatua kwa hatu.
Kwa kawaida, kituo hicho hufunguliwa asubuhi na kufanyakazi mpaka saa 2 jioni na katika siku hiyo ya oparesheni, ilipofika saa 1:57 jioni, infoma aliingia ndani na kuomba huduma ya fulla massage.
Saa 2:09 jioni, eneo lote la Stendi ya Makumbusho lilikuwa chini ya askari wa kutosha, waliovaa kijeshi na wengine kiraia na ilipofika saa 2:21, infoma alibipu hivyo kuonesha kwamba chumbani mambo yalikuwa yamekwishaiva.
Ilipofika saa 2:30, kituo chote kilikuwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi ambapo wahudumu wawili walikutwa wakiwa uchi kama walivyozaliwa vyumbani, hali iliyotoa picha ya wazi kuwa, walikuwa wakitoa huduma ya full massage kwa wateja.
Katika uvamizi huo, mbali na infoma aliyepandikizwa na kitengo cha habari za uchunguzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi, alikutwa mteja mwingine halisi aliyenaswa chumbani na mhudumu, wote wakiwa watupu kama walivyozaliwa.
Baada ya kamata kamata, iliyochukua dakika kadhaa, polisi waliwakamata wahudumu waliokutwa uchi vyumbani wakiwa kwenye taswira ya kutoa huduma ya ngono kwa wateja wao. Habari kutoka Oysterbay Dar es Salaam juzi, zilisema kuwa wahudumu waliokutwa uchi vyumbani tayari wamepelekwa kwenye Mahakama ya Jiji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
KUTOKA KWA MHARIRI Lengo la Kampuni ya magazeti ya Global kufuatilia uovu unaofanyika kwenye massage centre jijini Dar ni kuhakikisha jamii inaishi kwa maadili mema na kuepuka maambukizi ya gonjwa hatari la Ukimwi.
Aidha, Global inalipongeza jeshi la polisi nchini, mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Kamanda wa mkoa huo, Mark Karunguyeye, OC-CID, Damas Nyanda, Inspekta Peter Ngeni na wengine wote kwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kufanikisha zoezi hilo na mengine yaliyotangulia.

Last edited: