Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,065
- 22,758
- Thread starter
- #41
Lililotatanisha zaidi ni kwamba safari ya Spika Job Ndugai huko India ilifichwa hadi wananchi walipoanza kupaza sauti na kuanza kuulizia alipo spika. Ni hapo ndipo Katibu wa Bunge wakati huo Bw. Thomas Kashililah alipojitokeza na kusema Spika yuko nje ya nchi kwa uchunguzi wa afya yake bila kusema yuko nchi gani wala kinachomsumbua.
Wananchi walipozidi kudadisi, Bw. Kashililah alidai kwamba Bw. Ndugai yuko nje kwa uchunguzi tu na kwamba mtu yeyote anaweza kumpigia simu na kuongea naye na kwamba hii ilikuwa ni safari ya pili kwenda kwa madhumuni hayo hayo. Na kweli gazeti la Mwananchi ilipopiga simu ilipokelewa na Ndugai mwenyewe na kukiri yuko India...
Safari ya kwanza kwenda kutibiwa ilikuwa ni siri kubwa na hadi leo ufafanuzi wa kueleweka haujawahi kutolewa...maajabu! Safari siri, Ugonjwa siri, gharama ya matibabu siri...yani kodi zetu zinatumika kisirisiri!