Gharama za Sensa!!!

Elisha Ray

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
323
94
Wakuu, leo nimesikia news ambazo zimenipa kichefuchefu kwa kweli na kama ni za kweli basi hii nchi imejaa watu wezi na wanaiba kuliko tujuavyo huko serikalini. Kuna wahasibu wawili ndugu zangu wanaofanya kazi serikalini ambao walishiriki kutengeneza bajeti ya sensa na wameniambia kuwa malipo (posho) ya wale wanaotumika kufanya kazi ya kuhesabu watu ni shs 3,500,000/- kwa mtu mmoja kama posho yao mpaka wakimaliza ambayo ni sawa na 500,000/ kwa siku. Sasa ninachojua mimi ni kuwa kuna wanaolipwa 50,000/- na wengine 35,000/- kwa siku na hawa wahasibu walinipa bajeti kwa nyakati tofauti na wakashangaa nilipowaambia malipo ya hawa jamaa wanayolipwa kwa siku kuwa sio ilivyo kwenye bajeti. Kuna anaejua kama hii ni kweli wadau mnaojua hili maana ni WIZI MTUPU kila kona katika serikali hii ya ba nanihii......
 
Back
Top Bottom