Naomba kujuzwa kuhusu Kampuni ya Global Alliance

Mkuu, anaeijua kampuni inyoitwa Global Alliance anijuze, naona walinipigia simu nifike kwenye interview yao wanfanyia Kibo palace Arusha, kwa anaejua baadhi ya maswali wanoweza kutoa. Mimi nina BSc. Marketing Management
Hao ndio matangazo yao wanaweka kwenye nguzo za umeme, mshahara laki 3 😅.

Nenda mkuu na degree yaki ukatembeze vipodozi.
 
Wamekuita kwenye interview maana yake ulifanya application? Ulifanya application kwenye kampuni ambayo hujui inajihusisha na Nini?

Kama hukufanya application basi watakua matapeli wanatumia jina la global alliance ili wakupige na kitu kizito kichwani
 
Nilichukua namba kwa nguzo ya umeme
Wala usijichoshe na maswali kule inaangaliwa nguvu zako za kuhimili kuswampa na madishi ya vyombo 🤣🤣🤣🤣

Kuna uzi mmoja hivi wa member mmoja nikiuona nitakutag usome, km sio humu basi niliuona twitter 😂
 
Hivi unaweza kuomba kazi kwenye Kampuni hata hujui wanahusika na nini? Hivi chuo si umeenda wewe? Sasa unaombaje kazi kwenye kampuni hata hujui wana fanya nini? Una tatizo wewe kwanza, achana na kampuni husika, sbb hao kazi zao za hovyo, sio ajira hiyo, utatembea kwa miguu kusambaza vipodozi feki mwishowe ukamatwe bure..!!

Ila nimeshangaa sana hadi uombe kazi kwenye kampuni bila hata kujua ipo au ni feki au inahusika na nini, hii ni hatari sana
 
kwa kifupi hakuna ajira hapo... nawajua hao watu vizuri wana kidada cha korea wanatembea nacho ili kushawishi watu wawekeze pesa... kwaajili ya bidhaa zao...

pesa yako ina windwa kwa hali na mali... wanajidai mamilionea ila ajabu kwenye vikao vya hata maji tu wanashindwa kuweka...!

hakuna ajira hapo...!​
 
Mkuu, anaeijua kampuni inyoitwa Global Alliance anijuze, naona walinipigia simu nifike kwenye interview yao wanfanyia Kibo palace Arusha, kwa anaejua baadhi ya maswali wanoweza kutoa. Mimi nina BSc. Marketing Management

Mkuu, anaeijua kampuni inyoitwa Global Alliance anijuze, naona walinipigia simu nifike kwenye interview yao wanfanyia Kibo palace Arusha, kwa anaejua baadhi ya maswali wanoweza kutoa. Mimi nina BSc. Marketing Management
Nimemkumbuka jamaa yangu ghafla baada ya kuona kitu "Global Alliance".
Pesa hizi bhana
 
Mtoa Mada anaingia Global Alliance akiwa na sendoz
images (9).jpeg

Miaka mitano baadae.. kavaa kaunda (wa kulia kabisa)

images (10).jpeg
 
Nenda ukiwa umeandaa na 30,000 ya fomu,alafu utaambiwa hii sio ajira ni fursa.
Uanze semina za asubuhi mpaka jion kufundishwa namna ya kwenda kuomba pesa kwa watu wako wa karibu ili ukawekeze kwao.
Kuwa Makin Sana Mkuu io sio ajira na haina interview.
Wulize kwanza nakuja kufanya kazi gan na nitakuwa kitengo kipi kama watakujibu..bali watasema wewe njoo utajua huku huku
 
Mkuu, anaeijua kampuni inyoitwa Global Alliance anijuze, naona walinipigia simu nifike kwenye interview yao wanfanyia Kibo palace Arusha, kwa anaejua baadhi ya maswali wanoweza kutoa. Mimi nina BSc. Marketing Management
Global alliance ni networking business...... yaaani utapeli .....utaambiwa sijui kuunganisha watu kushoto kulia .....mara kuuza product zao wanakuzabua kiiingilio laki 600000 sijui

KUWA MAKINI HAKUNA UTAJIR WA HARAKA SO UKIFIKA HUKO WATAKUHADAHAA NA WATU WA UONGO ETI WALIO FANIKIWA KUPITIA GLOBAL ALLIANCE MARA NYINGI WATU HAO UPANGWA

nini ufanye bora usiende kama akili yako ni ya kuku yaani uwezo wako wa kuchanganua mambo ni mdogo maana hao watu wana high convincing power ya kitapeli mara nyingi kama huna hela wanakushauri ukope hata kwa ndugu au jamaa

Pia watu hawa hupenda kufanyia mijadala yao ya kitapeli kwenye hotel zenye hadhi au kumbi za gharama ili kuaminisha utapeli wao pia huja na magari ya gharama ILA NI PONZI SCHEME

NARUDIA TENA VIJANA WOTE HUMU NETWORKING BUSINESS NI UTAPELI UNLESS WEWE NDO MSIKA DAU YAANI WEWE UPO KWENYE CHAIN YA KUTAPELI WATU
 
Back
Top Bottom